< Maombolezo 1 >

1 Mji ambao mwanzo ulikuwa na watu wengi sasa umekaa peke yake. Amekuwa kama mjane, japo alikuwa taifa kubwa. Alikuwa mtoto wa mfalme miongoni mwa mataifa, lakini sasa amelazimishwa utumwani.
ああ哀しいかな古昔は人のみちみちたりし此都邑 いまは凄しき樣にて坐し 寡婦のごとくになれり 嗟もろもろの民の中にて大いなりし者 もろもろの州の中に女王たりし者 いまはかへつて貢をいるる者となりぬ
2 Analia na kuomboleza usiku, na machozi yake yanafunika mashavu yake. Hamna ata mpenzi wake anaye mliwaza. Marafiki wake wote wamemsaliti. wamekuwa maadui wake.
彼よもすがら痛く泣きかなしみて涙面にながる その戀人の中にはこれを慰むる者ひとりだに無く その朋これに背きてその仇となれり
3 Baada ya umaskini na mateso, Yuda ameenda matekani. Anaishi miongoni mwa mataifa na hapati pumziko lolote. Wanao wakimbiza wamewapata katika upweke wake.
ユダは艱難の故によりまた大いなる苦役のゆゑによりて擄はれゆき もろもろの國に住ひて安息を得ず これを追ふものみな狭隘にてこれに追しきぬ
4 Barabara za Sayuni zinaomboleza kwasababu hakuna anaye kuja kwenye sherehe iliyo andaliwa. Malango yake yote ni ukiwa. Makuhani wake wote wana sononeka. Mabikra wake wana uzuni na yeye mwenyewe yupo katika ugumu.
シオンの道路は節會の上り來る者なきがために哀しみ その門はことごとく荒れ その祭司は歎き その處女は憂へ シオンもまた自から苦しむ
5 Maadui wake wamekuwa bwana zake; maadui wake wana fanikiwa. Yahweh amemuadhibu kwa dhambi zake nyingi. Watoto wake wadogo wanaenda matekani kwa maadui zake.
その仇は首となり その敵は享ゆ その愆の多きによりてヱホバこれをなやませたまへるなり そのわかき子等は擄はれて仇の前にゆけり
6 Uzuri umemwacha binti wa Sayuni. Watoto wa mfalme wamekuwa kama ayala ambaye haoni malisho, na wanaenda bila uwezo kwa wanao wakimbiza.
シオンの女よりはその榮華ことごとく離れされり またその牧伯等は草を得ざる鹿のごとくに成り おのれを追ふものの前に力つかれて歩みゆけり
7 Katika siku za mateso yake na kutokuwa na nyumba, Yerusalemu itakumbuka hazina zake za dhamani alizo kuwa nazo awali. Wakati watu wake walipo angukia mikononi mwa adui, hakuna aliye msaidia. Maadui waliwaona na kucheka maangamizo yake.
ヱルサレムはその艱難と窘迫の時むかしの代にありしもろもろの樂しき物を思ひ出づ その民仇の手におちいり誰もこれを助くるものなき時 仇人これを見てその荒はてたるを笑ふ
8 Yerusalemu ili tenda dhambi sana, hivyo basi, amedhalillika kama kitu kichafu. Wote walio mheshimu sasa wana mdharau kwa kuwa wameona uchi wake. Anasononeka na kujaribu kugeuka pembeni.
ヱルサレムははなはだしく罪ををかしたれば汚穢たる者のごとくになれり 前にこれを尊とびたる者もその裸體を見しによりて皆これをいやしむ 是もまたみづから嗟き身をそむけて退ぞけり
9 Amekuwa mchafu chini ya sketi yake. Hakuwaza hatima yake. Anguko lake lilikuwa baya. Hakukuwa na wakumliwaza. Alilia, “Angalia mateso yangu, Yahweh, kwa kuwa adui amekuwa mkuu sana.”
その汚穢これが裾にあり 彼その終局をおもはざりき 此故に驚ろくまでに零落たり 一人の慰さむる者だに無し ヱホバよわが艱難をかへりみたまへ 敵は勝ほこれり
10 Adui ameeka mkono wake kwenye hazina zetu za dhamani. Ameona mataifa yakiingia sehemu yake takatifu, japo uliamuru wasiingie katika sehemu yako ya kukusanyikia.
敵すでに手を伸てその財寳をことごとく奪ひたり 汝さきに異邦人等はなんぢの公會にいるべからずと命じおきたまひしに 彼らが聖所を侵しいるをシオンは見たり
11 Watu wote wana sononeka wanapo tafuta mkate. Wametoa hazina zao za dhamani kwa ajili ya chakula cha kurejesha uhai wao. Tazama, Yahweh, ni kumbuke mimi, kwa kuwa nimekuwa sina faida.
その民はみな哀きて食物をもとめ その生命を支へんがために財寳を出して食にかへたり ヱホバよ見そなはし我のいやしめらるるを顧りみたまへ
12 Sio kitu kwako, wote mnao pita? Angalia na uone kama kuna mtu mwenye uzuni kama uzuni ninao teswa nao, tangu Yahweh amenitesa mimi katika siku ya hasira yake kali.
すべて行路人よ なんぢら何ともおもはざるか ヱホバその烈しき震怒の日に我をなやましてわれに降したまへるこの憂苦にひとしき憂苦また世にあるべきや考がへ見よ
13 Ni kutoka juu ndipo alipo tuma moto kwenye mifupa yangu na umenishinda. Ametanda nyavu kwa miguu yangu na kunigeuza. Amenifanya ukiwa na dhahifu.
ヱホバ上より火をくだしわが骨にいれて之を克服せしめ 網を張りわが足をとらへて我を後にむかしめ 我をして終日心さびしくかつ疾わづらはしめたまふ
14 Nira ya makosa yangu imefungwa na mikono yake. Zimesokotwa na kuekwa shingoni mwangu. Amefanya uweza wangu kushindwa. Bwana amenikabidhi mikononi mwa, na siwezi kusimama.
わが愆尤の軛は主の御手にて結ばれ諸の愆あひ纒はりてわが項にのれり 是はわが力をしておとろへしむ 主われを敵たりがたき者の手にわたしたまへり
15 Bwana ametupa pembeni wanaume wangu hodari walio niokoa. Ameitisha kusanyiko dhidi yangu kuponda wanaume wangu imara. Bwana amewakanyaga binti bikra wa Yuda kwenye chombo cha kusagia mvinyo.
主われの中なる勇士をことごとく除き 節會をもよほして我を攻め わが少き人を打ほろぼしたまへり 主酒榨をふむがごとくにユダの處女をふみたまへり
16 Kwa vitu hivi ninalia. Macho yangu, maji yanashuka chini ya macho yangu tangu mfariji aliye paswa kurejesha maisha yangu yuko mbali na mimi. Watoto wangu wamekuwa ukiwa kwasababu adui yangu ameshinda.
これがために我なげく わが目やわが目には水ながる わがたましひを活すべき慰さむるものわれに遠ければなり わが子等は敵の勝るによりて滅びうせにき
17 Sayuni ametandaza mikono yake; hakuna wakuwa mliwaza. Yahweh ameamuru hao karibu na Yakobo wawemaadui wake. Yerusalemu ni kitu kichafu kwao.
シオンは手をのぶれども誰もこれを慰さむる者なし ヤコブにつきてはヱホバ命をくだしてその周圍の民をこれが敵とならしめたまふ ヱルサレムは彼らの中にありて汚れたる者のごとくなりぬ
18 Yahweh ni mwenye haki, kwa kuwa nimeasi dhidi ya amri zake. Sikia, ninyi watu, na muone uzuni wangu. Mabikra wangu na wanaume imara wameenda matekani.
ヱホバは正し 我その命令にそむきたるなり 一切の民よわれに聽け わが憂苦をかへりみよ わが處女もわかき男も俘囚て往り
19 Niliita marafiki zangu, lakini walikuwa na hila kwangu. Makuhani wangu na wazee waliangamia kwenye mji, walipo kuwa wanatafuta chakula cha kurejesha uhai wao.
われわが戀人を呼たれども彼らはわれを欺むけり わが祭司およびわが長老は生命を繋がんとて食物を求むる間に都邑の中にて氣息たえたり
20 Tazama, Yahweh, kwa kuwa nipo kwenye ugumu; tumbo langu lina nguruma, moyo wangu umetibuka ndani yangu, kwa kuwa nimekuwa muasi sana. Nje, upanga umemliza mama, ndani ya nyumba kuna mauti tu.
ヱホバよかへりみたまへ 我はなやみてをり わが膓わきかへり わが心わが衷に顛倒す 我甚しく悖りたればなり 外には劍ありてわが子を殺し 内には死のごとき者あり
21 Wamesikia sononeko langu, lakini hakuna wakuni liwaza. Maadui zangu wote wamesikia shida zangu na wamefurahi umenifanyia hivi. Umeleta siku uliyo ahidi; sasa acha wawe kama mimi.
かれらはわが嗟歎をきけり 我をなぐさむるもの一人だに无し わが敵みなわが艱難をききおよび 汝のこれを爲たまひしを喜こべり 汝はさきに告しらせしその日を來らせたまはん 而して彼らもつひに我ごとくに成るべし
22 Acha uovu wote uje mbele zako. Shughulika nao kama ulivyo shughulika na mimi kwasababu ya makosa yangu yote. Masononeko yangu ni mengi na moyo umezimia.
ねがはくは彼等が與へし艱難をことごとくなんぢの御前にあらはし 前にわがもろもろの罪愆のために我におこなひし如く彼らにも行ひたまへ わが嗟歎は多くわが心はうれひかなしむなり

< Maombolezo 1 >