< Yoshua 4 >
1 Watu wote walipokwisha kuvuka Yordani, Yahweh akamwambia Yoshua,
国民尽都过了约旦河,耶和华就对约书亚说:
2 “Chagueni wenyewe watu waume kumi na wawili, mmoja katika kila kabila.
“你从民中要拣选十二个人,每支派一人,
3 Wape agizo hilo: 'Chukueni mawe kumi na mbili kutoka katikati ya Yordani mahali wanaposimama makuhani katika nchi kavu, na wayalete na kuyaweka chini katika sehemu ambapo mtalala usiku wa leo.
吩咐他们说:‘你们从这里,从约旦河中、祭司脚站定的地方,取十二块石头带过去,放在你们今夜要住宿的地方。’”
4 Kisha Yoshua akawaita wanaume kumi na wawili ambao aliwachagua kutoka katika makabila ya Israeli, mmoja kutoka kila kabila.
于是,约书亚将他从以色列人中所预备的那十二个人,每支派一人,都召了来。
5 Yoshua akawaambia, “Nendeni mbele za sanduku la Yahweh Mungu wenu katikati ya Yordani. Kila mmoja wenu achukue jiwe moja mabegani mwake, kulingana na hesabu ya makabila ya watu wa Israeli.
对他们说:“你们下约旦河中,过到耶和华—你们 神的约柜前头,按着以色列人十二支派的数目,每人取一块石头扛在肩上。
6 Hii itakuwa ni ishara miongoni mwenu kwa ajili yenu wakati watoto wenu watakapowauliza katika siku zijazo, 'Nini maana ya mawe haya kwenu?'
这些石头在你们中间可以作为证据。日后,你们的子孙问你们说:‘这些石头是什么意思?’
7 Ndipo mtakapowaambia, 'Maji ya Yordani yalitengwa mbele ya sanduku la Yahweh. Lililpopitishwa katika Yordani, maji ya Yordani yalisimamishwa. Hivyo, mawe haya yatakuwa kumbukumbu kwa watu wa Israeli milele.'”
你们就对他们说:‘这是因为约旦河的水在耶和华的约柜前断绝;约柜过约旦河的时候,约旦河的水就断绝了。这些石头要作以色列人永远的纪念。’”
8 Watu waisraeli walifanya kama Yoshua alivyowaagiza, na walichukua mawe kumi na mbili kutoka katikati ya Yordani, kama Yahweh alivyomwambia Yoshua, walipangwa sawa sawa na hesabu ya makabila ya watu wa Israeli. Waliyachukua mawe mpaka mahali walipolala na wakayaweka chini huko.
以色列人就照约书亚所吩咐的,按着以色列人支派的数目,从约旦河中取了十二块石头,都遵耶和华所吩咐约书亚的行了。他们把石头带过去,到他们所住宿的地方,就放在那里。
9 Kisha Yoshua akayapanga mawe kumi na mbili katikati ya Yordani, katika sehemu ambapo ilisimama miguu ya makuhani waliolichukua sanduku la agano. Na kumbukumbu hiyo ipo hadi leo.
约书亚另把十二块石头立在约旦河中,在抬约柜的祭司脚站立的地方;直到今日,那石头还在那里。
10 Makuhani waliolichukua sanduku walisimama katikati ya Yordani mpaka pale kila kitu ambacho Yahweh alimwamuru Yoshua kuwaambia watu kilipokamilika, sawa sawa na yote ambayo Musa alimwagiza Yoshua. Watu walifanya haraka na wakavuka.
抬约柜的祭司站在约旦河中,等到耶和华晓谕约书亚吩咐百姓的事办完了,是照摩西所吩咐约书亚的一切话。于是百姓急速过去了。
11 Wakati watu wote walipokwisha kuvuka, sanduku la Yahweh pamoja na makuhani walivuka mbele za watu.
众百姓尽都过了河,耶和华的约柜和祭司就在百姓面前过去。
12 Kabila la Rubeni, kabila la Gadi, na nusu ya kabila la Manase walipita kama jeshi mbele ya watu wa Israeli, kama ambavyo Musa alivyowaambia.
吕便人、迦得人、玛拿西半支派的人都照摩西所吩咐他们的,带着兵器在以色列人前头过去。
13 Yapata watu watu elfu arobaini walioandaliwa kwa vita walipita mbele za Yahweh, kwa ajili ya vita katika uwanda wa Yeriko.
约有四万人都准备打仗,在耶和华面前过去,到耶利哥的平原,等候上阵。
14 Katika siku hiyo Yahweh alimfanya Yoshua kuwa mkuu katika macho ya watu wote wa Israeli. Walimheshimu - kama walivyomheshimu Musa - siku zake zote.
当那日,耶和华使约书亚在以色列众人眼前尊大。在他平生的日子,百姓敬畏他,像从前敬畏摩西一样。
15 Kisha Yahweh akamwambia Yoshua,
耶和华晓谕约书亚说:
16 “Waamuru makuhani wanaolibeba sanduku la ushuhuda watoke katika Yordani.”
“你吩咐抬法柜的祭司从约旦河里上来。”
17 Hivyo Yoshua akawaamuru makuhani, '' pandeni mtoke Yordani.”
约书亚就吩咐祭司说:“你们从约旦河里上来。”
18 Wakati makuhani wenye kulibeba sanduku la agano la Yahweh walitoka katikati ya Yordani, na nyayo za miguu yao ilikuwa imeinuliwa katika nchi kavu, kisha maji ya Yordani yalirudi katika sehemu zake na kujaa hadi katika kingo zake kama ilivyokuwa siku nne zilizopita.
抬耶和华约柜的祭司从约旦河里上来,脚掌刚落旱地,约旦河的水就流到原处,仍旧涨过两岸。
19 Katika siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, watu walikwea kutoka Yordani. Wakakaa huko Gilgali, mashariki mwa Yeriko.
正月初十日,百姓从约旦河里上来,就在吉甲,在耶利哥的东边安营。
20 Mawe kumi na mawili ambayo yalichukuliwa katika Yordani, Yoshuua aliyasimamisha hapo Gilgali.
他们从约旦河中取来的那十二块石头,约书亚就立在吉甲,
21 Aliwaambia watu wa Israeli, “wakati watoto wenu watakapowauliza baba zao katika wakai ujao, 'Mawe haya ni ya nini?'
对以色列人说:“日后你们的子孙问他们的父亲说:‘这些石头是什么意思?’
22 Waambieni watoto wenu, 'Hapa ndipo Waisraeli walivuka Yordani katika nchi kavu.
你们就告诉他们说:‘以色列人曾走干地过这约旦河;
23 Yahweh Mungu wenu aliyakausha maji ya Yordani, mpaka hapo Yahweh Mungu wako aliyoyafanya katika bahari ya mianzi, ambayo aliikausha kwa ajili yetu ili tupite juu yakes,
因为耶和华—你们的 神在你们前面使约旦河的水干了,等着你们过来,就如耶和华—你们的 神从前在我们前面使红海干了,等着我们过来一样,
24 ili kwamba watu wote wa nchi wajue kwamba mkono wa Yahweh ni nguvu, na kwamba mtamweshimu Yahweh Mungu wenu milele.''
要使地上万民都知道,耶和华的手大有能力,也要使你们永远敬畏耶和华—你们的 神。’”