< Mambo ya Walawi 3 >

1 Kama mtu atoa dhabihu ambayo ni matoleo ya amani ya mnyama kutoka katika kundi, dume au jike, lazima atatoa mnyama asiyena kasoro mbele ya Bwana.
“‘Kama sadaka ya mtu ni sadaka ya amani, naye akatoa ngʼombe kutoka kundi, akiwa dume au jike, atamleta mnyama asiye na dosari mbele za Bwana.
2 Ataweka mikono yake juu ya sadaka yake na atamchinja mbele ya mlango wa hema ya kukutania. Kisha wana wa Haruni makuhani watanyunyizia damu yake katika pande za madhabahu.
Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka yake na kumchinja penye ingilio la Hema la Kukutania. Ndipo makuhani wana wa Aroni watanyunyiza damu yake pande zote za madhabahu.
3 Mtu akitoa dhabihu ya amani itolewayo kwa moto kwa ajili ya Bwana. Mafuta yanayofunika au yanayoungana na hizo sehemu za ndani,
Kutoka kwenye hiyo sadaka ya amani ataleta sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto: mafuta yote ya mnyama yafunikayo sehemu za ndani, ama yanayoungana na hizo sehemu za ndani,
4 figo mbili na mafuta yaliyofunika kiunoni na yanayozunguka ini, pamoja na figo atayatoa pamoja.
figo zote pamoja na mafuta yote yanayozizunguka karibu na kiuno na yale yanayofunika ini, ambayo atayaondoa pamoja na figo.
5 Wana wa Haruni watayachoma hayo katika madhabahu pamoja na sadaka ya kutekezwa, juu ya kuni zilizo kwenye moto. Zitaleta harufu nzuri mbele ya Bwana; itakuwa sadaka ya itolewayo kwake kwa moto.
Kisha wana wa Aroni wataiteketeza juu ya madhabahu, juu ya ile sadaka ya kuteketezwa iliyoko juu ya kuni zinazowaka, kama sadaka ya kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.
6 Kama dhabihu ya amani ya mtu itolewayo kwa Bwana ni kutoka katika mifugo ni mbuzi au kondoo ni dume au jike, atatoa dhabihu isiyo na kasoro.
“‘Kama akitoa kondoo au mbuzi kutoka kundi kama sadaka ya amani kwa Bwana, atamtoa dume au jike asiye na dosari.
7 Kama atatoa mwanakondoo kwa ajili ya dhabihu yake, atamtoa mbele za Bwana.
Kama akimtoa mwana-kondoo, atamleta mbele za Bwana.
8 Ataweka mkono wake juu ya ya kichwa cha dhabihu yake na atamchinja mbele ya hema ya kukutania. Ndipo wana wa Haruni watanyunyizia damu pande za madhabahu.
Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka yake, naye atamchinja mbele ya Hema la Kukutania. Kisha wana wa Aroni watanyunyiza damu yake kwenye madhabahu pande zote.
9 Mtu akitoa sadaka ya dhabihu ya amani kama sadaka ya kusogezwa kwa moto kwa Bwana. Mafuta, mafuta ya mkia yatakatwa hapo karibu na mfupa wa kiuno, na mafuta yanayofunika matumbo na mafuta yaliyo katika matumbo,
Kutoka kwenye hiyo sadaka ya amani ataleta dhabihu iliyotolewa kwa Bwana kwa moto: mafuta yake, mafuta yote ya mkia uliokatwa karibu na uti wa mgongo, mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani au yale yanayounganika nazo,
10 na figo zote mbili na mafuta yanayofunika yaliyo karibu na kiuno kitambi kilicho karibu na ini na figo ataziondoa zote.
figo mbili pamoja na mafuta yanayozizunguka yaliyo karibu na kiuno na yale yanayofunika ini, ambayo atayatoa pamoja na figo.
11 Na kuhani atayatekeza yote kwa moto katika madhabahu kama sadaka ya chakula isogezwayo kwa moto kwa Bwana.
Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu kama chakula, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto.
12 Kama matoleo ya mtu ni mbuzi, ndipo ataitoa mbele ya Bwana.
“‘Kama sadaka yake ni mbuzi, ataileta mbele za Bwana.
13 Ataweka mikono yake juu ya kichwa cha mbuzi na atamchinja mbele ya hema ya kukutania. Ndipo wana wa Haruni watanyunyizia damu pande zote za madhabahu.
Ataweka mkono wake juu ya kichwa chake na kumchinja mbele ya Hema la Kukutania. Kisha wana wa Aroni watanyunyiza damu yake kwenye madhabahu pande zote.
14 Mtu akitoa dhabihu kwa Bwana kwa njia ya moto. Ataondoa mafuta yanayozunguka matumbo, na mafuta yote yanayozunguka matumbo.
Kutokana na ile sadaka anayotoa, atatoa sadaka hii kwa Bwana kwa moto: mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani na yale yanayoungana nazo,
15 Ataondoa pia figo mbili na mafuta yanayozunguka, ambayo yanazunguka kiuno na kitambi cha maini pamoja na figo.
figo zote mbili pamoja na mafuta yaliyo juu yake karibu na kiuno na yanayofunika ini, ambayo atayaondoa pamoja na figo.
16 Kuhani atateketeza yote juu ya madhabahu kama matoleo ya chakula yatolewayo kwa moto, ni sadaka ya kuleta harufu nzuri sana. Mafuta yote ni ya Bwana.
Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu kama chakula, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri. Mafuta yote ya mnyama ni ya Bwana.
17 Itakuwa ni amri ya kudumu kwa kizazi cha watu katika maeneo yote mtakapotengeneza makazi, kwamba hamtakula mafuta au damu.”'
“‘Hii ni kanuni ya kudumu kwa vizazi vijavyo, popote muishipo: Msile mafuta yoyote ya mnyama wala damu.’”

< Mambo ya Walawi 3 >