< Yuda 1 >
1 Yuda, mtumwa wa Yesu Kristo, na ndugu yake Yakobo, kwa wale ambao wameitwa, wapendwao katika Mungu Baba, na waliotunzwa kwa ajili ya Yesu Kristo:
Jude, a servant of Jesus Christ, and brother of James, to those who are sanctified in God the Father, and preserved in Jesus Christ, and called:
2 rehema na amani na upendo viongezwe kwenu.
mercy be to you, and peace and love be multiplied.
3 Wapenzi, wakati nilipokuwa nikifanya kila juhudi kuwaandikia ninyi kuhusu wokovu wetu sote, ilinilazimu kuwaandikia kwa ajili ya kuwashauri ili mshindanie kwa uaminifu imani ambayo ilikuwa imekabidhiwa mara moja tu kwa waamini.
Beloved, using all diligence to write to you of the common salvation, I thought it necessary to write to you, and exhort you to contend earnestly for the faith once delivered to the saints.
4 Kwa sababu watu fulani wamejiingiza kwa siri kati yenu - watu ambao walitiwa alama kwa ajili ya hukumu - watu wasio wataua ambao hubadili neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, na kumkana Bwana wetu pekee na Bwana Yesu Kristo.
For some men have stealthily entered in, who were long ago appointed to this condemnation; ungodly men, who pervert the grace of our God, and use it for lascivious purposes, and deny our only Sovereign and Lord, Jesus Christ.
5 Sasa napenda kuwakumbusha ninyi ingawa kuna wakati mlijua kwa ukamilifu kwamba Bwana aliwaokoa watu kutoka nchi ya Misri, lakini baadaye kuwaangamiza wale ambao hawakuamini.
But I wish to remind you, though you once knew this, that the Lord, having saved the people from the land of Egypt, then destroyed those who believed not.
6 Na malaika ambao hawakuilinda enzi yao wenyewe lakini wakaacha makao yao maalum Mungu amewaweka katika minyororo ya milele, ndani ya giza, kwa ajili ya hukumu ya siku ile kuu. (aïdios )
The angels also that kept not their own dominion, but left their proper habitation, he has reserved, in eternal chains under darkness, to the judgment of the great day. (aïdios )
7 Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyoizunguka, ambayo pia ilijiingiza yenyewe katika uasherati na wakafuata tamaa isiyo ya asili. Walioneshwa kama mifano ya wale ambao huteseka katika hukumu ya moto wa milele. (aiōnios )
So Sodom and Gomorrah, and the cities which were about them, in like manner giving themselves over to lewdness, and following after other flesh, are set forth as an example, suffering the punishment of eternal fire. (aiōnios )
8 Hali kadhalika, kwa njia ile ile waota ndoto hawa pia huchafua miili yao, na hukataa mamlaka, na wananena uongo dhidi ya mtukufu.
Yet, these dreamers also in like manner defile the flesh, despise government, and speak evil of dignitaries.
9 Lakini hata Mikaeli malaika mkuu, wakati alipokuwa akishindana na ibilisi na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kuleta hukumu ya uongo dhidi yake, lakini badala yake alisema, “Bwana akukemee!”
But Michael the archangel, when, contending with the devil, he disputed about the body of Moses, durst not bring a railing accusation, but said: The Lord rebuke you.
10 Lakini watu hawa huleta uongo dhidi ya chochote wasicho kifahamu. Na kile wasicho kifahamu- kile ambacho wanyama wasio na akili hujua kwa silika- haya ndiyo yaliyo waharibu.
But these speak evil of the things which they know not: and those things which they know naturally, as animals without reason, in these they corrupt themselves.
11 Ole wao! Kwa kuwa wametembea katika njia ya Kaini, na kulifuata kosa la Balaamu. Wameangamia katika uasi wa Kora.
Alas for them! for they have gone in the way of Cain: and, in the error of Balaam, they have rushed headlong after reward, and have perished in the rebellion of Korah.
12 Hawa ni miamba katika sherehe zenu za upendo, wakisherehekea bila aibu, wakijilisha tu wenyewe. Ni mawingu yasiyo na maji, yanayobebwa na upepo, ni miti iliyopukutika isiyo na matunda iliyo kufa mara mbili, iliyong'olewa mizizi
These, while feasting with you, are spots in your lovefeasts, feeding themselves without fear; they are clouds without water, driven along by winds; trees of autumn, without fruit, twice dead, torn up by the roots:
13 Ni mawimbi ya bahari yenye kelele yakitoa aibu yao wenyewe, Ni nyota zinazorandaranda ambazo weusi wa giza umetunzwa kwa ajili yao milele. (aiōn )
raging waves of the sea, foaming up their own shame: wandering stars, for whom the blackness of darkness is reserved forever. (aiōn )
14 Enoko, wa saba katika orodha ya Adamu, alitabiri kuhusu wao, akisema, “Tazama! Bwana anakuja na maelfu kwa maelfu ya watakatifu wake,
And Enoch, the seventh from Adam, also prophesied with reference to these men, saying: Behold, the Lord comes with his holy myriads,
15 ili afanye hukumu juu ya kila mtu, na kutia hatia wote wasiomcha Mungu juu ya matendo yao yote waliyokwishafanya katika njia zisizo za kitauwa, na kwa maneno yote ya ukali ambayo wasio watauwa wameyanena dhidi yake.”
to execute judgment upon all, and to convict all the ungodly of all their ungodly works, which they have impiously committed, and of all the hard words which ungodly sinners have spoken against him.
16 Hawa ni wale wanung'unikao, walalamikao ambao hufuata tamaa zao za uovu, wajivunao mno, ambao kwa faida yao hudanganya wengine.
These are murmurers, fault-finders, walking according to their own desires; and their mouth speaks boastful words, while they admire persons for the sake of gain.
17 Lakini ninyi, wapenzi, kumbukeni maneno ambayo yalinenwa zamani na mitume wa Bwana Yesu Kristo.
But do you, beloved, remember the words that were formerly spoken by the apostles of our Lord Jesus Christ;
18 Walisema kwenu, “Katika wakati wa mwisho kutakuwa na watu wanaodhihaki ambao hufuata tamaa zao zisizo za kitauwa.”
that they said to you, There should come, in the last days, scoffers walking according to their own ungodly desires.
19 Watu hawa ni watenganishaji, wanatawaliwa na tamaa za asili, na hawana Roho.
These are they who separate themselves, animal, not having the Spirit.
20 Lakini ninyi, wapenzi, kama mjijengavyo katika imani yenu takatifu sana, na kama muombavyo katika Roho Mtakatifu,
But you, beloved, building yourselves up on your most holy faith, praying in the Holy Spirit,
21 jitunzeni katika upendo wa Mungu, na msubiri rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo ambayo huwapatia uzima wa milele. (aiōnios )
keep yourselves in the love of God, looking for the mercy of our Lord Jesus Christ, in order to eternal life. (aiōnios )
22 Onesheni rehema kwa wale walio na shaka.
And on some, have compassion, making a distinction:
23 Waokoeni wengine kwa kuwanyakua kutoka katika moto. Kwa wengine onesheni huruma kwa hofu, mkichukia hata vazi lililotiwa doa na mwili.
and others, save by fear, snatching them from the fire, hating even the garment spotted by the flesh.
24 Sasa kwake awezaye kuwalinda msijikwae, na kuwasababisha msimame mbele ya utukufu wake, bila mawaa na kuwa na furaha kuu,
Now to him that is able to keep you free from stumbling, and to present you blameless in the presence of his glory with exceeding joy,
25 kwake Mungu pekee mwokozi kupitia Yesu Kristo Bwana wetu, utukufu uwe kwake, ukuu, uwezo na nguvu kabla ya nyakati zote, na sasa na hata milele. Amina. (aiōn )
to the only God our Savior, be glory and majesty, strength and authority, both now and throughout all the ages. Amen. (aiōn )