< Luka 15 >
1 Basi watoza ushuru wote na wengine wenye dhambi walikuja kwa Yesu na kumsikiliza.
Now all the tax collectors and sinners were gathering around to listen to Jesus.
2 Mafarisayowaote na waandishi wakanung'unika wakisema, “Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi na hata hula nao.”
So the Pharisees and scribes began to grumble: “This man welcomes sinners and eats with them.”
3 Yesu akasema mfano huu kwao, akisema
Then Jesus told them this parable:
4 “Nani kwenu, kama ana kondoo mia moja na akipotelewa na mmoja wao, hatawaacha wale tisini na tisa nyikani, na aende akamtafute yule aliyepotea hadi amwone?
“What man among you, if he has a hundred sheep and loses one of them, does not leave the ninety-nine in the pasture and go after the one that is lost, until he finds it?
5 Naye akisha kumpata humweka mabegani pake na kufurahia.
And when he finds it, he joyfully puts it on his shoulders,
6 Afikapo kwenye nyumba, huwaita rafiki zake na jirani zake akawaambia furahini pamoja nami, kwa kuwa nimempata kondoo wangu aliyepotea.'
comes home, and calls together his friends and neighbors to tell them, ‘Rejoice with me, for I have found my lost sheep!’
7 nawaambia vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, zaidi ya wenye haki tisini na tisa ambao hawana haja ya kutubu
In the same way, I tell you that there will be more joy in heaven over one sinner who repents than over ninety-nine righteous ones who do not need to repent.
8 Au kuna mwanamke gani mwenye sarafu kumi za fedha, akipotewa na sarafua moja, hata washa taa na kufagia nyumba na kutafuta kwa bidii hadi atakapoipata?
Or what woman who has ten silver coins and loses one of them does not light a lamp, sweep her house, and search carefully until she finds it?
9 Na akiisha kuiona huwaita rafiki zake na jirani zake akawaambia furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena sarafu yangu niliyokua nimeipoteza.
And when she finds it, she calls together her friends and neighbors to say, ‘Rejoice with me, for I have found my lost coin.’
10 Hata hivyo nawaambia kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.”
In the same way, I tell you, there is joy in the presence of God’s angels over one sinner who repents.”
11 Na Yesu akasema, “Mtu mmoja alikua na wana wawili
Then Jesus said, “There was a man who had two sons.
12 yule mdogo akamwambia babaye, Baba nipe sehemu ya mali inayonistali kuirithi. Hivyo akagawanya mali zake kati yao.
The younger son said to him, ‘Father, give me my share of the estate.’ So he divided his property between them.
13 Siku si nyingi yule mdogo akakusanya vyote anavyomiliki akaenda nchi ya mbali, na huko akatapanya hela zake, kwa kununua vitu asivyo vihitaji, na kutapanya fedha zake kwa anasa.
After a few days, the younger son got everything together and journeyed to a distant country, where he squandered his wealth in wild living.
14 Nae alipokua amekwisha tumia vyote njaa kuu iliingia nchi ile naye akaanza kuwa katika uhitaji.
After he had spent all he had, a severe famine swept through that country, and he began to be in need.
15 Akaenda na kujiajiri mwenyewe kwa mmoja wa raia wa nchi ile, naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe.
So he went and hired himself out to a citizen of that country, who sent him into his fields to feed the pigs.
16 Na akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe kwa sababu hakuna mtu aliempa kitu chochote apate kula.
He longed to fill his belly with the pods the pigs were eating, but no one would give him a thing.
17 Ila yule mwana mdogo alipozingatia moyoni mwake, alisema 'ni watumishi wangapi wa baba yangu wanachakula kingi cha kutosha na mimi niko hapa, ninakufa na njaa!
Finally he came to his senses and said, ‘How many of my father’s hired servants have plenty of food? But here I am, starving to death!
18 Nitaondoka na kwenda kwa baba yangu, na kumwambia, “Baba nimekosa juu ya mbingu na mbele ya macho yako.
I will get up and go back to my father and say to him, “Father, I have sinned against heaven and against you.
19 Sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.”
I am no longer worthy to be called your son. Make me like one of your hired servants.”’
20 Ndipo akaondoka akaenda kwa baba yake. Alipokua angali mbali baba yake alimuona akamwonea huruma akaenda mbio na kumkumbatia na kumbusu.
So he got up and went to his father. But while he was still in the distance, his father saw him and was filled with compassion. He ran to his son, embraced him, and kissed him.
21 Yule mwana akamwambia, 'baba nimekosa juu ya mbingu na mbele ya macho yako sistahili kuitwa mwana wako.'
The son declared, ‘Father, I have sinned against heaven and against you. I am no longer worthy to be called your son.’
22 Yule baba aliwaambia watumishi wake, 'lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike mtieni na pete kidoleni na viatu miguuni.
But the father said to his servants, ‘Quick! Bring the best robe and put it on him. Put a ring on his finger and sandals on his feet.
23 Kisha mleteni ndama yule alienona mkamchinje tule na kufurai.
Bring the fattened calf and kill it. Let us feast and celebrate.
24 Kwa kuwa mwanangu alikua amekufa naye yu hai. Alikua amepotea nae ameonekana wakaanza kushangilia.
For this son of mine was dead and is alive again! He was lost and is found!’ So they began to celebrate.
25 Basi yule mwanae mkubwa alikuwako shamba. Alipokuwa akija na kuikaribia nyumba alisikia sauti ya nyimbo na michezo.
Meanwhile the older son was in the field, and as he approached the house, he heard music and dancing.
26 Akaita mtumishi mmoja akamuuliza mambo haya maana yake nini?
So he called one of the servants and asked what was going on.
27 Mtumishi akamwambia mdogo wako amekuja na baba yako amemchinjia ndama aliyenona kwa sababu amerudi salama.'
‘Your brother has returned,’ he said, ‘and your father has killed the fattened calf, because he has him back safe and sound.’
28 Mwana mkubwa akakasirika akakataa kuingia ndani na babaye alitoka nje kumsihi.
The older son became angry and refused to go in. So his father came out and pleaded with him.
29 Ila akamjibu babayake akisema, 'Tazama mimi nimekutumikia miaka mingi, wala sijakosa amri yako, lakini hujanipa mwana mbuzi, ili niweze kusherehekea na rafiki zangu.
But he answered his father, ‘Look, all these years I have served you and never disobeyed a commandment of yours. Yet you never gave me even a young goat so I could celebrate with my friends.
30 Lakini alipokuja huyu mwana wako aliyetapanya mali yako yote pamoja na makahaba umemchinjia ndama alienona.
But when this son of yours returns from squandering your wealth with prostitutes, you kill the fattened calf for him!’
31 Baba akamwambia, 'Mwanangu, wewe u pamoja nami siku zote na vyote nilivyo navyo ni vyako.
‘Son, you are always with me,’ the father said, ‘and all that is mine is yours.
32 Ila ilikua vyema kwetu kufanya sherehe na kufurahi, huyu ndugu yako alikua amekufa, na sasa yu hai; alikua amepotea naye ameonekana.”
But it was fitting to celebrate and be glad, because this brother of yours was dead and is alive again; he was lost and is found.’”