< Mambo ya Walawi 11 >

1 Yahweh akazungumza na Musa na Aroni, akasema,
Bwana akawaambia Mose na Aroni,
2 “Sungumzeni na watu wa Israeli muwaambie, 'Hivi ndivyo viumbe vyenye uhai ambavyo mwaweza kula miongoni mwa wanyama walioko juu ya nchi.
“Waambieni Waisraeli: ‘Kati ya wanyama wote waishio juu ya nchi, hawa ndio mtakaowala:
3 Mnaweza kula mnyama yeyote aliye na kwato zenye kugawanyika na ambaye pia hucheua.
Mwaweza kula mnyama yeyote mwenye kwato zilizogawanyika sehemu mbili na ambaye hucheua.
4 Hata hivyo, kuna baadhi ya wanyama ambao ama hawacheui au hana kwato zilizogawanyika, nanyi msiwale hao, wanyama kama ngamia, kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato zilizogawanyika. Kwa hiyo ngamia ni najisi kwenu.
“‘Kuna wanyama wengine ambao hucheua tu au wenye kwato zilizogawanyika tu, lakini hao kamwe msiwale. Ngamia ingawa hucheua hana kwato zilizogawanyika; kwa kawaida ya ibada hiyo ni najisi kwenu.
5 Pimbi pia: kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato zilizogawanyika mara mbili, huyo pia ni najisi kwenu.
Pelele ingawa hucheua hana kwato zilizogawanyika; huyo ni najisi kwenu.
6 Na sungura pia: kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato zilizogawanyika mara mbili, huyu naye ni najisi kwenu.
Sungura ingawa hucheua hana kwato zilizogawanyika; huyo ni najisi kwenu.
7 Na nguruwe pia: ingawaje yeye anazo kwato zilizogawanyika lakini hacheui, kwa hiyo yeye ni najisi kwenu.
Naye nguruwe ingawa anazo kwato zilizogawanyika sehemu mbili, hacheui; huyo ni najisi kwenu.
8 Msile aina yoyote ya nyama yao, wala msiiguse mizoga yao. Hao ni najisi kwenu.
Kamwe msile nyama yao wala kugusa mizoga yao; wao ni najisi kwenu.
9 Nao wanyama waishio majini mnaoweza kuwala ni wale wote walio na mapezi na magamba, iwe waliomo baharini au mitoni.
“‘Kuhusu viumbe wote wanaoishi ndani ya maji ya bahari na vijito, mtakula wale wote wenye mapezi na magamba.
10 Lakini viumbe wote hai wasio na mapezi na magamba waliomo baharini au mitoni, pamoja na wale waendao majini na viumbe hai waliomo majini —watakuwa chukizo kwenu.
Lakini viumbe wote ndani ya bahari au vijito wasio na mapezi na magamba, wakiwa miongoni mwa makundi au viumbe wote ndani ya maji, hao ni machukizo kwenu.
11 Kwa kuwa watakuwa chukizo, msile nyama yao, pia mizoga yao sharti itakuwa chukizo.
Nao watakuwa machukizo kwenu. Msile nyama yao, nayo mizoga yao itakuwa machukizo.
12 Chochote kisichokuwa na mapezi au magamba kilichomo majini ni lazima kiwe chukizo kwenu.
Chochote kinachoishi ndani ya maji ambacho hakina mapezi na magamba kitakuwa chukizo kwenu.
13 Nao ndege mtakaowachukia na msiopaswa kuwala ni hawa wafuatao: tai, furukombe, kipungu,
“‘Wafuatao ndio ndege watakaokuwa machukizo kwenu, hivyo msiwale kwa sababu ni chukizo: tai, furukombe, kipungu,
14 mwewe mwekundu, aina yoyote ya kipanga,
mwewe mwekundu, aina zote za mwewe mweusi,
15 kila aina ya kunguru,
aina zote za kunguru,
16 kiruka-njia, kipasuasanda, Shakwe, na aina yoyote ya mwewe.
mbuni, kiruka-njia, dudumizi, kipanga, shakwe, aina zote za kipanga,
17 Ni lazima pia bundi mdogo na bundi mkubwa muwaone kuwa chukizo, mnandi,
bundi, mnandi, bundi mkubwa,
18 bundi mweupe na mwari,
mumbi, mwari, nderi,
19 korongo na ina zote za koikoi, huduhudi na popo pia.
korongo, koikoi wa aina yoyote, hudihudi na popo.
20 Wadudu wote wenye mabawa wanatembea kwa miguu minne kwenu ni machukizo.
“‘Wadudu wote warukao ambao hutembea kwa miguu minne watakuwa chukizo kwenu.
21 Lakini manaweza kula wadudu wenye mabawa wanaotembea kwa miguu minne ya kurukia ardhini yenye vifundo.
Lakini wako viumbe wenye mabawa ambao hutembea kwa miguu minne mtakaowala: wale wenye vifundo katika miguu yao ya kurukaruka juu ya ardhi.
22 Na manaweza kula kula aina zote za nzige, senene, parare, au panzi.
Miongoni mwa hawa, mtakula nzige wa aina zote, senene, parare au panzi.
23 Lakini wadudu wote warukao wenye miguu minne ni chulkizo kwenu.
Lakini viumbe wengine wote wenye mabawa na wenye miguu minne ni machukizo kwenu.
24 Nanyi mtakuwa najisi hata jioni kutokana na wanyama hawa endapo mtagusa mizogo yao.
“‘Mtajinajisi kwa wanyama hawa. Yeyote agusaye mizoga yao atakuwa najisi mpaka jioni.
25 Na yeyote atakayeokota mojawapo wa mizoga yao ni lazima atazifua ngua zake naye atakuwa najisi hata jioni.
Yeyote atakayebeba mizoga ya viumbe hawa ni lazima afue nguo zake, naye atakuwa najisi mpaka jioni.
26 Mnyama yeyote ambaye anazo kwato ziliachana ambazo hazikugawanyika kabisa au hacheui huyo ni najisi kwenu. Yeyote awagusaye atakuwa najisi.
“‘Kila mnyama mwenye ukwato ulioachana lakini haukugawanyika kabisa, au yule asiyecheua, huyo ni najisi kwenu; yeyote agusaye mzoga wowote wa hao atakuwa najisi.
27 Mnyama yeyote anayetembea kwa vitanga vyake miongoni mwa wanyama waendao kwa miguu yote minne ni najisi kwenu. Yeyote agusaye mzoga kama huo atakuwa najisi hata jioni.
Miongoni mwa wanyama wote watembeao kwa miguu minne, wale watembeao kwa vitanga vyao ni najisi kwenu; yeyote agusaye mizoga yao atakuwa najisi mpaka jioni.
28 Na yeyote aokotaye mzoga kama huo ni zazima atazifua nguo zake na kuwa najisi hata jioni. Wanyama hawa watakuwa najisi kwenu.
Yeyote atakayebeba mizoga yao ni lazima afue nguo zake, naye atakuwa najisi mpaka jioni. Wanyama hawa ni najisi kwenu.
29 Kuhusiana na wanyama wataambaao juu ya ardhi, hawa ndiyo walio najisi kwenu: kicheche, panya, aina zote za mijusi mikubwa, guruguru,
“‘Kuhusu wanyama watambaao juu ya ardhi, hawa ni najisi kwenu: kicheche, panya, aina yoyote ya mijusi mikubwa,
30 kenge, mijusi ya ukutani, goromoe, na kinyonga.
guruguru, kenge, mijusi ya ukutani, goromoe na kinyonga.
31 Wanyama hawa wote ambao hutambaa, hawa ndiyo watakuwa najisi kwenu. Yeyote awagusaye atakuwa njisi hata jioni.
Hao wote watambaao juu ya ardhi ni najisi kwenu. Yeyote agusaye mizoga yao atakuwa najisi mpaka jioni.
32 Na iwapo mmoja wao anakufa na kuanguka juu ya chombo, chombo hicho kitakuwa najisi, ama kiwe kimetengenezwa kwa mbao, nguo, ngozi, au gunia. Kiwe chombo cha namna gani na kiwe kwa matumizi gani, ni lazima kitalowekwa katika maji nacho kitakuwa najisi hata jio. Kisha kitakuwa safi.
Ikiwa mmoja wao atakufa na kuangukia juu ya kitu fulani, chombo hicho, hata kikiwa cha matumizi gani, kitakuwa najisi, kiwe kimetengenezwa kwa mti, nguo, ngozi au gunia. Kiweke ndani ya maji; kitakuwa najisi mpaka jioni, kisha kitakuwa safi tena.
33 Kwa hiyo kila chungu ambacho mnyama najisi atakiangukia juu yake au ndani yake, chochote kilichomo kwenye chungu hicho kitakuwa najisi, na ni lazima mtakivunja chungu hicho.
Ikiwa mmoja wa wanyama aliyekufa ataangukia ndani ya chungu, kila kilichomo katika chungu hicho kitakuwa najisi, nawe ni lazima uvunje chungu hicho.
34 Vyakula vyote ambavyo ni safi na kilichuhusiwa kuliwa, lakini kikaingiwa na maji kutoka kwenye chungu najisi kilichoanguka, nacho kitakuwa najisi.
Chakula chochote ambacho chaweza kuliwa lakini kikawa kimeingia maji kutoka kwenye chungu hicho ni najisi, na kitu chochote cha majimaji ambacho chaweza kunyweka kutoka kwenye chungu hicho ni najisi.
35 Na kitu chochote kinachoweza kunywewa kutoka kwenye chungu kama hicho kitakuwa najisi. Kila kitu kitakachoangukiwa juu yake na kipande cha mzoga wa mnyama najisi nacho kitakuwa najisi, ama liwe ni jiko au vyungu vya kupikia. Ni najisi na ni lazima kiwe najisi kwenu.
Chochote ambacho mzoga wa mmojawapo utaangukia kitakuwa najisi. Jiko au chungu cha kupikia ni lazima kivunjwe. Ni najisi, nawe ni lazima uvihesabu kuwa najisi.
36 Chemchemi au kisima cha maji ya kunywa yanapokusanyika patabaki kuwa safi iwapo kiumbe najisi kama hicho kitaangukia humo. Lakini ikiwa yeyote anaugusa mzoga wa mnyama aliye najisi uliomo ndani ya maji, yeye atakuwa najisi.
Lakini chemchemi au kisima, mahali pa kuchota maji, patakuwa safi, lakini yeyote atakayegusa moja ya mizoga hii ni najisi.
37 Iwapo sehehemu yoyote ya mzoga wa mnyama aliyenajisi inaangukia juu ya mbegu zozote zilizo kwa ajili ya kupanda. Mbegu hizo zitakuwa bado zingali safi.
Kama mzoga ukianguka juu ya mbegu zozote ambazo ni za kupanda, zinabaki safi.
38 Lakini kama maji yanawekwa juu ya mbegu, na kama sehemu ya mzoga unaangukia juu yake, nazo zitakuwa najisi kwenu.
Lakini kama mbegu imetiwa maji na mzoga ukaanguka juu yake, hiyo mbegu ni najisi kwenu.
39 Iwapo mnyama yeyote awezaye kuliwa anakufa, naye yeyote amgusaye atakuwa najisi hata jioni.
“‘Kama mnyama ambaye mnaruhusiwa kumla akifa, yeyote atakayeugusa mzoga wake atakuwa najisi mpaka jioni.
40 Na yeyote alaye chochote cha mzoga huo atalazimika kufua nguo zake naye atakuwa anjisi hata jioni. Na yeyote aokotaye mzoga kama huo atafua nguo zake na kuwa najisi hata jioni.
Yeyote atakayekula sehemu ya mzoga huo ni lazima afue nguo zake, naye atakuwa najisi mpaka jioni. Yeyote atakayebeba mzoga huo ni lazima afue nguo zake, naye atakuwa najisi mpaka jioni.
41 Kila mnyama atambaaye juu ya ardhi atakuwa chukizo; hatakuwa wa kuliwa.
“‘Kila kiumbe kitambaacho juu ya ardhi ni chukizo; kisiliwe.
42 Chochote kitambaacho kwa kujivuta juu ya tumbo lake, na chochote kitembeacho kwa miguu yake yote minne, au chochote kilicho na miguu mingi—wanyama wote ambao hutambaa juu ya nchi, hawa msiwale, kwa sababu watakuwa machukizo.
Msile kiumbe chochote kitambaacho juu ya ardhi, kiwe kitambaacho kwa tumbo lake, au kitambaacho kwa miguu minne au kwa miguu mingi; ni chukizo.
43 Msijinajisi wenyewe kwa kiumbe chochote nnajisi kitaambacho; msijinasi wenyewe kwavyo, ili kwamba msije mkachafuliwa navyo.
Msijitie unajisi kwa chochote katika viumbe hivi. Msijitie unajisi kwa viumbe hivyo au kutiwa unajisi navyo.
44 Kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu. Nanyi lazima muwe watakatifu, kwa hiyo na iweni watakatifu, kwa sababu Mimi ni mtakatifu. Haiwapasi kujichafua kwa aina yoyote ya kiendacho juu ya nchi.
Mimi ndimi Bwana Mungu wenu; jitakaseni mwe watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu. Msijitie unajisi wenyewe kwa kiumbe chochote kile kiendacho juu ya ardhi.
45 Kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh, aliyewaleta ninyi kutoka nchi ya Misri, ili niwe Mungu wenu. Kwa hiyo lazima muwe watakatifu, kwa kuwa Mimi ni mtakatifu.
Mimi ndimi Bwana niliyewapandisha mtoke Misri ili niwe Mungu wenu. Kwa hiyo kuweni watakatifu kwa sababu Mimi ni mtakatifu.
46 Hii ndiyo sheria kuhusu wanyama, ndege, kila kiumbe hai kiendacho majini, na ya kila kiumbe kitambaacho juu ya nchi,
“‘Haya ndiyo masharti kuhusu wanyama, ndege, kila kiumbe hai kiendacho ndani ya maji, na kila kiumbe kiendacho juu ya ardhi.
47 kwa jili ya kilie kinachopaswa kutofautishwa kati ya kilicho najisi na kilicho safi, na kati ya vitu vilivyokufa na vilivyo hai ambavyo vyaweza kuliwa na vitu vyenye uihai visivyoweza kuliwa.”
Ni lazima mpambanue kati ya kilicho najisi na kilicho safi, kati ya viumbe hai vinavyoweza kuliwa na vile visivyoweza kuliwa.’”

< Mambo ya Walawi 11 >