< Mambo ya Walawi 23 >
1 Yahweh akamwambia Musa:
And the LORD spoke unto Moses, saying:
2 “Zungumza na watu wa Israeli, na uwaambie, 'Hizi ndizo sikukuu zilizoamriwa kwa ajili ya Yahweh, ambazo ni lazima mzitangaze kuwa makusanyiko matakatifu, ni sikukuu zangu za mara kwa mara.
Speak unto the children of Israel, and say unto them: The appointed seasons of the LORD, which ye shall proclaim to be holy convocations, even these are My appointed seasons.
3 Mnaweza kufanya kazi kwa siku sita, lakini siku ya saba ni Sabato ya kupumzika kabisa. Usifanye kazi kwa sababu ni Sabato kwa ajili ya Yahweh mahali pote mnaposhi.
Six days shall work be done; but on the seventh day is a sabbath of solemn rest, a holy convocation; ye shall do no manner of work; it is a sabbath unto the LORD in all your dwellings.
4 Hizi ndizo sikukuu za Yahweh zilizoamriwa, Makusanyiko matakatifu mtakayoyatangaza kwa nyakati zilioamriwa:
These are the appointed seasons of the LORD, even holy convocations, which ye shall proclaim in their appointed season.
5 Katika mwenzi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi kwenye mwanga hafifu wa machweo ya jua, ni Pasaka ya Yahweh.
In the first month, on the fourteenth day of the month at dusk, is the LORD'S passover.
6 Siku ya kumi na tano ya mwezi ule ule ni sikukuu ya mikate isiotiwa hamira kwa ajili ya Yahweh. Kwa muda wa siku saba mtakula mikate isiotiwa hamira.
And on the fifteenth day of the same month is the feast of unleavened bread unto the LORD; seven days ye shall eat unleavened bread.
7 Siku ya kwanza ni lazima mjitenge kwa pamoja, hamtafanya kazi ya kawaida.
In the first day ye shall have a holy convocation; ye shall do no manner of servile work.
8 Kwa siku saba mtamletea Yahweh matoleo ya chakula. Siku ya saba ni ya kusanyiko takatifu lililotengwa kwa ajili ya Yahweh, nanyi katika siku hiyo hamtafanya kazi yoyote ya kawaida.”
And ye shall bring an offering made by fire unto the LORD seven days; in the seventh day is a holy convocation; ye shall do no manner of servile work.
9 Yahweh akamwambia Musa, akisema,
And the LORD spoke unto Moses saying:
10 “Sema na watu wa Israeli uwaambie, 'mtakapika kwenye nchi nitakayowapa nyinyi, na mtakapovuna mazao yake, nanyi yawapasa kumletea kuhani fungu la masuke ya nafaka ya matunda yake ya kwanza.
Speak unto the children of Israel, and say unto them: When ye are come into the land which I give unto you, and shall reap the harvest thereof, then ye shall bring the sheaf of the first-fruits of your harvest unto the priest.
11 Naye ataliinua hilo fungu la masuke ya nafaka mbele za Yahweh na kulileta kwake, kwa kuwa litakubalika kwa niaba yenu. Nalo litaletwa siku baada ya Sabato ili kwamba kuhani ataliinua na kulileta kwangu.
And he shall wave the sheaf before the LORD, to be accepted for you; on the morrow after the sabbath the priest shall wave it.
12 Siku ile mtakapoliinua lile fungu la masuke ya nafaka na kulileta kwangu, itawabidi kutoa mwana—kondoo dume wa mwaka mmoja na asiye na dosari awe sadaka ya kuteketezwa kwa Yahweh.
And in the day when ye wave the sheaf, ye shall offer a he-lamb without blemish of the first year for a burnt-offering unto the LORD.
13 Matoleo ya nafaka yatakuwa sehemu za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta, uwe matoleo yaliyofanywa kwa moto kwa Yahweh, ili kutoa harufu nzuri ya kupendeza, pamoja na hiyo kutakuwa na matoleo ya kinywaji ya divai, moja ya nne ya hini.
And the meal-offering thereof shall be two tenth parts of an ephah of fine flour mingled with oil, an offering made by fire unto the LORD for a sweet savour; and the drink-offering thereof shall be of wine, the fourth part of a hin.
14 Hamtakula mkate, wala nafaka iliyokaangwa au nafaka mpya hata siku ile mliyoleta matoleo haya kwa Mungu wenu. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu, popote pale mnapoishi.
And ye shall eat neither bread, nor parched corn, nor fresh ears, until this selfsame day, until ye have brought the offering of your God; it is a statute for ever throughout your generations in all your dwellings.
15 Tangu siku iliyofuata baada ya Sabato—hiyo ilikuwa siku mlipolileta lie fungu la nafaka la matoleo ya kutikiswa—hesabuni majuma saba kamili.
And ye shall count unto you from the morrow after the day of rest, from the day that ye brought the sheaf of the waving; seven weeks shall there be complete;
16 Mtahesabu siku hamsini, ambazo zingekuwa siku baada ya Sabato ya saba. Kisha mtaleta matoleo ya nafaka mpya kwa Yahweh.
even unto the morrow after the seventh week shall ye number fifty days; and ye shall present a new meal-offering unto the LORD.
17 Mtaleta kutoka nyumbani mwenu mikate miwili iliyotengenezwa kutokana na mbili za kumi za efa. Ni lazima ifanywe kwa unga laini na uliochanganywa na hamira; zitakuwa matoleo ya kutikiswa ya malimbuko ya kwanza kwa Yahweh.
Ye shall bring out of your dwellings two wave-loaves of two tenth parts of an ephah; they shall be of fine flour, they shall be baked with leaven, for first-fruits unto the LORD.
18 Mtaileta hiyo mikate pamoja na wana—kondoo saba wa mwaka mmoja na wasiokuwa na dosari, fahali mmoja mchanga na dume wa kondoo wawili. Watakuwa matoleo ya kuteketezwa kwa moto kwa Yahweh, pamoja na matoleo yao ya nafaka na matoleo ya kinywaji, matoleo yaliyofanywa kwa moto na kutoa harufu nzuri ya kupendeza kwa Yahweh.
And ye shall present with the bread seven lambs without blemish of the first year, and one young bullock, and two rams; they shall be a burnt-offering unto the LORD, with their meal-offering, and their drink-offerings, even an offering made by fire, of a sweet savour unto the LORD.
19 Ni lazima mtowe mbuzi dume mmoja kwa ajili ya matoleo ya dhambi, na wana—kondoo dume wawili wa mwaka mmoja kwa ajili ya dhabihu, wawe matoleo ya ushirika.
And ye shall offer one he-goat for a sin-offering, and two he-lambs of the first year for a sacrifice of peace-offerings.
20 Ni lazima kuhani azitikise pamoja na mkate wa malimbuko ya kwanza mbele za Yahweh na kuzileta kwake kuwa matoleo pamoja na kondoo dume wawili. Watakuwa sadaka takatifu kwa Yahweh kwa ajili ya kuhani.
And the priest shall wave them with the bread of the first-fruits for a wave-offering before the LORD, with the two lambs; they shall be holy to the LORD for the priest.
21 Mtatoa tangazo siku iyo hiyo. Kutakuwa na kusanyiko takatifu, na hamtafanya kazi za kawaida. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vya watu wenu mahali pote mnapoishi.
And ye shall make proclamation on the selfsame day; there shall be a holy convocation unto you; ye shall do no manner of servile work; it is a statute for ever in all your dwellings throughout your generations.
22 Mtakapovuna mazao ya nchi yenu, Msivune kabisa kabisa pembeni mwa mashamba yenu, wala msivune mazazo ya mavuno yenu. Inawapasa kuyaacha kwa ajili ya masikini na mgeni. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.”
And when ye reap the harvest of your land, thou shalt not wholly reap the corner of thy field, neither shalt thou gather the gleaning of thy harvest; thou shalt leave them for the poor, and for the stranger: I am the LORD your God.
23 Yahweh akazungumza na Musa, akisema,
And the LORD spoke unto Moses, saying:
24 “Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, “Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza itakuwa siku ya pumzika makini kwa ajili yenu, kumbukumbu pamoja na kupigwa kwa tarumbeta na kusanyiko takatifu,
Speak unto the children of Israel, saying: In the seventh month, in the first day of the month, shall be a solemn rest unto you, a memorial proclaimed with the blast of horns, a holy convocation.
25 Hamtafanya kazi ya kawaida, na ni lazima mtoe dhabihu inayofanywa kwa moto kwa Yahweh.”
Ye shall do no manner of servile work; and ye shall bring an offering made by fire unto the LORD.
26 Kisha Yahweh akamwambia Musa, akisema,
And the LORD spoke unto Moses, saying:
27 “Sasa, siku ya kumi ya mwezi huu wa saba, ni Siku ya Upatanisho. Kutakuwa na kusanyiko takatifu, na ni lazima mjinyenyekeze na kuleta kwa Yahweh matoleo kwa moto.
Howbeit on the tenth day of this seventh month is the day of atonement; there shall be a holy convocation unto you, and ye shall afflict your souls; and ye shall bring an offering made by fire unto the LORD.
28 Hamtafanya kazi katika siku hiyo kwa sababu ni Siku ya Upatanisho, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu mbele za Yahweh Mungu wenu.
And ye shall do no manner of work in that same day; for it is a day of atonement, to make atonement for you before the LORD your God.
29 Yeyote asiyejinyenyekeza siku hiyo lazima akatiliwe mbali na watu wake.
For whatsoever soul it be that shall not be afflicted in that same day, he shall be cut off from his people.
30 Yeye afanyaye kazi yoyote katika siku hiyo, Mimi, Yahweh, nitamwangamiza atoke miongoni mwa watu wake.
And whatsoever soul it be that doeth any manner of work in that same day, that soul will I destroy from among his people.
31 Msifanye kazi ya aina yoyote katika siku hiyo. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu mahali pote mnapoishi.
Ye shall do no manner of work; it is a statute for ever throughout your generations in all your dwellings.
32 Siku hii itakuwa Sabato ya pumziko lenye utlivu, na ni lzima siku ya tisa ya mwezi mjinyenyekeze katika majira ya jioni. Tangu jioni hata jioni mtaishika Sabato yenu.”
It shall be unto you a sabbath of solemn rest, and ye shall afflict your souls; in the ninth day of the month at even, from even unto even, shall ye keep your sabbath.
33 Yahweh akazungumza na Musa, akisema,
And the LORD spoke unto Moses, saying:
34 “Zungumza na watu ISraeli, uwaambie 'Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba kutakuwa na Sikukuu ya vibanda kwa Yahweh. nayo itadumu siku saba.
Speak unto the children of Israel, saying: On the fifteenth day of this seventh month is the feast of tabernacles for seven days unto the LORD.
35 Siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko takatifu. Hamtafanya kazi ya kawaida.
On the first day shall be a holy convocation; ye shall do no manner of servile work.
36 Kwa muda wa siku saba mtatoa dhabihu iliyofanywa kwa moto kwa Yahweh. Siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu, nanyi mtato dhabihu iliyofanywa kwa moto kwa Yahweh. Hili ni kusanyiko lenye utulivu, nanyi msifanye kazi yoyote ya kawaida.
Seven days ye shall bring an offering made by fire unto the LORD; on the eighth day shall be a holy convocation unto you; and ye shall bring an offering made by fire unto the LORD; it is a day of solemn assembly; ye shall do no manner of servile work.
37 Hizi ndizo sikukuu zilizoamriwa kwa ajili ya Yahweh, ambazo mnapaswa kuzitangaza kuwa ni makusanyiko matakatifu ya kutoa dhabihu kwa moto kwa Yahweh, matoleo ya kuteketezwa na matoleo ya nafaka, dhabihu na matoleo ya vinywaji, kila moja kwa siku yake.
These are the appointed seasons of the LORD, which ye shall proclaim to be holy convocations, to bring an offering made by fire unto the LORD, a burnt-offering, and a meal-offering, a sacrifice, and drink-offerings, each on its own day;
38 Sikukuu hizi zitakuwa nyongeza kwa Sabato za Yahweh na zawadi zenu, viapo vyenu vyote, na sadaka zenu zote za hiari mzitoazo kwa Yahweh.
beside the sabbaths of the LORD, and beside your gifts, and beside all your vows, and beside all your freewill-offerings, which ye give unto the LORD.
39 Kuhusu Sikukuu ya vibanda, siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, mtakapokuwa mmeyakusanya ndani matunda ya nchi, ni lazima muitunze sikukuu hii ya Yehweh kwa muda wa siku saba. Siku ya kwanza itakuwa ya pumziko lenye utulivu, na siku ya nane pia itakuwa ya pumziko lenye utulivu.
Howbeit on the fifteenth day of the seventh month, when ye have gathered in the fruits of the land, ye shall keep the feast of the LORD seven days; on the first day shall be a solemn rest, and on the eighth day shall be a solemn rest.
40 Siku ya kwanza mtachuma tunda lililobora kutoka kwenye miti, mtakata makuti ya mtende, na matawi ya miti minene yenye majani mengi, na majani ya mierebi kutoka chemchemi za maji, nanyi mtashangilia mbele za Yahweh Mungu wenu kwa siku saba.
And ye shall take you on the first day the fruit of goodly trees, branches of palm-trees, and boughs of thick trees, and willows of the brook, and ye shall rejoice before the LORD your God seven days.
41 Kwa muda wa siku saba kila mwaka, mtaisherehekea sikukuu hii kwa Yahweh. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu mahali potepote mtakapoishi. Mtaisherehekea sikukuu hii katika mwezi wa saba.
And ye shall keep it a feast unto the LORD seven days in the year; it is a statute for ever in your generations; ye shall keep it in the seventh month.
42 Mtaishi kwenye vibanda vidogovidogo kwa siku saba. Waisraeli wenyeji wa kuzaliwa wote itawapasa kuishi katika vibanda vidogovidogo kwa siku saba,
Ye shall dwell in booths seven days; all that are home-born in Israel shall dwell in booths;
43 ili kwamba wazao wenu, kizazi baada ya kizazi, waweze kujifunza nilivyowafanya wana wa Israeli kuishi kwenye vibanda kama hivi nilipowaongoza kutoka katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.'”
that your generations may know that I made the children of Israel to dwell in booths, when I brought them out of the land of Egypt: I am the LORD your God.
44 Katika njia hii Musa akazitangaza kwa watu wa ISraeli sikukuu zilizoamria kwa ajili ya Yahweh.
And Moses declared unto the children of Israel the appointed seasons of the LORD.