< Luka 20 >
1 Ikawa siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu Hekaluni na kuhubiri injili, makuhani wakuu na walimu wa Sheria walimwendea pamoja na wazee.
2 Walizungumza, wakimwambia, 'Tuambie ni kwa mamlaka gani unafanya mambo haya? Au ni nani huyo ambaye amekupa mamlaka haya? “
3 Naye akajibu, akawaambia, 'Nami pia nitawauliza swali. Niambieni
4 ubatizo wa Yohana. Je, ulitoka mbinguni ama kwa watu? '
5 Lakini wakajadiliana wao kwa wao, wakisema, 'Tukisema, `litoka mbinguni, atatuuliza, ` Basi, mbona hamkumwamini?'
6 Na tukisema; ilitoka kwa wanadamu; watu wote hapa watatupiga mawe, maana wote wanaamini kwamba Yohana alikuwa nabii. '
7 Basi, wakamjibu ya kwamba hawakujua ilikotoka.
8 Yesu akawaambia, '“Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.”
9 Aliwaambia watu mfano huu, “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima wa mizabibu, na akaenda nchi nyingine kwa muda mrefu.
10 Kwa muda uliopangwa, alimtuma mtumishi kwa wakulima mizabibu, kwamba wampe sehemu ya matunda ya shamba la mizabibu. Lakini wakulima wa mzabibu wakampiga, wakamrudisha mikono- mitupu.
11 Kisha akamtuma tena mtumishi mwingine na nao wakampiga, kumtendea vibaya, na wakamrudisha mikono- mitupu.
12 Alimtuma tena wa tatu na nao wakamjeruhi na kumtupa nje.
13 Hivyo bwana wa shamba akasema, 'Nitafanya nini? Nitamtuma mwanangu mpendwa. Labda watamheshimu. '
14 Lakini wakulima wa mzabibu walipomwona, walijadili wao kwa wao wakisema, `Huyu ndiye mrithi. Tumuue, ili urithi wake uwe wetu. '
15 Wakamtoa nje ya shamba la mizabibu na kumuua. Je bwana shamba atawafanya nini?
16 Atakuja kuwaangamiza wakulima wa mzabibu, na atawapa shamba hilo wengine”. 'Nao waliposikia hayo, wakasema, 'Mungu amekataa'
17 Lakini Yesu akawatazama, akasema, “Je andiko hili lina maana gani? 'Jiwe walilolikataa wajenzi, limekuwa jiwe la pembeni'?
18 Kila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo, atavunjika vipande vipande. Lakini yule ambaye litamwangukia, litamponda. '
19 Hivyo waandishi na wakuu wa makuhani walitafuta njia ya kumkamata wakati huohuo, walijua kwamba alikuwa amesema mfano huu dhidi yao. Lakini waliwaogopa watu.
20 Walimuangalia kwa makini, wakatuma wapelelezi waliojifanya kuwa watu wa haki, ili wapate kupata kosa kwa hotuba yake, ili kumpelekakwa watawala na wenye mamlaka.
21 Nao wakamwuliza, wakisema, “Mwalimu, tunajua kwamba unasema na kufundisha mambo ya kweli na si kushawishiwa na mtu yeyote, lakini wewe hufundisha ukweli kuhusu njia ya Mungu.
22 Je, ni halali kwetu kulipa kodi kwa Kaisari, au la?”
23 Lakini Yesu alitambua mtego wao, akawaambia,
24 “Nionyesheni dinari. Sura na chapa ya nani ipo juu yake?” Walisema, '“Ya Kaisari.”
25 Naye akawaambia, 'Basi, mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari, na Mungu yaliyo yake Mungu.'
26 Waandishi na wakuu wa makuhani hawakuwa na uwezo wa kukosoa kile alichosema mbele ya watu. Wakastaajabia majibu yake na hawakusema chochote.
27 Baadhi ya Masadukayo wakamwendea, wale ambao wanasema kwamba hakuna ufufuo,
28 wakamwuliza, wakisema, “Mwalimu, Musa alituandikia kwamba kama mtu akifiwa na ndugu mwenye mke ambaye hana mtoto basi anapaswa kumchukuna mke wa ndugu yake na kuzaa nae kwa ajili ya kaka yake.
29 Kulikuwa na ndugu saba Wa kwanza alioa, akafa bila kuacha mtoto,
30 na wa pili pia.
31 Wa tatu akamchukua vilevile, vivyo hivyo wa saba hakuacha watoto na akafa.
32 Baadaye yule mwanamke pia akafa.
33 Katika ufufuo atakuwa mke wa nani? Maana wote saba walikuwa wamemwoa. '
34 Yesu akawaambia, “Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa. (aiōn )
35 Lakini wale wanastaohili kupokea ufufuo wa wafu na kuingia uzima wa milele hawaoi wala hawaolewi. (aiōn )
36 Wala hawawezi kufa tena, kwa sababu huwa sawasawa na malaika na ni watoto wa Mungu, wana wa ufufuo.
37 Lakini hiyo wafu wanafufuliwa, hata Musa alionyesha mahali katika habari za kichaka, pale alimwita Bwana kama Mungu wa Ibrahimu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.
38 Sasa, yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai, kwa sababu wote huishi kwake. “
39 Baadhi ya walimu wa Sheria wakamjibu, 'Mwalimu, umejibu vema. '
40 Hawakuthubutu kumwuliza maswali mengine zaidi.
41 Yesu akawaambia, “Ki vipi watu wanasema kwamba Kristo ni mwana wa Daudi?
42 Maana Daudi mwenyewe anasema katika Zaburi: Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti mkono wa kulia,
43 mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako. '
44 Daudi anamwita Kristo 'Bwana', basi atakuwaje mwana wa Daudi?”
45 Watu wote walipokuwa wakimsikiliza akawaambia wanafunzi wake,
46 'Jihadharini na waandishi, wapendao kutembea wamevaa mavazi marefu, na wapenda salamu maalum sokoni na viti vya heshima katika masinagogi, na maeneo ya heshima karamuni.
47 Wao pia hula nyumba za wajane, na wanajifanya wanasali sala ndefu. Hawa watapokea hukumu kubwa zaidi. '