< Maombolezo 5 >
1 Kumbuka, Yahweh, yaliyo tutokea na uone aibu yetu.
Kumbuka, Ee Bwana, yaliyotupata, tazama, nawe uione aibu yetu.
2 Urithi wetu umegeuziwa kwa wageni; nyumba zetu kwa wageni.
Urithi wetu umegeuziwa kwa wageni, na nyumba zetu kwa wageni.
3 Tumekuwa yatima, bila baba, na mama zetu ni kama wajane.
Tumekuwa yatima wasio na baba, mama zetu wamekuwa kama wajane.
4 Lazima tulipe fedha kwa maji tunayo kunywa, na tulipe fedha kupata mbao zetu.
Ni lazima tununue maji tunayokunywa, kuni zetu zapatikana tu kwa kununua.
5 Hao wanakuja kwetu wamekaribia nyuma yetu; tumechoka na hatuwezi pata mapumziko.
Wanaotufuatilia wapo kwenye visigino vyetu, tumechoka na hakuna pumziko.
6 Tumejitoa kwa Misri na kwa Assiria tupate chakula cha kutosha.
Tumejitolea kwa Misri na Ashuru tupate chakula cha kutosha.
7 Baba zetu walifanya dhambi, na hawapo tena, na tumebeba dhambi zao.
Baba zetu walitenda dhambi na hawapo tena, na sisi tunachukua adhabu yao.
8 Watumwa walitutawala, na hakuna wa kutuokoa na mikono yao.
Watumwa wanatutawala na hakuna wa kutuokoa mikononi yao.
9 Tunapata mkate wetu pale tunapo hatarisha maisha, kwasababu ya upanga wa nyikani.
Tunapata chakula chetu kwa kuhatarisha maisha yetu kwa sababu ya upanga jangwani.
10 Ngozi zetu zimekuwa na moto kama jiko kwasababu ya joto la njaa.
Ngozi yetu ina joto kama tanuru, kwa sababu ya fadhaa itokanayo na njaa.
11 Wanawake wanabakwa Sayuni, na mabikra katika mji wa Yuda.
Wanawake wametendwa jeuri katika Sayuni, na mabikira katika miji ya Yuda.
12 Watoto wa mfalme wamenyongwa na mikono yao, na hakuna heshima inayoonyeshwa kwa wazee.
Wakuu wametungikwa juu kwa mikono yao, wazee hawapewi heshima.
13 Wanaume vijana wanalizimishwa kusaga mbegu kwa jiwe la kusagia, na wavulana wanajikwa chini ya vifurushi vya kuni.
Vijana wanataabika kwenye mawe ya kusagia, wavulana wanayumbayumba chini ya mizigo ya kuni.
14 Wazee wameacha lango la mji, na vijana wameacha miziki.
Wazee wameondoka langoni la mji, vijana wameacha kuimba nyimbo zao.
15 Furaha ya moyo imekoma na kucheza kwetu kumegeuka kilio.
Furaha imeondoka mioyoni mwetu, kucheza kwetu kumegeuka maombolezo.
16 Taji limeanguka kichwani mwetu; ole wetu, kwa kuwa tumetenda dhambi!
Taji imeanguka kutoka kichwani petu. Ole wetu, kwa maana tumetenda dhambi!
17 Kwa kuwa moyo wetu umekuwa unaumwa, na machozi yetu ya fifia, kwa vitu hivi macho yetu yanafifia
Kwa sababu hiyo, mioyo yetu inazimia, kwa sababu ya hayo, macho yetu yamefifia,
18 maana Mlima Sayuni umelala ukiwa, mbwa wa mitaani wacheza juu yake.
kwa ajili ya Mlima Sayuni, ambao unakaa ukiwa, nao mbweha wanatembea juu yake.
19 Lakini wewe, Yahweh, unatawala milele, na utaketi katika kiti chako cha enzi vizazi na vizazi. Kwanini unatusahau milele?
Wewe, Ee Bwana unatawala milele, kiti chako cha enzi chadumu kizazi hadi kizazi.
20 Kwanini unatutelekeza kwa siku nyingi?
Kwa nini watusahau siku zote? Kwa nini umetuacha kwa muda mrefu?
21 Turejeshe kwako, Yahweh, na sisi tutarejea. Fanya upya siku zetu kama zilivyo kuwa hapo zamani -
Turudishe kwako mwenyewe, Ee Bwana, ili tupate kurudi. Zifanye mpya siku zetu kama siku za kale,
22 vinginevyo labda uwe umetukataa na una hasira kwetu kupita kiasi.
isipokuwa uwe umetukataa kabisa na umetukasirikia pasipo kipimo.