< Mambo ya Walawi 5 >
1 Kama mtu atatenda dhambi kwa sababu hakusema ukweli wakati alipotakiwa kutoa ushahidi fulani kuhusu kile alichotakiwa, ameona au kufahamu habari zake, yeye anastahili adhabu.
“‘Ikiwa mtu atakuwa ametenda dhambi kwa sababu hakusema alipotakiwa kutoa ushahidi hadharani kuhusu jambo aliloona au kujua habari zake, yeye anastahili adhabu.
2 Au mtu akigusa kitu chochote ambacho Mungu amekitaja kuwa ni najisi hata kama ni mzoga wa wanyama wa porini au ni mzoga wa wanyama wa kufugwa au wataambaao hata kama mtu huyo hakukusudia kumgusa, yeye ni najisi na mwenye hatia.
“‘Au kama mtu akigusa kitu chochote ambacho ni najisi, iwe ni mizoga ya wanyama pori walio najisi, au ya wanyama wafugwao walio najisi, au ya viumbe vitambaavyo ardhini, hata akiwa hana habari, amekuwa najisi na mwenye hatia.
3 Au amegusa kitu chochote kilicho kichafu, kwa vyovyote kama hakujua, ndipo atakuwa na hatia akijua vile.
“‘Au kama akigusa kitu kilicho kichafu kinachotokana na binadamu, kitu chochote kile kinachoweza kumfanya awe najisi, hata akiwa hana habari, atakapofahamu atakuwa na hatia.
4 Au kama yeyote akiapa bila kufikiri kwa midomo yake kufanya ubaya, au kufanya vyema kwa vyovyote vile mtu ameapa kwa haraka atakapotambua atakuwa na hatia kwa vitu hivyo.
“‘Au kama mtu ameapa kufanya kitu chochote bila kufikiri, kiwe chema au kibaya, kwa vyovyote mtu aweza kuapa bila kujali, hata akiwa hana habari, atakapofahamu atakuwa na hatia.
5 Mtu yeyote akiwa na hatia kwa vitu hivi, lazima akiri kwa yoyote dhambi aliyotenda.
“‘Wakati mtu yeyote atakapokuwa na hatia katika mojawapo ya haya, lazima akiri ni kwa njia gani ametenda dhambi,
6 Ndipo atakapoleta sadaka yake ya hatia mbele za Bwana kwa dhambi aliyokwisha tenda. Ataleta kondoo jike au mbuzi kutoka katika kundi lake kuwa matoleo ya dhambi, kuhani atafanya upatanisho kuhusu dhambi yake.
na kama adhabu ya dhambi aliyoitenda, lazima alete kwa Bwana kondoo jike au mbuzi jike kutoka kwenye kundi lake kama sadaka ya dhambi; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi yake.
7 Kama hataweza kununua mwana kondoo ataleta kama sadaka ya hatia, hua wawili au makinda mawili ya njiwa kwa Bwana, mmoja kwa sadaka ya dhambi na mwingine ni sadaka ya kutekeketezwa.
“‘Lakini huyo mtu kama hataweza kumtoa mwana-kondoo, ataleta hua wawili au makinda mawili ya njiwa kwa Bwana kuwa adhabu kwa ajili ya dhambi yake, mmoja wa hao ndege kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na wa pili kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa.
8 Atawaleta kwa kuhani, wa kwanza atatoa kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Atamvunja shingo yake lakini ataacha kichwa chake kinaning'inia wala hataiondoa kabisa shingo yake katika mwili.
Atawaleta kwa kuhani, ambaye atamtoa kwanza ndege mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Atamvunja shingo na kuacha kichwa chake kikiningʼinia,
9 Ndipo atanyunyizia damu yake katika sehemu za madhabahu, na damu inayobaki ataimwaga chini ya madhabahu. Hii ni dhabihu ya dhambi.
naye atanyunyiza sehemu ya hiyo damu ya sadaka ya dhambi kwenye pembe za madhabahu. Damu iliyobaki lazima ichuruzwe chini ya madhabahu. Hii ni sadaka ya dhambi.
10 Ndipo ataoa ndege wa pili kama sadaka ya kuteketezwa kama ilivyoelekezwa, na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya dhambi alizokwisha kufanya, na huyo mtu atakuwa amesamehewa.
Kisha kuhani atamtoa yule ndege wa pili kama sadaka ya kuteketezwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa, na hivyo kufanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi aliyoitenda, naye atasamehewa.
11 Lakini kama hataweza kununua hua wawili au makinda ya njiwa mawili, ndipo ataleta kama dhabihu ya dhambi zake sehemu ya kumi ya unga laini kama sadaka ya dhambi. Asiweke mafuta wala ubani juu yake, kwa kuwa ni sadaka ya dhambi.
“‘Ikiwa basi, hawezi kupata hua wawili au makinda mawili ya njiwa, ataleta sehemu ya kumi ya efa ya unga laini kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Kamwe asiweke mafuta wala uvumba juu yake, kwa sababu ni sadaka ya dhambi.
12 Atauleta kwa kuhani, na kuhani atachukua konzi moja ya unga kama ukumbusho wa wema wa Bwana na atauweka juu ya madhabahu na kuteketeza juu ya sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa ajili ya Bwana. Hii ni sadaka ya dhambi.
Atauleta unga kwa kuhani, ambaye atachukua konzi moja kama sehemu ya kumbukumbu na atauteketeza kwenye madhabahu juu ya sadaka zilizotolewa kwa Bwana kwa moto. Hii ni sadaka ya dhambi.
13 Kuhani atafanya upatanisho kwa dhambi yoyote aliyofanya mtu yeyote, mtu huyo atasamehewa. Na sadaka inayobaki itakuwa ya kuhani, kama ilivyo sadaka ya nafaka.'”
Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi yoyote ya hizo alizotenda, naye atasamehewa. Sadaka iliyobaki itakuwa ya kuhani, kama ilivyokuwa ile sadaka ya nafaka.’”
14 Bwana akamwambia Musa, akasema,
Bwana akamwambia Mose:
15 “Kama mtu akikiuka amri na kufanya dhambi kinyume na mambo matakatifu ya Bwana, lakini akifanya bila kukusudia ataleta sadaka ya hatia kwa Bwana. Sadaka hii itakuwa ni kondoo dume asiye na kasoro kutoka katika kundi; thamani yake halisi kifedha kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kama sadaka ya hatia.
“Mtu anapokiuka na kutenda dhambi pasipo kukusudia kuhusu mojawapo ya mambo matakatifu ya Bwana, huyo mtu ataleta kwa Bwana kama adhabu kondoo dume mmoja kutoka kundi lake, asiye na dosari na mwenye thamani halisi kifedha, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. Hii ni sadaka ya hatia.
16 Lazima atalipa kwa Bwana kwa kile alichokosa kulingana na kitakatifu, na ataongezea moja ya tano na kumpa kuhani. Ndipo kuhani ataweka upatanisho kwa ajili yake pamoja na kondoo wa sadaka ya hatia, na mtu atakuwa amesamehewa.
Ni lazima alipe kwa yale aliyoshindwa kufanya kuhusu vitu vitakatifu, kwa kuongeza sehemu ya tano ya thamani ile na kuitoa yote kwa kuhani, ambaye atamfanyia upatanisho kwa huyo kondoo dume kama sadaka ya dhambi, naye atasamehewa.
17 Kama mtu akitenda dhambi kwa kufanya kile ambacho Bwana aliagiza kisifanyike, hata kama hakujuwa, atakuwa na hatia na ataibeba hatia yake.
“Kama mtu akifanya dhambi na kufanya yale yaliyokatazwa katika mojawapo ya amri za Bwana, hata ikiwa hajui, yeye ana hatia na anastahili adhabu.
18 Lazima ataleta kondoo dume asiye na kasoro kutoka katika kundi, anayestahili thamani ya fedha, kama sadaka ya hatia kwa kuhani. Ndipo kuhani atafanya upatanisho kulingana na dhambi aliyotenda, ambayo hakujua atakuwa amesamehewa.
Atamletea kuhani kama sadaka ya hatia kondoo dume kutoka kundi lake, kondoo asiye na dosari na mwenye thamani halisi kifedha. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa kosa alilotenda bila kukusudia, naye atasamehewa.
19 Ni sadaka ya hatia, na amekuwa na hatia mbele za Bwana.”
Hii ni sadaka ya hatia; amekuwa na hatia kwa kufanya kosa dhidi ya Bwana.”