< Mambo ya Walawi 12 >
1 Yahweh akamwambia Musa,
2 “zungumza na watu wa Israeli, uwaambie, 'endapo mwanamke anakuwa mjamzito na kujifungua mtoto wa kiume, naye atakuwa najisi kwa muda wasiku saba, ni kama tu vile anavyokuwa najisi katika siku za kipindi chake kwa mwezi.
3 Katika siku ya nane nyama ya govi la mtoto mvulana itatahiriwa.
4 Kisha utakaso wa mama wa kutokwa damu yake utaendelea kwa muda wa siku tatu. Haimpasi kugusa kitu chochote kilicho kitakatifu au kukaribia eneo la hema mpaka zitakapomalizika siku za kutakaswa kwake.
5 Lakini kama atajifungua mtoto wa kike, naye atakuwa najisi kwa mud wa majuma mawili, kama alivyo wakati wa kipindi chake. Kisha utakaso wa mama utaendelea kwa siku sitini sita.
6 Siku za kutakaswa kwake zitakapoisha, kwa ajili ya mwana au binti, atalazimika kuleta kwa kuhani mwana-kondoo wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa, na kinda la njiwa au huwa kuwa sadaka ya dhambi, mbele ya ingilio la hema la kukutania,
7 Kisha atawatoa mbele za Yahweh na kufanya sadaka ya upatanisho kwa ajili yake, naye atatakaswa kutokana kutiririka kwa damu yake. Hii ndiyo sheria kuhusu mwanamke aifunguaye ama mtoto wa kiume au wa kike.
8 Na kama hana uwezo wa kutoa mwana-kondoo, naye ataleta makinda mawili ya njiwa ua hua, mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na mwingine kuwa sadaka ya dhambi, naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake; naye atakuwa safi.”