< Maombolezo 2 >
1 Bwana amemfunika binti wa Sayuni chini ya wingu la hasira yake. Ametupa utukufu wa Israeli chini kutoka mbinguni hadi duniani. Hajakumba stuli yake ya miguu siku ya hasira yake.
Tazama jinsi Bwana alivyomfunika Binti Sayuni kwa wingu la hasira yake! Ameitupa chini fahari ya Israeli kutoka mbinguni mpaka duniani, hakukumbuka kiti chake cha kuwekea miguu katika siku ya hasira yake.
2 Bwana amemeza na hajawa na huruma kwa miji yote ya Yakobo. Siku za hasira zake ameangusha miji imara ya binti wa Yuda; kwa aibu ameshusha chini ufalme na watala wake.
Bila huruma Bwana ameyameza makao yote ya Yakobo; katika ghadhabu yake amebomoa ngome za Binti Yuda. Ameuangusha ufalme wake na wakuu wake chini kwa aibu.
3 Kwa hasira kali amekata kila pembe ya Israeli. Ameurudisha mkono wake kutoka kwa adui. Amechoma Yakobo kama moto mkali unao teketeza kila kitu karibu yake.
Katika hasira kali amevunja kila pembe ya Israeli. Ameuondoa mkono wake wa kuume alipokaribia adui. Amemteketeza Yakobo kama moto uwakao ule uteketezao kila kitu kinachouzunguka.
4 Kama adui amepindisha upinde wake kuelekea kwetu, na wakulia wake yupo tayari kushambulia. Amewachinja wote walio kuwa wanampendeza katika hema la binti wa Sayuni; Amemwaga gadhabu yake kama moto
Ameupinda upinde wake kama adui, mkono wake wa kuume uko tayari. Kama vile adui amewachinja wote waliokuwa wanapendeza jicho, amemwaga ghadhabu yake kama moto juu ya hema la Binti Sayuni.
5 Bwana amekuwa kama adui. Amemeza Israeli. Amemeza majumba yake yote. Ameharibu ngome zake. Ameongeza kilio na maombolezo kati ya mabinti wa Yuda.
Bwana ni kama adui; amemmeza Israeli. Amemeza majumba yake yote ya kifalme na kuangamiza ngome zake. Ameongeza huzuni na maombolezo kwa ajili ya Binti Yuda.
6 Ameshambulia hema lake la kukutania kama kajumba cha bustani. Ameharibu sehemu ya kukusanyikia. Yahweh amesababisha kukusanyika na Sabato kusahaulika Sayuni, kwa kuwa amemdharau mfalme na kuhani katika ukali wa hasira yake.
Ameharibu maskani yake kama bustani, ameharibu mahali pake pa mkutano. Bwana amemfanya Sayuni kusahau sikukuu zake zilizoamriwa na Sabato zake; katika hasira yake kali amewadharau mfalme na kuhani.
7 Bwana amekataa madhabahu yake na kukana sehemu yake takatifu. Ametoa kuta za majumba mikononi mwa adui. Wamepaza sauti nyumbani mwa Yahweh, kama siku ya sherehe.
Bwana amekataa madhabahu yake na kuacha mahali patakatifu pake. Amemkabidhi adui kuta za majumba yake ya kifalme; wamepiga kelele katika nyumba ya Bwana kama katika siku ya sikukuu iliyoamriwa.
8 Yahweh aliamua kuharibu ukuta wa mji wa binti wa Sayuni. Amenyoosha kamba ya kipimo na hajauzuia mkono wake kutoharibu ukuta. Amefanya minara na ukuta kuomboleza; pamoja vilipotea.
Bwana alikusudia kuangusha ukuta uliomzunguka Binti Sayuni. Ameinyoosha kamba ya kupimia na hakuuzuia mkono wake usiangamize. Alifanya maboma na kuta ziomboleze, vyote vikaharibika pamoja.
9 Malango yake yameanguka chini, ameharibu na kuvunja chuma za ukuta. Mfalme wake na watoto wa mfalme wapo miongoni mwa mataifa, sheria haipo tena na manabii wake hawapati maono kutoka kwa Yahweh.
Malango yake yamezama ardhini, makomeo yake ameyavunja na kuyaharibu. Mfalme wake na wakuu wake wamepelekwa uhamishoni miongoni mwa mataifa, sheria haipo tena, na manabii wake hawapati tena maono kutoka kwa Bwana.
10 Wazee wa binti wa Sayuni wameketi chini na ukimya. Wamerusha vumbi kichwani mwao na kuvaa magunia. Mabikra wa Yerusalemu wameinamisha vichwa vyao chini.
Wazee wa Binti Sayuni wanaketi chini kimya, wamenyunyiza mavumbi kwenye vichwa vyao na kuvaa nguo za gunia. Wanawali wa Yerusalemu wamesujudu hadi ardhini.
11 Macho yangu yamekaukiwa machozi yake; tumbo langu la nguruma; sehemu zangu za ndani zimemwagika chini kwasababu ya uharibifu wa binti wa watu wangu, watoto na wachanga wamezimia mitaani mwa mji.
Macho yangu yamedhoofika kwa kulia, nina maumivu makali ndani, moyo wangu umemiminwa ardhini kwa sababu watu wangu wameangamizwa, kwa sababu watoto na wanyonyao wanazimia kwenye barabara za mji.
12 Wanasema kwa mama zao, “Mbegu ziko wapi na mvinyo?” kama wanavyo zimia kama mtu aliye jeruhiwa mitaani mwa mji, maisha yao yamemwaga kwenye kifua cha mama zao.
Wanawaambia mama zao, “Wapi mkate na divai?” wazimiapo kama watu waliojeruhiwa katika barabara za mji, maisha yao yadhoofikavyo mikononi mwa mama zao.
13 Nini naeza kusema kwako, binti wa Yerusalemu? Naweza kufananisha na nini, ili ni kufariji, binti bikra wa Sayuni? Jera lako ni kubwa kama bahari. Nani anaweza kukuponya?
Ninaweza kusema nini kwa ajili yako? Nikulinganishe na nini, ee Binti Yerusalemu? Nitakufananisha na nini, ili nipate kukufariji, ee Bikira Binti Sayuni? Jeraha lako lina kina kama bahari. Ni nani awezaye kukuponya?
14 Manabii wako wameona uongo na maono batili kwa ajili yako. Hawaja weka wazi dhambi zako kurejesha mali zako, lakini kwako wametoa matamko ya uongo na ya kupotosha.
Maono ya manabii wako yalikuwa ya uongo na yasiyofaa kitu, hawakuifunua dhambi yako ili kukuzuilia kwenda utumwani. Maneno waliyokupa yalikuwa ya uongo na ya kupotosha.
15 Wote wanao pita pembeni mwa barabara wana piga makofi kwako. Wanaguna na kutikisa vichwa vyao dhidi ya binti wa Yerusalemu na kusema, “Huu ndio mji walio uita 'Ukamilifu wa uzuri,' 'Furaha ya Dunia Yote'?”
Wote wapitiao njia yako wanakupigia makofi, wanakudhihaki na kutikisa vichwa vyao kwa Binti Yerusalemu: “Huu ndio ule mji ulioitwa mkamilifu wa uzuri, furaha ya dunia yote?”
16 Maadui zako wote walifungua vinywa vyao na kukudhihaki. Walizomea na kusaga meno na kusema, “Tumemmeza yeye! Hii ni siku tulio subiri! Tumeishi kuweza kuiona!”
Adui zako wote wanapanua vinywa vyao dhidi yako, wanadhihaki na kusaga meno yao na kusema, “Tumemmeza. Hii ndiyo siku tuliyoingojea, tumeishi na kuiona.”
17 Yahweh amefanya alivyo panga kufanya. Ametimiza neno lake. Amekupindua bila huruma, kwa kuwa amemruhusu adui kukusherehekea; amenyanyua pembe za maadui zako.
Bwana amefanya lile alilolipanga; ametimiza neno lake aliloliamuru siku za kale. Amekuangusha bila huruma, amewaacha adui wakusimange, ametukuza pembe ya adui yako.
18 Mioyo yao ikamlilia Bwana, kuta za binti wa Sayuni! Fanya machozi yako kutiririka chini kama mto usiku na mchana. Usijipatie hauweni, macho yako bila hauweni.
Mioyo ya watu inamlilia Bwana. Ee ukuta wa Binti Sayuni, machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike.
19 Nyanyuka, lia usiku, mwanzo usiku wa manane! Mwaga moyo wako kama maji mbele za uso wa Bwana. Nyoosha juu mikono yako kwa ajili ya uzima wa watoto wako wanao zimia kwa njaa kwenye njia ya kila mtaa.
Inuka, lia usiku, zamu za usiku zianzapo; mimina moyo wako kama maji mbele za Bwana. Mwinulie yeye mikono yako kwa ajili ya maisha ya watoto wako, ambao wanazimia kwa njaa kwenye kila mwanzo wa barabara.
20 Ona, Yahweh, na ukumbuke hao ulio watende haya. Wanawake wale tunda la uzazi wao, watoto walio wajali? Makuhani na manabii wa chinjwe sehemu takatifu ya Bwana?
“Tazama, Ee Bwana, ufikirie: Ni nani ambaye umepata kumtendea namna hii? Je, wanawake wakule wazao wao, watoto waliowalea? Je, kuhani na nabii auawe mahali patakatifu pa Bwana?
21 Wote wadogo kwa wakubwa wana keti kwenye udongo wa mitaa. Wanawake wangu wadogo na wanaume wangu wadogo wameanguaka kwa upanga; umewachinja pasipo kuwa hurumia.
“Vijana na wazee hujilaza pamoja katika mavumbi ya barabarani, wavulana wangu na wasichana wameanguka kwa upanga. Umewaua katika siku ya hasira yako, umewachinja bila huruma.
22 Umeitisha, kama ungewaita watu katika siku ya maakuli, hofu yangu kila sehemu, katika siku ya hasira ya Yahweh hakuna aliye toroka; hao niliyo wajali na kuwakuza, adui wangu amewaharibu.
“Kama ulivyoita siku ya karamu, ndivyo ulivyoagiza hofu kuu dhidi yangu kila upande. Katika siku ya hasira ya Bwana hakuna yeyote aliyekwepa au kupona; wale niliowatunza na kuwalea, adui yangu amewaangamiza.”