< Luka 10 >
1 Baada ya mambo hayo, Bwana akachagua sabini wengine, na kuwatuma wawili wawili wamtangulie katika kila mji na eneo alilotarajia kwenda.
Baada ya hayo, Bwana aliwachagua wengine sabini na wawili, akawatuma wawiliwawili, wamtangulie katika kila kijiji na mahali ambapo yeye mwenyewe alitaka kwenda.
2 Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini wafanyakazi ni wachache. Hivyo basi muombeni Bwana wa mavuno, ili kwamba atume haraka wafanyakazi katika mavuno yake.
Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini wavunaji ni wachache. Kwa hivyo, mwombeni mwenye shamba atume wavunaji shambani mwake.
3 Enendeni katika miji. Angalieni, ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu.
Sasa nendeni; fahamuni kwamba ninawatuma ninyi kama kondoo wanaokwenda kati ya mbwa mwitu.
4 Msibebe mfuko wa pesa, wala mikoba ya wasafiri, wala viatu, wala msimsalimie yeyote njiani.
Msichukue mfuko wa fedha, mkoba, wala viatu; msimsalimu mtu yeyote njiani.
5 Katika nyumba yeyote mtakayo ingia, kwanza semeni, 'Amani iwe katika nyumba hii.'
Mkiingia katika nyumba yoyote, kwanza wasalimuni hivi: Amani iwe katika nyumba hii!
6 kama mtu wa amani yupo pale, amani yenu itabaki juu yake, lakini kama sivyo, itarudi kwenu.
Kama akiwako mwenye kupenda amani, amani yenu itakaa naye, la sivyo, itawarudieni.
7 Bakini katika nyumba hiyo, kuleni na mnywe watakachokitoa, kwa maana mfanyakazi anastahili mshahara wake. Msihame kutoka nyumba hii kwenda nyingine.
Kaeni katika nyumba hiyo mkila na kunywa wanavyowapeni, maana mfanyakazi anastahili mshahara wake. Msiende mara nyumba hii mara nyumba ile.
8 Mji wowote muuingiao, na wakawapokea, kuleni chochote kitakachowekwa mbele yenu,
Kama mkifika mji fulani na watu wakiwakaribisha, kuleni wanavyowapeni.
9 na ponyeni wagonjwa waliomo humo. Semeni kwao, 'Ufalme wa Mungu umekuja karibu yanu'
Ponyeni wagonjwa walioko huko, waambieni watu: Ufalme wa Mungu umekaribia kwenu.
10 Lakini katika mji wowote mtakaoingia, na wasiwapokee, nendeni nje katika barabara na semeni,
Lakini mkiingia katika mji wowote, wasipowakaribisheni, tokeni; nanyi mpitapo katika barabara zao semeni:
11 'Hata vumbi katika mji wenu lililonata miguu mwetu tunalikung'uta dhidi yenu! Lakini tambueni hili, Ufalme wa Mungu umekaribia.'
Hata mavumbi ya mji wenu yaliyoshikamana na miguu yetu tunawakung'utieni. Lakini, jueni kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia.
12 Ninawambieni kwamba siku ya hukumu itakuwa ni usitahamilivu zaidi kwa Sodoma kuliko mji huo.
Hakika nawaambieni, siku ile mji huo utapata adhabu kubwa zaidi kuliko ile ya watu wa Sodoma.
13 Ole kwako Korazini, Ole kwako Bethsaida! Kama kazi kuu zilizo fanyika ndani yako ingalifanyika Tiro na Sidoni, Wangelitubu zamani sana, wakikaa ndani ya nguo za gunia na majivu.
“Ole wako Korazini! Ole wako Bethsaida! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika kule Tiro na Sidoni, watu wake wangalikwishavaa mavazi ya gunia kitambo, na kukaa katika majivu kuonyesha kwamba wametubu.
14 Lakini itakuwa usitahamilivu zaidi siku ya hukumu kwa Tiro na Sidoni zaidi yenu.
Hata hivyo, Siku ya Hukumu ninyi mtapata adhabu kubwa zaidi kuliko ile ya watu wa Tiro na Sidoni.
15 Wewe Kapernaumu, Unafikiri utainuliwa mpaka Mbinguni? Hapana, utashushwa chini mpaka kuzimu (Hadēs )
Na wewe Kafarnaumu, unataka kujikweza mpaka mbinguni? La; utaporomoshwa mpaka Kuzimu.” (Hadēs )
16 Atakaye wasikiliza ninyi anisikiliza mimi, na yeyote atakaye wakataa anikataa mimi, na yeyote anikataaye mimi anmtakaa aliyenituma”
Halafu akasema, “Anayewasikiliza ninyi, ananisikiliza mimi; na anayekataa kuwapokea ninyi, anakataa kunipokea mimi. Yeyote anayekataa kunipokea, anakataa kumpokea yule aliyenituma.”
17 Wale sabini walirudi kwa furaha, wakisema, “Bwana, hata mapepo wanatutii katika jina lako.”
Baadaye, wale sabini na wawili walirudi wamejaa furaha, wakisema, “Bwana, hata pepo wametutii tulipolitaja jina lako.”
18 Yesu akawaambia, “Nilimwona Shetani akianguka kutoka mbinguni kama radi.
Yeye akawaambia, “Nilimwona Shetani jinsi alivyokuwa anaporomoka kama umeme kutoka mbinguni.
19 Tazama, nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za adui, na hapana chochote kwa njia yoyote kitakachowadhuru.
Naam, nimewapeni uwezo wa kukanyaga nyoka na ng'e, na uwezo juu ya nguvu zote za yule adui; hakuna chochote kitakachowadhuru.
20 Hata hivyo msifurahi tu katika hili, kwamba roho zinawatii, lakini furahini zaidi kwamba majina yenu yameandikwa mbinguni.”
Hata hivyo, msifurahi kwa sababu pepo wamewatii, bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.”
21 Katika mda uleule alifurahi sana katika Roho Mtakatifu, na kusema, “Ninakusifu wewe, Baba, Bwana wa mbingu na dunia, kwa sababu umeyaficha mambo haya kutoka kwa wenye hekima na akili, na kuyafunua kwa wasio fundishwa, kama watoto wadogo. Ndio, Baba, kwa kuwa ilipendeza katika machoni pako.”
Saa ileile, Yesu akafurahi kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akasema, “Nakushukuru ee Baba, Bwana wa mbingu na dunia, kwa kuwa umewaficha wenye hekima na elimu mambo haya, ukawafumbulia wadogo. Naam, Baba, ndivyo ilivyokupendeza.”
22 “Kila kitu kimekabidhiwa kwangu na Baba yangu, na hakuna afahamuye Mwana ni nani ila Baba, na hakuna afahamuye Baba ni nani ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana hutamani kujifunua kwake.”
Kisha akasema, “Baba yangu ameweka yote mikononi mwangu. Hakuna amjuaye Mwana ni nani ila Baba, wala amjuaye Baba ni nani ila Mwana, na yeyote yule ambaye Mwana anataka kumfunulia hayo.”
23 Akawageukia wanafunzi, akasema faraghani, “Wamebarikiwa wayaonayo haya ambayo ninyi mnayaona.
Halafu akawaelekea wafuasi wake akawaambia, “Heri wanaoona yale mnayoyaona ninyi!
24 Ninawambia ninyi, kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuona mambo myaonayo, na hawakuyaona, na kusikia kusikia mnayoyaikia, na hawakuyasikia.”
Hakika, manabii na wafalme walitamani kuona yale mnayoyaona ninyi wasiyaone, na kusikia yale mnayoyasikia wasiyasikie.”
25 Tazama, mwalimu fulani wa sheria ya Kiyahudi alisimama na kumjaribu, akisema, “Mwalimu, nifanye nini niurithi izima wa milele?” (aiōnios )
Baadaye mwalimu mmoja wa Sheria alisimama akamwuliza akitaka kumtega, “Mwalimu, nifanye nini ili nipate uzima wa milele?” (aiōnios )
26 Yesu akamwambia, “Kimeandikwa nini katika sheria? Unaisoma je?”
Yesu akamwuliza, “Imeandikwa nini katika Sheria? Unaelewaje?”
27 Akajibu akasema, “Utampenda Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote, na jirani yako kama nafsi yako mwenyewe.”
Akamjibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili yako yote. Na, mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.”
28 Yesu akasema, “Umejibu kwa usahihi. Fanya hivi na utaishi.”
Yesu akawaambia, “Vema! Fanya hivyo, nawe utaishi.”
29 Lakini mwalimu, akitamani kujihesabia haki mwenyewe, Akamwambia Yesu, “Na jirani yangu ni nani?”
Lakini yeye akitaka kujihakikishia kuwa mwema akamwuliza Yesu, “Na jirani yangu ni nani?”
30 Yesu akijibu akasema, “Mtu fulani alikuwa akitelemka kutoka Yerusalem kwenda Yeriko. Akaangukia kati ya wanyang'anyi, waliomnyang'anya mali yake, na kumpiga na kumuacha karibu akiwa nusu mfu.
Yesu akamjibu, “Mtu mmoja alikuwa anashuka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko. Alipokuwa njiani, alivamiwa na majambazi, wakamnyang'anya mali yake na kumpiga, wakamwacha amelala pale nusu mfu.
31 Kwa bahati kuhani fulani alikuwa akishuka katika njia hiyo, alipo muona alipita upande mwingine.
Kumbe, kuhani mmoja akawa anapita barabara ileile, akamwona, akapita kando.
32 Vivyo hivyo Mlawi pia, alipofika mahali pale na kumuona, akapita upande mwingine.
Hali kadhalika na Mlawi mmoja, alipofika mahali akamwona, akapita kando.
33 Lakini Msamaria mmoja, alipokuwa akisafiri, alipita pale alipokuwa mtu huyo. alipomuona, alisukumwa kwa huruma.
Lakini Msamaria mmoja aliyekuwa anasafiri, alifika pale yule mtu alipokuwa, naye alipomwona, alimwonea huruma.
34 Alimkaribia na kumfunga vidonda vyake, akimwiga mafuta na divai juu yake. Alimpandisha juu ya mnyama wake, na kumpeleka katika nyumba ya wageni na kumhudumia.
Akamwendea, akamtibu majeraha yake kwa kumtia mafuta na divai; na kuyafunga halafu akampandisha juu ya punda wake akampeleka katika nyumba moja ya wageni akamuuguza.
35 Siku ilyofuata alichukua dinari mbili, na akampatia mmiliki wa nyumba ya wageni na kumwambia, 'Muhudumie na chochote cha ziada utakacho tumia, nitakulipa nitakaporudi.'
Kesho yake akatoa fedha dinari mbili akampa yule mwenye nyumba, akamwambia, Muuguze mtu huyu; na chochote utakachotumia zaidi, nitakulipa nitakaporudi.”
36 Ni yupi kati ya hawa watatu, unafikiri, alikuwa ni jirani kwake yeye aliyeangukia kati ya wanyang'anyi?”
Kisha Yesu akauliza, “Kati ya hao watatu, ni yupi aliyeonyesha kuwa jirani yake yule aliyevamiwa na majambazi?”
37 Mwalimu alisema, “Ni yule aliyeonesha huruma kwake.” Yesu akamwambia, “Nenda na ukafanye vivyo hivyo”
Yule mwalimu wa Sheria akamjibu, “Ni yule aliyemwonea huruma.” Yesu akamwambia, “Nenda ukafanye vivyo hivyo.”
38 Sasa walipokuwa wakisafiri, waliingia katika kijiji fulani, na mwanamke mmoja jina lake Martha alimkaribisha nyumbani kwake.
Walipokuwa safarini, waliingia katika kijiji kimoja na mwanamke mmoja, aitwaye Martha, alimkaribisha nyumbani kwake.
39 Alikuwa na dada aliyeitwa Mariamu, aliekaa miguuni pa Bwana na kusikiliza neno lake.
Martha alikuwa na dada yake aitwaye Maria; huyu aliketi karibu na Yesu akisikiliza mafundisho yake.
40 Lakini Martha alijipa shughuli nyingi za kuandaa mlo. Alikwenda kwa Yesu, na kusema, “Bwana, haujali kwamba dada yangu ameniacha nihudumu peke yangu? Hivyo basi mwambie anisaidie.”
Lakini Martha alikuwa anashughulika na mambo mengi. Basi, akamwendea Yesu, akamwambia, “Bwana, hivi hujali kwamba dada yangu ameniacha nishughulike peke yangu? Mwambie basi, anisaidie.”
41 Lakini Bwana alimjibu na kumwambia, “Martha, Martha, una sumbuka juu ya mambo mengi,
Lakini Bwana akamjibu, “Martha, Martha, unahangaika na kusumbuka kwa mambo mengi.
42 lakini ni kitu kimoja tu cha muhimu. Mariamu amechagua kilicho chema, ambacho hakitaondolewa kutoka kwake.”
Kitu kimoja tu ni muhimu. Maria amechagua kitu bora zaidi ambacho hakuna mtu atakayemnyag'anya.”