< Luka 2 >
1 Sasa katika siku hizo, ikatokea kwamba Kaisari Agusto alitoa agizo akielekeza kwamba ichukuliwe sensa ya watu wote wanaoishi duniani.
2 Hii ilikuwa ni sensa ya kwanza iliyofanyika wakati Krenio akiwa gavana wa Siria.
3 Hivyo kila mmoja akaenda mjini kwake kuandikishwa sensa.
4 Naye Yusufu aliondoka pia katika mji wa Nazareti huko Galilaya na akasafiri Yudea katika mji wa Bethlehemu, ujulikanao kama mji wa Daudi, kwa sababu alitokea katika ukoo ya Daudi.
5 Alikwenda huko kujiandikisha pamoja na Mariamu, ambaye alikuwa amemposa na alikuwa akitazamia mtoto.
6 Sasa ilitokea kwamba, wakiwa kule wakati wake wa kujifungua mtoto ukawadia.
7 Akajifungua mtoto wa kiume, mzaliwa wake wa kwanza, akamzungushia nguo mwilini kumkinga na baridi mtoto. Ndipo akamweka kwenye kihori cha kulishia wanyama, kwa sababu haikuwepo nafasi kwenye nyumba za wageni.
8 Katika eneo hilo, walikuwapo wachungaji walioishi mashambani wakilinda makundi ya Kondoo wao usiku.
9 Ghafla, malaika wa Bwana akawatokea, na utukufu wa Bwana ukang'aa kuwazunguka, na wakawa na hofu sana.
10 Ndipo malaika akwaambia, “Msiogope, kwasababu nawaletea habari njema ambayo italeta furaha kuu kwa watu wote.
11 Leo Mwokozi kazaliwa kwaajili yenu mjini mwa Daudi! Yeye ndiye Kristo Bwana!
12 Hii ndiyo ishara ambayo mtapewa, mtamkuta mtoto amefungwa nguo na amelala kwenye hori la kulishia wanyama.”
13 Ghafla kukawa na jeshi kubwa la mbinguni likaungana na malaika huyo wakamsifu Mungu, wakisema,
14 “Utukufu kwa Mungu aliye juu sana, na amani iwe duniani kwa wote ambao anapendezwa nao.”
15 Ikawa kwamba malaika walipokwisha kuondoka kwenda mbinguni, wachungaji wakasemezena wao kwa wao, “Twendeni sasa kule Bethlehemu, na tukaone hiki kitu ambacho kimetokea, ambacho Bwana ametufahamisha.”
16 Wakaharakisha kule, na wakamkuta Mariamu na Yusufu, na wakamuona mtoto amelala kwenye hori la kulishia wanyama.
17 Na walipoona hivi, wakawajulisha watu kile walichokuwa wameambiwa kumhusu mtoto.
18 Wote waliosikia habari hii wakashangazwa na kile kilichosemwa na wachungaji.
19 Lakini Mariamu akaendelea kufikiri kuhusu yote aliyokwisha kuyasikia, akiyatunza moyoni mwake.
20 Wachungaji wakarudi wakimtukuza na kumsifu Mungu kwa ajili ya kila kitu walichokwisha sikia na kuona, kama tu ilivyokuwa imenenwa kwao.
21 Ilipofika siku ya nane na ilikuwa ni wakati wa kumtahiri mtoto, wakamwita jina Yesu, jina alilokwishapewa na yule malaika kabla mimba haijatungwa tumboni.
22 zao zilizotakiwa za utakaso zilipopita, kulingana na sheria ya Musa, Yusufu na Mariamu wakampeleka hekaluni kule Yerusalemu kumweka mbele za Bwana.
23 Kama ilivyoandikwa katika sheria ya Bwana, “Kila mwanaume anayefungua tumbo ataitwa aliyetolewa wakfu kwa Bwana.”
24 Wao vilevile walikuja kutoa sadaka kulingana na kile kinachosemwa katika sheria ya Bwana, “Jozi ya njiwa au makinda mawili ya njiwa.”
25 Tazama, palikuwa na mtu katika Yerusalemu ambaye jina lake alikuwa akiitwa Simeoni. mtu huyu alikuwa mwenye haki na mcha Mungu. Yeye alikuwa akisubiri kwa ajili ya mfariji wa Israeli, na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.
26 Ilikuwa imekwisha funuliwa kwake kupitia Roho Mtakatifu kwamba yeye hangelikufa kabla ya kuwomwona Kristo wa Bwana.
27 Siku moja alikuja ndani ya hekalu, akiongozwa na Roho Mtakatifu. Ambapo wazazi walimleta mtoto, Yesu, kumfanyia yale yaliyopasa kawaida ya sheria,
28 ndipo Simeoni alimpokea mikononi mwake, na akamsifu Mungu na kusema,
29 “Sasa ruhusu mtumishi wako aende kwa amani Bwana, kulingana na Neno lako.
30 Kwa kuwa macho yangu yameuona wakovu wako,
31 ambao umeonekana kwa macho ya watu wote.
32 Yeye ni nuru kwa ajili ya ufunuo kwa Wamataifa na utukufu wa watu Israeli.”
33 Baba na Mama wa mtoto walishangazwa kwa mambo ambayo yalizungumzwa juu yake.
34 Ndipo Simeoni akawabariki na akasema kwa Mariamu mama yake, “Sikiliza kwa makini! Mtoto huyu atakuwa sababu ya kupotea na kuokoka kwa watu wengi katika Israeli na ni ishara ambayo watu wengi wataipinga.
35 Pia ni upanga utakaochoma nafsi yako mwenyewe, ili kwamba mawazo ya mioyo ya wengi yadhihirike”.
36 Nabii mwanamke aliyeitwa Ana pia alikuwako hekaluni. Yeye alikuwa binti wa Fanueli kutoka kabila la Asheri. Alikuwa na miaka mingi sana. Naye aliishi na mume wake kwa miaka saba baada ya kuoana,
37 na ndipo akawa mjane kwa miaka themanini na minne. Naye hakuwahi kuondoka hekaluni na alikuwa akiendelea kumwabudu Mungu pamoja na kufunga na kuomba, usiku na mchana.
38 Na kwa wakati huo, alikuja pale walipo akaanza kumshukuru Mungu. Aliongea kumhusu mtoto kwa kila mtu ambaye alikuwa akisubiri ukombozi wa Yerusalemu.
39 Walipomaliza kila kitu walichotakiwa kufanya kuligana na na sheria ya Bwana, walirudi Galilaya, mjini kwao, Nazareti.
40 Mtoto alikua, na akawa na nguvu, akiongezeka katika hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.
41 Wazazi wake kila mwaka walikwenda Yerusalemu kwaajili ya sikukuu ya Pasaka.
42 Alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, walikwenda tena wakati mwafaka kidesturi kwa ajili ya sikukuu.
43 Baada ya kubaki siku zote kwa ajili ya sikukuu, walianza kurudi nyumbani. Lakini mvulana Yesu alibaki nyuma mle Yerusalemu na wazazi wake hawakujua hili.
44 Walidhani kwamba yumo kwenye kundi walilokuwa wakisafiri nalo, hivyo walisafiri safari ya siku. Ndipo wakaanza kumtafuta miongoni wa ndugu na marafiki zao.
45 Waliposhindwa kumpata, walirudi Yerusalemu na wakaanza kumtafuta humo.
46 Ikatokea kwamba baada ya siku tatu, wakampata hekaluni, akiwa ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.
47 Wote waliomsikia walishangazwa na ufahamu wake na majibu yake.
48 Walipomwona, walistaajabu. Mama yake akamwambia, “Mwanangu, kwa nini umetutendea hivi? Sikiliza, baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa wasiwasi mkubwa.”
49 Akawaambia, “Kwa nini mmekuwa mkinitafuta? Hamkujua kwamba lazima niwe kwenye nyumba ya Baba yangu?
50 Lakini hawakuelewa nini alichomaanisha kwa maneno hayo.
51 Ndipo akaenda pamoja nao mpaka nyumbani Nazareti na alikuwa mtii kwao. Mama yake alihifadhi mambo yote moyoni mwake.
52 Lakini Yesu aliendelea kukua katika hekima na kimo, na akazidi kupendwa na Mungu na watu.