< Mambo ya Walawi 22 >
1 Yahweh akazungumza na Musa, kusema,
2 “Ongea na Aroni na wanawe, waambie wajiepushe na vitu vitakatifu vya watu wa Israeli wanavyovitenga kwangu. Wasilinajisi jina langu. Mimi ndimi Yahweh.
3 Waambie, 'Ikiwa mmoja wa wazao wenu katika vizazi vyenu vyote anakaribia vitu vitakatiifu vile ambavyo watu wa Israeli wamevitenga kwa Yahweh, wakati akiwa najisi, sharti mtu huyo akatiliwe mbali atoke mbele zangu. Mimi ndimi Yahweh.
4 Hatakuwapo yeyote wa uzao wa Aroni aliye na ungonjwa wa ngozi wa kuambukiza, au maambukizi yatirirkayo kutoka mwilini mwake, atakayekula sehemu yoyote ya dhabihu inatolewayo kwa Yahweh mpaka atakapotakasika. Yeyote agusaye kitu chochote kilichonajisi kwa njia ya kugusa maiti, au kwa kumgusa mtu yeyote aliyetokwa na shahawa,
5 au yeyote agusaye mnyama atakayemtia unajisi, au mtu yeyote atakayemfanya najisi, kwa hiyo unajisi wowote unaweza kuwa—
6 kuhani yeyote agusaye kitu chochote kisichosafi atakuwa najisi hata jioni. Hatakula chochote cha vitu vitakatifu, isipokuwa ameuosha mwili wake katika maji.
7 Jua linapotua, ndipo atakuwa safi. Baada ya machweo anaweza kula kutoka katika vitu vitakatifu, kwasababu hivyo ni vyakuala vyake.
8 Asile mzoga wowote uliookotwa au mnyama aliyeraruliwa na wanyama pori, ambaye kwake atajitia unajisi. Mimi ndimi Yahweh.
9 Ni lazima makuhani wafuate maagizo yangu, ama sivyo watakuwa na hatia ya dhambi na wangeweza kufa kwa kunitia unajisi. Mimi ndimi Yahweh ninayewafanya wao watakatifu.
10 Hakuna mtu kutoka nje ya familia ya kuahani, wakiwemo wageni wa kuhani au watumwa wake wa kuajiliwa, atakayeweza kula kitu chochote kilicho kitakatifu.
11 Lakini kama huyo kuhani amenunua mtumwa kwa fedha yake mwenyewe, mtumwa huyo anaweza kula kutoka katika vitu vilivyotengwa kwa Yahweh. Na watu wa familia ya kuhani na watumwa waliozaliwa nyumbani mwake, pia wanaweza kula pamoja naye kutoka katika vitu hivyo.
12 Ikiwa binti wa kuhani ameolewa na mtu asiye kuhani, hataweza kula chochote cha mchango wa matoleo matakatifu.
13 Lakini ikiwa huyo binti wa kuhani ni mjane au ametalikiwa, na ikiwa hana mtoto, na anarudi kuishi knyumbani kwa baba yake kama alivyokuwa wakati wa ujana wake, anaweza kula kutoka katika chakula cha baba yake. Lakini hakuna yeyote asiye wa familia ya kikuhani anatakayeruhusiwa kula kutoka katika chakula cha kuhani.
14 Kama mtu anakula chakula kitakatifu bila ya kukijua, naye atamlipa kuahani kwa ajili ya hicho; itampasa kuongeza moja ya tano juu yake na kukirejesha kwa kuhani.
15 Haiwapasi watu wa Israeli kutoheshimu vitu vitakatifu ambavyo vimeinuliwa juu na kuletwa kwa Yahweh,
16 kisha wakajisababishia wenyewe kuchukua dhambi amabyo ingewafanya kuwa na hatia ya kula chakula kitakatifu, kwa kuwa mimi ndimi Yahweh awafanyaye wao watakatifu.”
17 Yahweh akazungumza na Musa, akasema,
18 “Sema na Aroni na wanawe, na kwa watu wa Israeli wote. Waambie, Mwisraeli yeyote, au Mgeni anayeishi katika Israeli, waletapo dhabihu—iwe ni kutimiza kiapo, au iwe ni sadaka ya hiari, au wanaleta kwa Yahweh sadaka ya kuteketezwa kwa moto,
19 ikiwa wanataka ikubalike, ni lazima watowe mnyama dume asiye na dosari, kutoka kwenye kundi la ng'ombe, kondoo au mbuzi
20 Lakini hamtatoa chochote kilicho na dosari. Sitakipokea kwa niaba yenu.
21 Yeyote atoae dhabihu ya sadaka ya ushirika kutoka katika kundi la ng'ombe au la kondoo kwa Yahweh ili kutimiza kiapo, au kama sadaka ya hiari, ili ikubalike, ni lazima isiwe na kilema. Ni lazima pasiweko na kasoro katika mnyama.
22 Msitoe kabisa wanyama waliovipofu, waliojeruhiwa, wala walio na kilema, wenye upele, vidonda vitokavyo usaha, wala wenye vigaga. Msiwatoe hawa kuwa dhabihu ya kuteketezwa kwa moto iliyotolewa kwa Yahweh juu ya madhabahu.
23 Unaweza kumleta makisai au mwana-kondoo mlemavu au aliyedumaa kuwa sadaka ya hiari, lakini sadaka kama hiyo kwa ajili kutimiza kiapo, haitapokelewa.
24 Usitoe kwa Yahweh mnyama yeyote aliyetiwa jeraha, kupondwa, au kukatwa korodani zake.
25 Usifanye haya katika nchi yako. Usilete mkate wa Mungu wako kutoka mkononi mwa mgeni. Hao wanyama wenye vilema na dosari ndani yao, hawatapokelewa kabisa kwa ajili yako.
26 Yahweh akamwambia Musa na akasema,
27 “Wakati ndama, mwana—kondo au mwana—mbuzi azaliwapo, sharti abaki na mama yake kwa muda wa siku saba. Ndipo kuanzia siku ya nane na kuendelea, anaweza kupokelewa kuwa dhabihu iliyofanywa kwa moto kwa Yahweh.
28 Usimchinje ng'ombe jike pamoja na ndama wake au mbuzi jike pamoja na kitoto chake kwa siku moja.
29 Utoapo sadaka ya shukrani kwa Yahweh utaitoa kwa njia iliyokubalika.
30 Ni lazima iliwe siku iyo hiyo inayotolewa. Hutakiwi kubakiza chochote hata asubuhi. Mimi ndimi Yahweh.
31 Kwa hiyo imewapasa kuzishika amri zangu na kuzifuata. Mimi ndimi Yahweh.
32 Msiliabishe jina langu takatifu. Ni lazima nitambuliwe kuwa ni mtakatifu na watu wa Israeli. Mimi ndimi Yahweh niwafanyaye ninyi watakatifu,
33 ambaye amewaleta kutoka katika nchi ya Misri ili niwe Mungu wenu: Mimi ndimi Yahweh.”