< Mambo ya Walawi 17 >
1 Yahweh akamwambia Musa,
여호와께서 모세에게 일러 가라사대
2 “Zungumza na Aroni na wanawe, na watu wote wa Israeli. Waambie mambo ambayo ameamru Yahweh:
아론과 그 아들들과 이스라엘 모든 자손에게 고하여 그들에게 이르기를 여호와의 명령이 이러하시다 하라
3 Mtu yeyote wa Isreli anayeua fahali au mwana—kondoo au mbuzi kambini, au amuuaye nje ya kambi, ili kumtoa dhabihu—
무릇 이스라엘 집의 누구든지 소나 어린 양이나 염소를 진 안에서 잡든지 진 밖에서 잡든지
4 kama hamleti katika ingilio la hema la kukutania ili kumtoa dhabihu kwa Yahweh mbele za hema lake la kukutania, mtu huyo ana hatia ya damu iliyomwagika. Amemwaga damu, na mtu huyo ni sharti akatiliwe mabali kutoka miongoni mwa watu wake.
먼저 회막문으로 끌어다가 여호와의 장막 앞에서 여호와께 예물로 드리지 아니하는 자는 피흘린 자로 여길 것이라 그가 피를 흘렸은즉 자기 백성 중에서 끊쳐지리라!
5 Kusudi la amri hii ni kwamba watu wa Israeli wataleta dhabihu zao kwa Yahweh kwenye ingilio la hema la kukutania, watazileta kwa kuhani ziweze kutolewa kuwa matoleo ya shukrani kwa Yahweh, badala ya kutoa dhabihu hadharani katika shamba.
그런즉 이스라엘 자손이 들에서 잡던 희생을 회막 문 여호와께로 끌어다가 제사장에게 주어 화목제로 여호와께 드려야 할 것이요
6 Kuhani atainyunyiza damu juu ya madhabahu ya Yahweh kwenye ingilio la hema la kukutania; atayachoma mafuta yake ili kutoa harufu ya kupendeza mbele za Yahweh.
제사장은 그 피를 회막 문 여호와의 단에 뿌리고 그 기름을 불살라 여호와께 향기로운 냄새가 되게 할 것이라
7 Ni lazima watu wasitoe tena dhabihu zao kwa sanamu za mbuzi, ambazo kwazo hutenda kama makahaba. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa ajili yao katika vizazi vya watu wao vyote.
그들은 전에 음란히 섬기던 수염소에게 다시 제사하지 말 것이니라 이는 그들이 대대로 지킬 영원한 규례니라!
8 Ni lazima uwaambie, 'Mtu yeyote wa Israeli, au Mgeni yeyote aishiye miongoni mwao, atoweye dhabihu
너는 또 그들에게 이르라 무릇 이스라엘 집 사람이나 혹시 그들중에 우거하는 타국인이 번제나 희생을 드리되
9 na asiilete kwenye ingilio la hema la kukutania ili kuitoa kwa Yahweh, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.'
회막 문으로 가져다가 여호와께 드리지 아니하면 그는 백성 중에서 끊쳐지리라!
10 Na Mtu yeyote wa Israeli, au yeyote wa Wageni anayeishi miongoni mwao, ambaye hunywa damu; nitamkatilia mbali atoke miongoni mwa watu wake.
무릇 이스라엘 집 사람이나 그들 중에 우거하는 타국인 중에 어떤 피든지 먹는 자가 있으면 내가 그 피 먹는 사람에게 진노하여 그를 백성중에서 끊으리니
11 Kwa kuwa uhai wa mnyama yeyote umo katika damu yake. Nimeitoa damu yake kwenu kufanya upatanisho juu ya madhabahu kwa ajili ya uhai wenu, kwa sababu ni damu ndiyo ifanyayo upatanisho, kwa kuwa ni damu ipatanishayo kwa ajili ya uhai
육체의 생명은 피에 있음이라 내가 이 피를 너희에게 주어 단에 뿌려 너희의 생명을 위하여 속하게 하였나니 생명이 피에 있으므로 피가 죄를 속하느니라
12 Kwa hiyo Niliwaambia Watu wa Israeli kwamba hayupo miongoni mwenu impasaye kula damu, wala yeyote wa Wageni aishiye miongoni mwenu atakaye kula damu.
그러므로 내가 이스라엘 자손에게 말하기를 너희 중에 아무도 피를 먹지 말며 너희 중에 우거하는 타국인이라도 피를 먹지 말라 하였나니
13 Na yeyote miongoni mwa watu wa Israeli, au yeyote wa Wageni aishiye miongoni mwenu ni lazima aimwage damu ya mnyama na kuifukia hiyo damu kwa mafumbi.
무릇 이스라엘 자손이나 그들 중에 우거하는 타국인이 먹을 만한 짐승이나 새를 사냥하여 잡거든 그 피를 흘리고 흙으로 덮을지니라
14 Kwa kuwa uhai wa kila kiumbe umo katika damu yake. Ni kwa sababu hii niliwaambia watu wa Israeli, ni lazima msile damu ya kiumbe cho chote, kwa kuwa maisha ya kila kiumbe chenye uhai ni damu yake. Yeyeote ailaye ni lazima akatiliwe mbali.
모든 생물은 그 피가 생명과 일체라 그러므로 내가 이스라엘 자손에게 이르기를 너희는 어느 육체의 피든지 먹지 말라 하였나니 모든 육체의 생명은 그 피인즉 무릇 피를 먹는 자는 끊쳐지리라!
15 Mtu yeyote alaye mnyama aliyekufa au ambaye amelaruliwa na wanyama pori, ama yule mtu ni mwenyeji wa kuzaliwa au ni mgeni aishiye miongoni mwenu, ni lazima atazifua nguo zake na kujiosha katika maji, naye atakuwa najisi hata jioni. Kisha atakuwa safi.
무릇 스스로 죽은 것이나 들짐승에게 찢겨 죽은 것을 먹은 자는 본토인이나 타국인이나 물론하고 그 옷을 빨고 물로 몸을 씻을 것이며 저녁까지 부정하고 그 후에 정하려니와
16 Lakini kama hazifui nguo zake au kuosha mwili wake, ni lazima aichukue hatia yake”.
그가 빨지 아니하거나 몸을 물로 씻지 아니하면 죄를 당하리라