< Luka 14 >
1 Iltokea siku ya Sabato, alipokua akienda nyumbani kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo kula mkate, nao walikuwa wakimchunguza kwa karibu.
2 Tazama, pale mbele yake alikuwa mtu ambaye anasumbuliwa na uvimbe.
3 Yesu aliuliza wataalam katika sheria ya Wayahudi na Mafarisayo, “Je, ni halali kumponya siku ya Sabato, au sivyo?”
4 Lakini wao walikuwa kimya, kwahiyo Yesu akamshika, akamponya na kumruhusu aende zake.
5 Naye akawaambia, “Ni nani kati yenu ambaye ana mtoto au ng'ombe anatumbukia kisimani siku ya Sabato hata mvuta nje mara moja?”
6 Wao hawakuwa na uwezo wa kutoa jibu kwa mambo haya.
7 Wakati Yesu alipogundua jinsi wale walioalikwa kwamba wamechagua viti vya heshima, akawaambia mfano, akiwaambia,
8 “Wakati mnapoalikwa na mtu harusini, usiketi katika nafasi za heshima, kwa sababu inawezekana amealikwa mtu ambaye ni wakuheshimiwa zaidi kuliko wewe.
9 Wakati mtu aliyewaalika ninyi wawili akifika, atakuambia wewe, “mpishe mtu huyu nafasi yako,” na kisha kwa aibu utaanza kuchukua nafasi ya mwisho.
10 Lakini wewe ukialikwa, nenda ukakae mahali pa mwisho, ili wakati yule aliyekualika akija, aweze kukuambia wewe, `Rafiki, nenda mbele zaidi.” ndipo utakuwa umeheshimika mbele ya wote walioketi pamoja nawe mezani.
11 Kwa maana kila ajikwezaye atashushwa, na yeye ajishushae atakwezwa. '
12 Yesu pia alimwambia mtu aliyemwalika, 'Unapotoa chakula cha mchana au cha jioni, usiwaalike rafiki zako au ndugu zako au jamaa zako au majirani zako matajiri, ili kwamba wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo.
13 Badala yake, unapofanya sherehe, waalike maskini, vilema, viwete na vipofu,
14 na wewe utabarikiwa, kwa sababu hawawezi kukulipa. Kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.”
15 Wakati mmoja wa wale walioketi mezani pamoja na Yesu aliposikia hayo, naye akamwambia, “Amebarikiwe yule atakayekula mkate katika Ufalme wa Mungu!”
16 Lakini Yesu akamwambia, “Mtu mmoja aliandaa sherehe kubwa, akaalika watu wengi.
17 Wakati sherehe ilipokuwa tayari, alimtuma mtumishi wake kuwaambia wale walioalikwa, `'Njooni, kwa sababu vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari.'
18 Wote, wakaanza kuomba radhi. Wa kwanza akamwambia mtumishi, 'Nimenunua shamba, lazima niende kuliona. Tafadhali unisamehe.'
19 Na mwingine akasema, `'Nimenunua jozi tano za ng'ombe, na mimi naenda kuwajaribu. Tafadhali uniwie radhi.'
20 Na mtu mwingine akasema, 'Nimeoa mke, kwa hiyo siwezi kuja.'
21 Mtumishi akarudi na kumwambia bwana wake mambo hayo. Yule mwenye nyumba alikasirika akamwambia mtumishi wake, `'Nenda upesi mitaani na katika vichochoro vya mji ukawalete hapa maskini, vilema, vipofu na walemavu.”
22 Mtumimishi akasema, `Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa bado kuna nafasi.'
23 Bwana akamwambia mtumishi, 'Nenda katika njia kuu na vichochoro na uwashurutishe watu waingie, ili nyumba yangu ijae.
24 Kwamaana nawaambia, katika wale walioalikwa wa kwanza hapana atakayeonja sherehe yangu. '
25 Sasa umati mkubwa walikuwa wanakwenda pamoja naye, naye akageuka na akawaambia,
26 'Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, mama yake, mke wake, watoto wake, ndugu zake waume na wanawake- ndio, na hata maisha yake pia -hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
27 Mtu asipochukua msalaba wake na kuja nyuma yangu hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
28 Maana ni nani kati yenu, ambaye anatamani kujenga mnara hataketi kwanza akadirie gharama kwa mahesabu kama ana kile anachohitaji ili kukamilisha hilo?
29 Vinginevyo, baada ya kuweka msingi na kushindwa kumaliza, wote walioona wataanza kumdhihaki,
30 wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.'
31 Au mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine katika vita, ambae hatakaa chini kwanza na kuchukua ushauri kuhusu kama ataweza, pamoja na watu elfu kumi kupigana na mfalme mwingine anayekuja juu yake na watu elfu ishirini?
32 Na kama sivyo, wakati jeshi la wengine bado liko mbali, hutuma balozi kutaka masharti ya amani.
33 Kwa hiyo basi, yeyote kati yenu ambaye hataacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
34 Chumvi ni nzuri, lakini ikiwa Chumvi imepoteza ladha yake, jinsi gani inaweza kuwa chumvi tena?
35 Haina matumizi kwa udongo au hata kwa mbolea. hutupwa mbali. Yeye aliye na masikio ya kusikia, na asikie.”