< Maombolezo 4 >
1 Dhahabu imechakaa; jinsi gani dhahabu safi imebadilika! Mawe matakatifu yamezagaa katika kila njia ya mtaa.
2 Wana wa dhamani wa Sayuni walikuwa na dhamani ya uzito wa dhahabu safi, lakini sasa hawana dhamani zaidi ya majagi ya udogo, kazi ya mikono ya mfinyazi!
3 Ata mbwa wa mitaani wanatoa maziwa yao kuwanyonyesha watoto wao, lakini binti wa watu wangu amekuwa katili, kama mbuni katika jangwa.
4 Ulimi wa mtoto mchanga anaye nyonya unagota juu mdomo wake kwa kiu; watoto wanaomba chakula, lakini hakuna kwa ajili yao.
5 Wao walizoea kula chakula cha gharama sasa wana shinda njaa mitaani; wao walio lelewa kwa kuvaa nguo za zambarau, sasa wamelala katika majalala.
6 Hukumu ya binti wa watu wangu ni kubwa kuliko hiyo ya Sodoma, na ilipinduliwa kwa dakika na hakuna aliye yanyua mkono kumsaidia.
7 Viongozi wake walikuwa wasafi kuliko theluji, weupe kuliko maziwa; miili yao ilikuwa imara kuliko jiwe, mwili wao ulikuwa kama yakuti samawi.
8 Muonekano wao umekuwa mweusi kama giza; hawatambuliki mitaani. Ngozi zao zimesinya kwenye mifupa yao; imekuwa kavu kama kuni.
9 Hao walio uawa kwa upanga walikuwa na furaha zaidi kuliko hao walio kufa kwa njaa, walio potea, wakatobolewa kwa ukosefu wa mavuno shambani.
10 Mikono ya wanawake wenye huruma imewachemsha watoto wao; wamekuwa chakula chao wakati ambapo binti wa watu wangu alipo kuwa akiharibiwa.
11 Yahweh alionyesha gadhabu yake yote; alimwaga hasira yake kali. Aliwasha moto Sayuni uliteketeza misingi yake.
12 Wafalme wa dunia hawaku amini, wala wakazi wa dunia, kwamba maadui au wapinzani waliweza kuingia malangoni ya Yerusalemu.
13 Haya yalitokea kwasababu ya dhambi za manabii na na maasi ya makuhani walio mwaga damu ya wenye haki mbele zake.
14 Walitanga, kwa upofu, mitaani. Walikuwa wamejitia unajisi kwa damu hiyo ambapo hakuna aliye ruhusiwa kushika nguo zao.
15 “Kaa mbali! Wewe mnajisi!” Watu waliwapazia sauti. “Kaa mbali! Kaa mbali! Usiguse!” Hivyo wakatanga; watu walisema miongoni mwa mataifa, “Hawawezi kukaa hapa tena.”
16 Yahweh mwenyewe akawatawanyisha; hawatazami tena. Hawa waheshimu makuhani, na hawaonyeshi upendeleo kwa wazee.
17 Macho yetu yalikwama, yakitazama bure kwa msaada; kutoka minara yetu ya ulinzi tulitazama taifa lisilo weza tuokoa.
18 Walifuata hatua zetu, hatukuweza kutembea mitaani mwetu. Mwisho wetu ulikuwa karibu na siku zetu zilihesabiwa, mwisho wetu ulifika.
19 Walio tukimbiza walikuwa wepesi kuliko tai wa aangani. Walitukimbiza kwenye milima na kutuwinda nyikani.
20 Pumzi katika pua zetu - mpakwa mafuta wa Yahweh - ndiye aliye kamatwa katika shimo; ambaye ndiye aliye semewa, “Chini ya kivuli chake tutaishi miongoni mwa mataifa.”
21 Shangilia na ufurahi, binti wa Edomu, wewe unaye ishi nchi ya Uzi. Lakini kwako pia kikombe kitapitishwa; utalewa na kuvua nguo.
22 Binti wa Sayuni, hukumu yako itafika mwisho, hataongeza mateka yako lakini binti wa Edomu, ata muhadhibu; ata funua dhambi zako.