< Mambo ya Walawi 26 >
1 Msijitengenezee sanamu, wala msisimamishe kinyago cha kuchonga au nguzo ya jiwe ya kuabudia, na msisimamisha sura ya jiwe la kuchonga katika nchi yenu mtayoiinamia, kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
2 Ni lazima muitunze Sabato Yangu na kupaheshimu patakatifu pangu. Mimi ndimi Yahweh.
3 Iwapo mtatembea katika sheria zangu na kuzishika amri zangu na kuzitii,
4 Nami nitawapa ninyi mvua katika majira yake; nayo nchi itatoa mazao yake, na miti ya shambani itatoa matunda yake.
5 Upuraji wenu utaendelea hata wakati wa mavuno ya zabibu, na mavuno ya zabibu yataendelea mpaka majira ya kupada mbegu. Nanyi mtakula mkate na kushiba na kuishi salama mahali mtakapofanya mji wenu katika nchi.
6 Nitawapa amani; mtalala bila ya kitu chochote kuwatia hofu. Nitawaondolea mbali wanyama waliohatari katika nchi, na upanga hautapita katika nchi yenu.
7 Mtawafukuza adui zenu, nao wataanguka mbele yenu kwa upanga.
8 Watu wenu watano watafukuza adui mia moja, na watu wenu mia moja watafukuza adui elfu kumi; adui zenu wataanguka mbele yenu kwa upanga.
9 Nitawatazama kwa upendeleo na kuwafanya nyinyi mzae na kuwazidisha nyinyi.
10 Mtakula chakula kilichotunzwa ghalani kwa muda mrefu. Mtayaondoa mazao yaliyohifadhiwa ghalani kwa sababu mtahitaji ghala kwa ajili ya mavuno mapya.
11 Nitaliweka hema langu katikati yenu, nami stachukizwa nanyi.
12 Nitatembea miongoni mwenu nami nitakuwa Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu.
13 Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu, aliyewaleta nyinyi kutoka nchi ya Misri, ili kwamba msingeendelea kuwa watumwa wao. Nimevunja makomeo ya nira yenu na nikawafanya mtembee kwa kunyooka.
14 Lakini ikiwa hamtanisikiliza mimi,
15 na kutozitii amri hizi, na ikiwa mtayakataa maagizo yangu, na kuzichukia sana sheria zangu, kiasi kwamba hamtaweza kuzitii amri zangu zote, lakini mkalivunja agano langu—
16 —kama mtafanya mambo haya, Nami nitafanya hili kwenu: Nitasababisha hofu juu yenu, maradhi na homa kali itakayoangamiza macho na kuondoa uhai wenu. Mtapanda mbegu zenu kwa hasara, kwa sababu adui zenu watakula mazao yake.
17 Nitakaza uso wangu dhidi yenu, na mtashindwa na adui zenu. Watu wanaowachukia watatawala juu yenu, na mtakimbia hata kama hakutakuwa na yeyote anayewafukuza.
18 Iwapo hamtasikiliza maagizo yangu, Nami niwataadhibu vikali mara saba kwa dhambi zenu.
19 Nami nitakivunja kiburi chenu katika uwezo wenu. Nitaifanya mbingu juu yenu iwe kama chuma na nchi yenu kama shaba.
20 Nguvu yenu itatumika bure, kwa sababu nchi yenu haitazalisha mavuno yake, na miti yenu katika nchi haitazaa matunda yake.
21 Iwapo mtataenenda kinyume changu na hamtanisikiliza mimi, nitaleta mapigo mara saba zaidi juu yenu, sawasawa na dhambi zenu.
22 Nitatuma wanyama mapori hatari dhidi yenu, ambao watawaibia watoto wenu, kuangamiza mifugo yenu na kuwafanya mwe wachache katika idadi yenu. Hivyo barabara zenu zitakuwa nyeupe.
23 Endapo pamoja na mambo haya kuwapata lakini msiyakubali marekebisho yangu na mkazidi kuenenda katika upinzani dhidi yangu,
24 ndipo nami pia nitaenenda kinyume chenu, na Mimi mwenyewe nitawaadhibu mara saba kwa sababu ya dhambi zenu.
25 Nitaleta upanga juu yenu utakaowaadhibu kwa kisasi kwa sababu ya kulivunja agano. Nanyi mtajikusanya kwenye miji yenu, Nami nitatuma humo maafa miongoni mwenu, na mtachukuliwa mikononi mwa adui yenu.
26 Nitakapokomesha mgao wa chakula, wanawake kumi wataweza kuoka mkate wako katika chombo kimoja cha kuokea na watakugawia mkate wako kwa uzani. Nanyi mtakula lakini hamtatoshelezwa.
27 Endapo hamtanisikiliza pamoja na mambo haya kuwapata, lakini mkazidi kuenenda kinyume na mimi,
28 kisha nami nitakwenda kinyume nanyi katika hasira, Nami nitawaadhibu hata mara saba kulingana na wingi wa dhambi zenu.
29 Ndipo mtakapokula nyama ya wana wenu; mtakula nyama ya binti zenu.
30 Nitapaangamiza mahali penu pa juu, kuziangusha chini madhabahu zenu za kufukizia uvumba, na kuzitupa maiti zenu juu ya maiti ya sanamu zenu, na Mimi mwenyewe nitawadharau nyinyi.
31 Nitaigeuza miji yennu kuwa magofu na kupaharibu patakatifu penu. Nami sitapendezwa na harufu nzuri ya matoleo yenu.
32 Nami nitaiharibu nchi. Adui zenu watakaokuwa wakiishi humo watashtushwa na uharibifu huo.
33 Nami nitawatawanya nyinyi katika mataifa, na nitaufuta upanga wangu na kuwafuatia. Nchi yenu itatelekezwa, na miji yenu itakuwa magofu.
34 Nayo nchi itazifurahia Sabato zake kwa kuwa itakuwa imetelekezwa na ninyi mkiwa katika nchi za daui zenu. Katika nyakati hizo, nchi itapumzika na kufurahia Sabato zake.
35 Maadamu itakuwa imetelekezwa, itakuwa na pumziko, ambalo litakuwa ni pumziko iliyolikosa pamoja na Sabato zenu mlipokuwa mkiishi ndani yake.
36 Na kwa wale watakoachwa humo kwenye nchi za adui zenu, Nitatuma hofu ndani ya mioyo yenu kiasi kwamba hata kama ni maelfu ya majani tu yatakapopeperushwa katika upepo yatawaogofyeni. Nanyi mtaanguka hata kama hakutakuwa na awafukuzaye.
37 Mtajikwaa kila mmoja juu ya mwenzake kama vile mlikuwa mkiukimbia upanga, hata kama hakutakuwa na awafukuzaye nyinyi. Hamtakuwa na nguvu ya kusimama mbele ya daui zenu.
38 Nanyi mtaangamia miongoni mwa mataifa, nayo nchi ya adui zenu yenyewe itawamezani.
39 Wale watakosalia miongoni mwenu watapotelea katika dhambi zao, huko kwenye nchi za adui zenu, na kwa sababu ya dhambi zao, na kwa sababu ya dhambi za baba zao watapotelea mbali pia.
40 Lakini kama watakiri dhambi zao na dhambi ya baba zao, na usaliti wao ambao kwao hawakuwa waaminifu kwangu, pia na mwenendo wao dhidi yangu—
41 ambao ulinisababisha kuwa kinyume nao, na kuwaleta katika nchi ya adui zao—iwapo mioyo yao isiyotahiriwa itanynyekezwa,
42 na iwapo wataikubali adhabu kwa ajili ya dhambi zao, nami nitalikumbuka agano langu na Yakobo, agano langu na Isaka, agano langu na Abrahamu; Pia, nitaikumbuka nchi.
43 Nchi itakayotelekezwa na wao, hivyo itapendezwa na Sabato zake inapobaki imetelekezwa na wao. Itawapasa kulipa hatia kwa dhambi zao kwa sababu ni wao wenyewe ndiyo walioyakataa maagizo yangu na kuzichukia sheria zangu.
44 Lakini pamoja na haya yote, watapokuwa katika nchi ya adui zao, Mimi stawakataa wao, wala sitawachukia ili kuwaangamiza kabisa na kulifutilia mbali agano langu nilililoagana nao, kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh Mungu wao.
45 Bali kwa ajili yao, nitalikumbuka agano langu na baba zao, niliowaleta kutoka katika nchi ya Misri machoni pa mataifa, ili niwe Mungu wao. Mimi ndimi Yahweh.”
46 Hizi ndizo amri, hukumu, na sheria ambazo Yahweh alifanya baina yake na watu wa Israeli kwenye Mlima Sinai kwa kupitia Musa.