< Mambo ya Walawi 7 >
1 Hii ndiyo sheria ya sadaka ya hatia. Kwa sababu hiyo ni sadaka takatifu sana.
“赎愆祭的条例乃是如此:这祭是至圣的。
2 Ni lazima waichinje sadaka ya hatia mahali panapostali kuchinjwa, na ni lazima watainyunyiza damu yake pande zote za madhabahu.
人在那里宰燔祭牲,也要在那里宰赎愆祭牲;其血,祭司要洒在坛的周围。
3 Mafuta yote yaliyomo ndani yake yataondolewa: mafuta ya mkiani, mafuta yaliyo sehamu za ndani,
又要将肥尾巴和盖脏的脂油,
4 zile figo mbili pamoja na mafuta yaliyo juu yake, yaliyo karibu na kiuno, na yanayofunika ini—nyama hii yote lazima iondolewe pamoja na hizo figo.
两个腰子和腰子上的脂油,就是靠腰两旁的脂油,并肝上的网子和腰子,一概取下。
5 Kuhani ataviteketeza vipande hivi juu ya madhabahu viwe dhabihu iliyofanywa kwa Yahweh kwa moto. Hii ni sadaka ya hatia
祭司要在坛上焚烧,为献给耶和华的火祭,是赎愆祭。
6 Kila mwanaume miongoni mwa familia ya kuhani anaweza kula sehemu ya sadaka hii. Lakini ni lazima iliwe ndani ya mahali patakatifu kwa sababu ni takatifu sana.
祭司中的男丁都可以吃这祭物;要在圣处吃,是至圣的。
7 Nayo sadaka ya dhambi ni kama ilivyo sadaka ya hatia. Ni sheria ileile hutumika kwa zote mbili. Zote ni mali ya kuhani azitumiaye kufanya upatanisho.
赎罪祭怎样,赎愆祭也是怎样,两个祭是一个条例。献赎愆祭赎罪的祭司要得这祭物。
8 Kuhani atoaye sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya mtu yeyote anaweza kuchuku ngozi ya sadaka hiyo kwa ajili yake mwenyewe.
献燔祭的祭司,无论为谁奉献,要亲自得他所献那燔祭牲的皮。
9 Kila sadaka ya nafaka inayookwa mekoni, na kila sadaka kama hiyo ipikwayo kaangoni au kwenye sufuria itakuwa ya kuhani aitoaye.
凡在炉中烤的素祭和煎盘中做的,并铁鏊上做的,都要归那献祭的祭司。
10 Kila sadaka ya nafaka, ama iwe unga mkavu au uliochanganywa na mafuta ya zeitu itakuwa ya ukoo wa Aroni kwa usawa.
凡素祭,无论是油调和的是干的,都要归亚伦的子孙,大家均分。”
11 Hii ndiyo sheria ya dhabihu ya sadaka za amani, ambazo watu watazitoa kwa Yahweh.
“人献与耶和华平安祭的条例乃是这样:
12 Iwapo mtu yeyote anaitoa ili kuonyesha shukrani kwa Yahweh, basi ataitoa pamoja na dhabih uya mikate iliyotengenezwa bila hamira, bali kwa mafuta ya zeituni yaliyochanganywa na unga lakini bila hamira, na maandazi yaliyotengenezwa bila hamira, bali yaliyopakwa mafuta juu yake, na mikate miembamba iliyofanywa kwa unga laini uliochanganywa na mafuta.
他若为感谢献上,就要用调油的无酵饼和抹油的无酵薄饼,并用油调匀细面做的饼,与感谢祭一同献上。
13 Kwa kusudi la kutoa shukrani, pia anapaswa kutoa pamoja na sadaka yake ya amani, vipande vya mikate iliyotiwa hamira.
要用有酵的饼和为感谢献的平安祭,与供物一同献上。
14 Ni lazima atatoa moja kila aina ya sadaka hizi kama sadaka iliyoletwa kwa Yahweh. Nayo itakuwa ya makuhani wanaonyunyizia damu ya sadaka ya amani kwenye madhabahu.
从各样的供物中,他要把一个饼献给耶和华为举祭,是要归给洒平安祭牲血的祭司。
15 Mtu anayeleta sadaka ya amani kwa kusudi la kutoa shukrani ni lazima ataila nyama ya sadaka yake siku ya kutoa dhabihu. Hatakiwi kusaza chochote kilicho cha sadaka hiyo hata asubuhi ya pili.
为感谢献平安祭牲的肉,要在献的日子吃,一点不可留到早晨。
16 Lakini iwapo dhabihu ya matoleo yake kusudi lake ni nadhiri, au kwa kusudi la sadaka ya hiari, nyama yake italiwa siku iyo hiyo aitoapo dhabihu yake, lakini chochote kinachosalia cha sadaka hiyo kinaweza kuliwa siku inayofuata.
若所献的是为还愿,或是甘心献的,必在献祭的日子吃,所剩下的第二天也可以吃。
17 Hata hivyo, nyama yoyote ya dhabihu inayobaki siku ya tatu ni lazima ichomwe moto.
但所剩下的祭肉,到第三天要用火焚烧;
18 Iwapo kipande chochote cha nyama hiyo ya dhabihu kinachobaki kinaliwa katika siku ya tatu, hakitakubalika, wala hakitatolewa kwa aliyeitoa. Kitakuwa ni kitu cha kuchukiza, na mtu akilaye atabeba hatia ya dhambi mwenyewe yake.
第三天若吃了平安祭的肉,这祭必不蒙悦纳,人所献的也不算为祭,反为可憎嫌的,吃这祭肉的,就必担当他的罪孽。
19 Nyama yoyote inayogusa kitu kilicho najisi haitaliwa. Ni lazima ichomwe moto. Na kwa ajili ya nyama inayobaki, yeyote aliye safi anaweza kuila.
“挨了污秽物的肉就不可吃,要用火焚烧。至于平安祭的肉,凡洁净的人都要吃;
20 Hata hivyo, mtu najisi anayekula nyama kutoka kwenye dhabihu ya matoleo ya amani ambayo ni ya Yahweh yapasa mtu huyu akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.
只是献与耶和华平安祭的肉,人若不洁净而吃了,这人必从民中剪除。
21 Iwapo mtu yeyote anagusa kitu chochote kilichonajisi—iwe ni unajisi wa binadamu, au wa mnyama aliyenajisi, au wa kitu fulani kilichonajisi na chenye kuchukiza, na kisha akala baadhi ya nyama ya dhabihu ya sadaka ya amani iliyotolewa kwa Yahweh, lazima mtu huyo akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.
有人摸了什么不洁净的物,或是人的不洁净,或是不洁净的牲畜,或是不洁可憎之物,吃了献与耶和华平安祭的肉,这人必从民中剪除。”
22 Kisha Yahweh akazungumza na Musa, akisema,
耶和华对摩西说:
23 “Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, 'hamruhusiwi kula mafuta ya fahali au kondoo au mbuzi.
“你晓谕以色列人说:牛的脂油、绵羊的脂油、山羊的脂油,你们都不可吃。
24 Mafuta ya mnyama yoyote afaye peke yake bila ya kuwa dhabihu, au mafuta ya mnyama yeyote aliyeraruliwa na wanyama pori, yanaweza kutumika kwa makusudi mengine, lakini hakika hamtayala.
自死的和被野兽撕裂的,那脂油可以做别的使用,只是你们万不可吃。
25 Yeyote atakayekula mafuta ya mnyama ambayo watu wanaweza kuyatoa kuwa dhabihu ya iliyofanywa kwa Yahweh kwa moto, mtu huyo lazima atakatiliwa mbali kutoka kwa watu wake.
无论何人吃了献给耶和华当火祭牲畜的脂油,那人必从民中剪除。
26 Hamtakula damu yoyote katika mojawapo ya nyumba zenu, ama iwe kutoka kwa ndege au mnyama.
在你们一切的住处,无论是雀鸟的血是野兽的血,你们都不可吃。
27 Yeyote alaye damu yoyote, mtu huyo lazima akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.'”
无论是谁吃血,那人必从民中剪除。”
28 Kwa hiyo Yahweh akazungumza na Musa na akasema,
耶和华对摩西说:
29 “Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, 'Yeye atoaye dhabidhu ya sadaka ya amani kwa Yahweh lazima alete sehemu ya dhabihu yake kwa Yahweh.
“你晓谕以色列人说:献平安祭给耶和华的,要从平安祭中取些来奉给耶和华。
30 Mikono yake mwenyewe lazima iilete hiyo sadaka ifanywayo kwa Yahweh kwa moto. Naye atayaleta hayo mafuta pamoja na kidari, ili kwamba kidari kiweze kutikiswa kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za Yahweh.
他亲手献给耶和华的火祭,就是脂油和胸,要带来,好把胸在耶和华面前作摇祭,摇一摇。
31 Kuhani atayachoma mafuta hayo juu ya madhabahu, lakini kile kidari kitakuwa mali ya Aroni na uzao wake.
祭司要把脂油在坛上焚烧,但胸要归亚伦和他的子孙。
32 Ni lazima utatoa paja la kulia kwa kuhani kama sadaka iliyotokana na dhabihu ya sadaka yako ya amani.
你们要从平安祭中把右腿作举祭,奉给祭司。
33 Yule kuhani, mmoja wa wazao wa Aroni, atoaye damu na mafuta ya sadaka ya amani—ni lazima atapata paja la kulia kama mgao wake wa sadaka.
亚伦子孙中,献平安祭牲血和脂油的,要得这右腿为分;
34 Kwa kuwa nimetwaa kidari, na paja la sadaka ya kutikiswa kutoka kwa watu wa Israeli uwe mchango wao, na amepewa Aroni kuhani na wanawe kuwa mgao wao wa kawaida.
因为我从以色列人的平安祭中,取了这摇的胸和举的腿给祭司亚伦和他子孙,作他们从以色列人中所永得的分。”
35 Huu ndiyo mgao wa Aroni na uzao wake utokanao na matoleo yaliyofanywa kwa Yahweh kwa moto, siku ile Musa alipowaweka wakfu ili kumtumikia Yahweh katika kazi ya kuhani.
这是从耶和华火祭中,作亚伦受膏的分和他子孙受膏的分,正在摩西叫他们前来给耶和华供祭司职分的日子,
36 Huu ndio mgao ambao Yahweh aliamru waweze kupewa kutoka kwa watu wa Israeli, katika siku hiyo aliyowatia mafuta ya upako wawe makuhani. Nao utakuwa mgao wao wa kila siku katika vizazi vyote.
就是在摩西膏他们的日子,耶和华吩咐以色列人给他们的。这是他们世世代代永得的分。
37 Hii ndiyo sheria ya sadaka ya kuteketezwa, ya sadaka ya nafaka, ya sadaka ya dhambi, ya sadaka ya hatia, ya sadaka ya kuweka wakfu, na ya dhabihu, ya sadaka za amani,
这就是燔祭、素祭、赎罪祭、赎愆祭,和平安祭的条例,并承接圣职的礼,
38 ni sheria ambazo Yahweh alizitoa kwa Musa kwenye Mlima Sinai siku aliyowaamru watu wa Israeli kutoa dhabihu zao kwa Yahweh katika jangwa la Sinai.'”
都是耶和华在西奈山所吩咐摩西的,就是他在西奈旷野吩咐以色列人献供物给耶和华之日所说的。