< Yoshua 22 >

1 Kwa wakati huo, Yoshua aliwaita Warubeni, Wagadi, na nusu ya kabila la Manase.
אז יקרא יהושע לראובני ולגדי ולחצי מטה מנשה
2 Aliwaambia, “Mmefanya kila kitu ambacho Musa mtumishi wa Yahweh aliwaagiza ninyi. Mmeitii sauti yangu katika yote niliyowaagiza.
ויאמר אליהם--אתם שמרתם את כל אשר צוה אתכם משה עבד יהוה ותשמעו בקולי לכל אשר צויתי אתכם
3 Bado hamjawaacha ndugu zenu hawa kwa siku zote hizi, mpaka siku hii ya leo. Na mmetimiza wajibu unaotakiwa na amri za Yahweh Mungu wenu.
לא עזבתם את אחיכם זה ימים רבים עד היום הזה ושמרתם--את משמרת מצות יהוה אלהיכם
4 Sasa Yahweh Mungu wenu amewapa pumziko ndugu zenu, kama alivyowaahidi. Hivyo basi, rudini na mwende katika hema zenu katika nchi mnayoimiliki, ambayo Musa mtumishi wa Yahweh aliwapeni katika upande mwingine wa Yordani.
ועתה הניח יהוה אלהיכם לאחיכם כאשר דבר להם ועתה פנו ולכו לכם לאהליכם אל ארץ אחזתכם אשר נתן לכם משה עבד יהוה בעבר הירדן
5 Lakini zingatieni kuzishika amri na sheria ambazo Musa mtumishi wa Yahweh aliwaagiza ninyi, kumpenda Yahweh Mungu wenu, kutembea katika njia zake, kuzitunza amri zake, na kuambatana naye na kumwabudu yeye kwa moyo wenu wote na kwa roho zenu zote.
רק שמרו מאד לעשות את המצוה ואת התורה אשר צוה אתכם משה עבד יהוה לאהבה את יהוה אלהיכם וללכת בכל דרכיו ולשמר מצותיו ולדבקה בו ולעבדו בכל לבבכם ובכל נפשכם
6 Basi Yoshua akawabariki na kisha akawaacha waende zao, nao wakarudi katika hema zao.
ויברכם יהושע וישלחם וילכו אל אהליהם
7 Na kwa nusu ya kabila la Manase, Musa alikuwa amewapa urithi katika Bashani, lakini kwa nusu ya kabila hilo, Yoshua aliwapa urithi karibu na ndugu zao katika nchi magharibi mwa Yordani. Yoshua aliwaaga waende katika hema zao; aliwabarikia,
ולחצי שבט המנשה נתן משה בבשן ולחציו נתן יהושע עם אחיהם מעבר (בעבר) הירדן ימה וגם כי שלחם יהושע אל אהליהם--ויברכם
8 na kisha akawaambia, “Rudini katika hema zenu mkiwa na pesa nyingi, na mkiwa na mifugo mingi, pamoja na na fedha, na dhahabu, na shaba na chuma, na nguo nyingi. Gawaneni na ndugu zenu nyara mlizochukua kutoka kwa maadui zenu.
ויאמר אליהם לאמר בנכסים רבים שובו אל אהליכם ובמקנה רב מאד בכסף ובזהב ובנחשת ובברזל ובשלמות הרבה מאד חלקו שלל איביכם עם אחיכם
9 Hivyo, wazawa wa Rubeni, wazawa wa Gadi na nusu ya kabila la Manase walirudi nyumbani, waliwaacha watu wa Isaeli hapo Shilo, ambayo imo ndani ya nchi ya Kanaani. Waliondoka wakaenda katika mkoa wa Gileadi, katika nchi yao, ambayo wao wenyewe waliimiliki, katika utiifu wa amri za Yahweh, kwa mkono wa Musa.
וישבו וילכו בני ראובן ובני גד וחצי שבט המנשה מאת בני ישראל משלה אשר בארץ כנען--ללכת אל ארץ הגלעד אל ארץ אחזתם אשר נאחזו בה על פי יהוה ביד משה
10 Nao walipofika hapo Yordani iliyo katika nchi ya Kanaani, Warubeni na Wagadi na nusu ya kabila la Manase walijenga madhabahu karibu na Yordani, madhabahu kubwa na iliyotokeza na mashuhuri.
ויבאו אל גלילות הירדן אשר בארץ כנען ויבנו בני ראובן ובני גד וחצי שבט המנשה שם מזבח על הירדן--מזבח גדול למראה
11 Watu wa Israeli walisikia habari hizo na wakaseam, “Tazama! Watu wa Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase wamejenga madhabahu mbele ya nchi ya Kanaani, huko Gelilothi, katika mkoa karibu na Yordani, katika upande ambao ni miliki ya watu wa Israeli.”
וישמעו בני ישראל לאמר הנה בנו בני ראובן ובני גד וחצי שבט המנשה את המזבח אל מול ארץ כנען--אל גלילות הירדן אל עבר בני ישראל
12 Wakati watu wa Israeli waliposikia hivyo, kusanyiko lote la watu wa Israeli walikusanyika kwa pamoja huko Shilo ili wapande kupigana vita nao.
וישמעו בני ישראל ויקהלו כל עדת בני ישראל שלה לעלות עליהם לצבא
13 Kisha watu wa Israeli walituma wajumbe kwa Warubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, katika nchi ya Gileadi. Walimtuma pia Finehasi mwana wa Eliezari, kuhani,
וישלחו בני ישראל אל בני ראובן ואל בני גד ואל חצי שבט מנשה--אל ארץ הגלעד את פינחס בן אלעזר הכהן
14 na viongozi kumi pamoja naye, mmoja kutoka katika familia za mababa wa Israeli, na kila mmoja wao alikuwa ni kiongozi wa ukoo miongoni mwa watu wa Israeli.
ועשרה נשאים עמו--נשיא אחד נשיא אחד לבית אב לכל מטות ישראל ואיש ראש בית אבותם המה לאלפי ישראל
15 Walienda kwa watu wa Rubeni, Gadi, na nusu ya kabila la Manase, katika nchi ya Gileadi, na wakawaambia:
ויבאו אל בני ראובן ואל בני גד ואל חצי שבט מנשה--אל ארץ הגלעד וידברו אתם לאמר
16 “Kusanyiko lote la Yahweh linasema kuwa, ' Ni jambo gani hili lisilo la uaminifu ambalo mmelitenda kinyume na Mungu wa Israeli, kwa kugeuka badala ya kumfuata Yahweh siku hii na kujijengea wenyewe madhabahu katika uasi kinyume na Yahweh katika siku hii?
כה אמרו כל עדת יהוה מה המעל הזה אשר מעלתם באלהי ישראל לשוב היום מאחרי יהוה--בבנותכם לכם מזבח למרדכם היום ביהוה
17 Je dhambi zetu huko Peori hazikututosha? Bado hata sasa hatujajitakasa wenyewe kwa dhambi hiyo. Kwa ajili ya dhambi ile lilikuja pigo kwa kusanyiko lote la Yahweh.
המעט לנו את עון פעור אשר לא הטהרנו ממנו עד היום הזה ויהי הנגף בעדת יהוה
18 Je, nanyi leo pia mwageuka na kuacha kumfuata Yahweh? Kama mtaasi kinyume na Yahweh leo, kesho atakuwa na hasira na kusanyiko lote la Israeli.
ואתם תשבו היום מאחרי יהוה והיה אתם תמרדו היום ביהוה ומחר אל כל עדת ישראל יקצף
19 Na kama nchi ambayo mnaimiliki imetiwa unajisi, basi mwaweza kuvuka katika nchi ambayo Sanduku la Yahweh lasimama na mjichukulie kwa ajili yenu umiliki miongoni mwetu. Hamtakiwi kuasi kinyume na Yahweh tu, wala kuasi kinyume chetu kwa kujenga madhabahu kwa ajili yenu wenyewe badala ya madhabahu ya Yahweh Mungu wa wetu.
ואך אם טמאה ארץ אחזתכם עברו לכם אל ארץ אחזת יהוה אשר שכן שם משכן יהוה והאחזו בתוכנו וביהוה אל תמרדו ואתנו אל תמרדו בבנתכם לכם מזבח מבלעדי מזבח יהוה אלהינו
20 Je hakuwa Akani mwana wa Zera aliyeivunja imani kwa vitu vile ambavyo vilikuwa vimetunzwa kwa ajili ya Mungu? Na je ghadhabu ya Mungu haikushuka kwa watu wote wa Israeli? Mtu yule hakuangamia peke yake kwa uovu wake.
הלוא עכן בן זרח מעל מעל בחרם ועל כל עדת ישראל היה קצף והוא איש אחד לא גוע בעונו
21 Kisha makabila ya Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase wakawajibu wazee wa koo za Israeli:
ויענו בני ראובן ובני גד וחצי שבט המנשה וידברו את ראשי אלפי ישראל
22 “Yahweh, Mungu Mwenye nguvu! Yahweh, Mungu Mwenye nguvu! Yeye anajua, na Israeli naijue yenyewe! Kama ilikuwa ni katika uasi au katika kuvunja imani kinyume na Yahweh, msituache hai katika siku hii ya leo
אל אלהים יהוה אל אלהים יהוה הוא ידע וישראל הוא ידע אם במרד ואם במעל ביהוה אל תושיענו היום הזה
23 kwa ajili ya kujenga madhabahu ili tugeuka na kuacha kumfuata Yahweh. Kama tumejenga madhabahu hii ili kutoa juu yake sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya nafaka, au sadaka ya amani, basi Yahweh na atuadhibu.
לבנות לנו מזבח לשוב מאחרי יהוה ואם להעלות עליו עולה ומנחה ואם לעשות עליו זבחי שלמים--יהוה הוא יבקש
24 La hasha, tulifanya hivyo kwa sababu ya hofu kwamba katika siku zijazo watoto wenu wanaweza kuwaambia watoto wetu, ' Mna nini ninyi na Yahweh, Mungu wa Israeli?
ואם לא מדאגה מדבר עשינו את זאת לאמר מחר יאמרו בניכם לבנינו לאמר מה לכם וליהוה אלהי ישראל
25 Kwa kuwa Yahweh ameifanya Yordani kuwa mpaka kati yetu na ninyi. Ninyi watu wa Rubeni na watu wa Gadi, hamna kitu chochote naYahweh.' Na kwa hali hiyo, watoto wenu wanaweza kuwafanya watoto wetu waacha kumwabudu Yahweh.
וגבול נתן יהוה ביננו וביניכם בני ראובן ובני גד את הירדן--אין לכם חלק ביהוה והשביתו בניכם את בנינו לבלתי ירא את יהוה
26 Basi tukasema, 'Hebu na tujenge sasa madhabahu, si kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa wala si kwa sadaka yoyote ile,
ונאמר--נעשה נא לנו לבנות את המזבח לא לעולה ולא לזבח
27 ila iwe ni ushahidi kati yetu na ninyi, na kati ya kizazi chetu baada yetu, kwamba tutafanya ibada ya Yahweh mbele yake, pamoja na sadaka zetu za kuteketezwa na dhabihu zetu na sadaka zetu za amani, ili kwamba watoto wenu wasiweze kuwaambia watoto wetu katika siku zijazo kuwa, “Hamna sehemu katika Yahweh.”'
כי עד הוא בינינו וביניכם ובין דרותינו אחרינו לעבד את עבדת יהוה לפניו בעלותינו ובזבחינו ובשלמינו ולא יאמרו בניכם מחר לבנינו אין לכם חלק ביהוה
28 Hivyo tukasema, 'kama hili litasemwa kwa kwetu au kwa watoto wetu katika siku zijazo, tutasema, “Tazama! Huu ni mfano wa madhabahu ya Yahweh, ambayo mababu zetu waliifanya, si kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, wala si kwa dhabihu, bali kwa ajili ya ushahidi kati yetu ninyi.”
ונאמר--והיה כי יאמרו אלינו ואל דרתינו מחר ואמרנו ראו את תבנית מזבח יהוה אשר עשו אבותינו לא לעולה ולא לזבח--כי עד הוא בינינו וביניכם
29 Na iwe mbali nasi kwamba tunataka kugeuka kinyume na Yahweh, na kuacha kumfuata yeye kwa kujenga madhabahu kwa ajili sadaka ya kuteketezwa, na kwa sadaka ya nafaka, au kwa dhabihu, badala ya madhabahu ya Yahweh Mungu wetu ambayo iko mbele ya hema la kukutania.'”
חלילה לנו ממנו למרד ביהוה ולשוב היום מאחרי יהוה לבנות מזבח לעלה למנחה ולזבח--מלבד מזבח יהוה אלהינו אשר לפני משכנו
30 Finehasi kuhani na viongozi wa watu, ambao ni wakuu wa koo za Waisraeli ambao walikuwa pamoja naye, waliposikia maneno amabayo watu wa Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase, kwamba yalikuwa ni mazuri machoni pao.
וישמע פינחס הכהן ונשיאי העדה וראשי אלפי ישראל אשר אתו את הדברים אשר דברו בני ראובן ובני גד ובני מנשה וייטב בעיניהם
31 Finehasi mwana wa Eliazeri kuhani aliwaambia watu wa Rubeni, Gadi na Manase, “Leo tumejua kwambaYahweh yuko miongoni mwetu, kwa kuwa hamjatenda uvunjaji wa imani kinyume naye. Sasa, mmewaokoa watu wa Israeli kutoka katika mkono wa Yahweh.”
ויאמר פינחס בן אלעזר הכהן אל בני ראובן ואל בני גד ואל בני מנשה היום ידענו כי בתוכנו יהוה אשר לא מעלתם ביהוה המעל הזה אז הצלתם את בני ישראל--מיד יהוה
32 Kisha Finehasi mwana wa Eliazeri kuhani, na viongozi walirudi kutoka kwa Warubeni na Wagadi, kutoka katika nchi ya Gileadi, na kurudi katika nchi ya Kanaani, kwa watu wa Israeli, na waliwaletea taarifa.
וישב פינחס בן אלעזר הכהן והנשיאים מאת בני ראובן ומאת בני גד מארץ הגלעד אל ארץ כנען--אל בני ישראל וישבו אותם דבר
33 Taarifa yao ilikuwa nzuri katika macho ya watu wa Israeli. Watu wa Israeli walimbarikia Mungu na hawakuendelea kusema tena juu ya kuinua vita dhidi ya Warubeni na Wagadi, ili kuiharibu nchi ambayo walikuwa wanaishi.
וייטב הדבר בעיני בני ישראל ויברכו אלהים בני ישראל ולא אמרו לעלות עליהם לצבא לשחת את הארץ אשר בני ראובן ובני גד ישבים בה
34 Warubeni na Wagadi waliita ile madhabahu “Ushahidi,” kwa kuwa walisema, “Ni ushahidi miongoni mwetu kuwa Yahweh ni Mungu.”
ויקראו בני ראובן ובני גד למזבח כי עד הוא בינתינו כי יהוה האלהים

< Yoshua 22 >