< Yoshua 19 >

1 Upigaji wa pili wa kura uliangukia kwa Simoni na waligawiwa kwa kila ukoo wao. Urithi wao ulikuwa katikati ya urithi ulikuwa ni mali ya kabila la Yuda.
Kura ya pili ikaangukia kabila la Simeoni, ukoo kwa ukoo. Urithi wao ulikuwa ndani ya eneo la Yuda.
2 Urithi waliokuwa nao ni Beerisheba, Sheba, Molada,
Ulijumuisha: Beer-Sheba (au Sheba), Molada,
3 Hazari Shuali, Bala, Ezemu,
Hasar-Shuali, Bala, Esemu,
4 Elitoladi, Bethuli na Horma.
Eltoladi, Bethuli, Horma,
5 Simoni alikuwa pia na Ziklagi, Bethi Markabothi, Hazari Susa,
Siklagi, Beth-Markabothi, Hasar-Susa,
6 Bethi Lebaothi, na Sharuheni. Kulikuwa na miji kumi na mitatu pamoja na vijiji vyake. Vile vile
Beth-Lebaothi na Sharuheni; hii ilikuwa miji kumi na mitatu pamoja na vijiji vyake.
7 Simoni alimiliki Aini, Rimon, Etheri, na Ashani. Hii ilikuwa ni miji minne pamoja na vijiji vyake.
Pia Aini, Rimoni, Etheri, na Ashani; hii ilikuwa miji minne na vijiji vyake,
8 Miji hii pamoja na vijiji vilivyoizunguka hata kufika Baalathi Beeri (ambao ndio Rama katika Negevu). Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Simoni, waliopewa kwa koo zao.
pamoja na vijiji vyote vinavyoizunguka miji hii mpaka Baalath-Beeri (ambayo ndiyo Rama iliyo katika Negebu). Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Simeoni ukoo kwa ukoo.
9 Urithi wa kabila la Simoni ulikuwa sehemu ya himaya ya kabila la Yuda. Hii ni kwasababu nchi waliyopewa kabila la Yuda ilikuwa ni kubwa kwao, na hivyo kabila la Simoni lilipokea urithi wao kutoka katika sehemu yao ya katikati.
Urithi wa Wasimeoni ulitolewa kutoka fungu la Yuda, kwa kuwa fungu la Yuda lilikuwa kubwa kuliko walivyohitaji. Hivyo kabila la Simeoni lilipewa urithi wao ndani ya eneo la Yuda.
10 Upigaji wa kura ya tatu uliangukia kwa kabila la Zabuloni, na walipewa kwa koo zao. Mpaka wa urithi wao ulianzia huko Saridi.
Kura ya tatu ikaangukia kabila la Zabuloni, ukoo kwa ukoo: Mpaka wa urithi wao uliendelea hadi Saridi.
11 Mpaka wao ulipanda upande wa magharibi kuelekea Marala na ukaigusa Dabeshethi, na kisha ukasonga kuelekea kijito kilichokuwa mkabala na Yokineamu.
Kuelekea upande wa magharibi ukafika Marala, ukagusa Dabeshethi, na kuendelea mpaka kwenye bonde karibu na Yokneamu.
12 Kutoka Saridi mpaka ulizunguka upande wa mashariki kuelekea mashariki na ulienda hadi mpaka wa Kislothi Tabori. Kutoka hapo uliendelea hadi Daberathi na kisha ulipanda hata Yafia.
Ukageuka mashariki, kuanzia Saridi kuelekea mawio ya jua hadi kwenye nchi ya Kisiloth-Tabori, na kwenda hadi Daberathi, kupanda Yafia.
13 Kutoka hapo ulipita katika upande wa mashariki mwa Gathi Heferi, na kisha ukafika Ethikazini, baadaye ulienda hadi Rimoni na kisha ukageuka kuelekea Nea.
Kisha ukaendelea mashariki hadi Gath-Heferi na kufika Eth-Kasini, ukatokea Rimoni na kugeuka kuelekea Nea.
14 Mpaka ulizunguka kueleka kaskazini ukafika Hanathoni na ulikomea katika bonde la Ifta Eli.
Huko mpaka ukazungukia upande wa kaskazini hadi Hanathoni na kuishia katika Bonde la Ifta-Eli.
15 Mkoa huu ulijumuisha miji ya Katathi, Nahalali, Shimroni, Idala, na Bethlehemu. Kulikuwa na miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake.
Miji mingine iliyojumuishwa ni Katathi, Nahalali, Shimroni, Idala na Bethlehemu. Kulikuwa na miji kumi na miwili pamoja na vijiji vyake.
16 Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Zabuloni, waliopewa kwa kufuatana na koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.
Miji hii na vijiji vyake ilikuwa ndio urithi wa Zabuloni, ukoo kwa ukoo.
17 Upigaji kura wa nne uliangukia kwa Isakari, na waligawiwa kufuatana na koo zao.
Kura ya nne ikamwangukia Isakari, ukoo kwa ukoo.
18 Eneo lao lilijumuisha Jezreelli, Kesuloothi, Shunemu,
Eneo lao lilijumuisha: Yezreeli, Kesulothi, Shunemu,
19 Hafaraimu, Shioni, na Anaharathi.
Hafaraimu, Shioni, Anaharathi,
20 Pia ilijumuisha miji ya Rabithi, Kishioni, Ebezi,
Rabithi, Kishioni, Ebesi,
21 Remethi, Enganimu, Enihada, na Bethipazezi.
Remethi, En-Ganimu, En-Hada na Beth-Pasesi.
22 Mpaka wao ulifika Tabor, Shahazuma, na Bethi Shemeshi, na ukakomea katika Yordani. Ilikuwa ni miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.
Mpaka ule ukagusa Tabori, Shahasuma na Beth-Shemeshi, na ukaishia kwenye Yordani. Ilikuwa miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.
23 Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Isakari, na walipewa kufuatana na koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.
Miji hii pamoja na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Isakari, ukoo kwa ukoo.
24 Upigaji wa kura ya tano uliangukia kwa kabila la Asheri, na walipewa kwa koo zao.
Kura ya tano ikaangukia kabila la Asheri, ukoo kwa ukoo.
25 Eneo lao lilijumuisha miji ya Helikathi, Hali, Beteni, Akashafu,
Eneo lao lilijumuisha: Helkathi, Hali, Beteni, Akishafu,
26 Alameleki, Amadi, na Mshali. Mpaka wa magharibi ulitanuka hadi Karmeli na Shihori Libnathi.
Alameleki, Amadi na Mishali. Upande wa magharibi mpaka uligusa Karmeli na Shihor-Libnathi.
27 Kisha ulizunguka upande wa mashariki kueleka Bethi Dagoni na ukaenda hadi Zabuloni, na kisha ukafika katika bonde la ifutaheli, upande wa kaskazini mwa Bethemeki na Neieli. Baadaye uliendelea mbele hata Kabuli kueleka upande wa Kaskazini.
Tena ukageuka mashariki kuelekea Beth-Dagoni, ukagusa Zabuloni na Bonde la Ifta-Eli, ukaenda upande wa kaskazini hadi Beth-Emeki na Neyeli, ukipitia Kabul upande wa kushoto.
28 Na kisha ulienda hadi Ebroni, Rehobu, Hammoni, na Kana, hata kufika mji mkubwa wa Sidoni.
Ukaendelea hadi Abdoni, Rehobu, Hamoni na Kana, na kufika Sidoni Kuu.
29 Mpaka ulirudi nyuma kuelekea Rama, na kisha ukafika kwenye mji wa Tiro uliokuwa na ngome. Baada ya hapo mpaka ulizunguka kuelekea Hosa na ulikomea katika bahari, katika mkoa wa Akizibu,
Mpaka huo ukageukia nyuma kuelekea Rama na kwenda hadi kwenye mji wenye ngome wa Tiro, ukageuka kuelekea Hosa na kutokeza baharini katika eneo la Akzibu,
30 Umma, Afeki, na Rehobu. Kulikuwa na miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake.
Uma, Afeki na Rehobu. Ilikuwepo miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake.
31 Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Asheri, na waliopewa kwa koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.
Miji hii pamoja na vijiji vyake ilikuwa ndio urithi wa kabila la Asheri, ukoo kwa ukoo.
32 Upigaji wa kura wa mara ya sita uliangukia kwa kabila la Nafutali, na walipewa kufuatana na koo zao.
Kura ya sita ikaangukia kabila la Naftali, ukoo kwa ukoo:
33 Mpaka wao ulianzia Helefu, kutoka katika mwaloni huko Zaananimu, ulipanda hadi Adaminekebu na Yabneeli, umbali kama Lakumu; na ulikomea katka Yordani.
Mpaka wao uliendelea kutoka Helefi na kwenye mti mkubwa ulio katika Saananimu, ukipitia Adami-Nekebu na Yabineeli hadi Lakumu, na kuishia katika Mto Yordani.
34 Mpaka ule ulizunguka upande wa magharibi kuelekea Aznothi Tabori na ulipanda hadi Hukoki; uligusa Zabuloni katika upande wa kusini, na ulifika hata Asheri katika upande wa magharibi, na Yuda katika upande wa mashariki huko katika mto Yordani.
Mpaka ukaendelea magharibi kupitia Aznoth-Tabori na kutokea Hukoki. Ukagusa Zabuloni upande wa kusini, Asheri upande wa magharibi, na Yordani upande wa mashariki.
35 Miji yenye ngome ilikuwa ni Zidimu, Zeri, Hammathi, Rakathi, Kinnerethi,
Miji yenye ngome ilikuwa Sidimu, Seri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi,
36 Adama, Rama, Hazori,
Adama, Rama, Hazori,
37 Kedeshi, Edrei, na Eni Hazori.
Kedeshi, Edrei, na En-Hasori,
38 Pia kulikuwa na miji ya Yironi, Migdaleli, Horemu, Bethi Anathi, na Bethi Shemeshi. Kulikuwa na miji kumi na tisa, pamoja na vijiji vyake.
Ironi, Migdal-Eli, Horemu, Beth-Anathi na Beth-Shemeshi. Kulikuwa na miji kumi na tisa na vijiji vyake.
39 Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Nafutali, na walipewa miji pamoja na vijiji vyake kufuatana na koo zao.
Miji hiyo pamoja na vijiji vyake ndio iliyokuwa urithi wa kabila la Naftali, ukoo kwa ukoo.
40 Upigaji wa kura ya saba uliangukia kwa kabila la Dani, na walipewa kufuatana na koo zao.
Kura ya saba ikaangukia kabila la Dani, ukoo kwa ukoo.
41 Eneo lao la urithi lilijumuisha miji ya Zora, Eshitaoli, Iri Shemeshi,
Eneo la urithi wao lilijumuisha: Sora, Eshtaoli, Iri-Shemeshi,
42 Shaalabini, Aijaloni, na Ithila.
Shaalabini, Aiyaloni, Ithla,
43 Vile vile lilijumuisha miji ya Eloni, Timna, Ekroni,
Eloni, Timna, Ekroni,
44 Eliteke, Gibethoni, Baalathi,
Elteke, Gibethoni, Baalathi,
45 Yehudi, Bene - Beraki, Gathi Rimoni,
Yehudi, Bene-Beraki, Gath-Rimoni,
46 Me -Yarkoni, na Rakoni sambamba na eneo la karibu na Yopa.
Me-Yarkoni na Rakoni, pamoja na eneo linalotazamana na Yafa.
47 Ilitokea wakati mpaka wa kabila la Dani ulipowapotea, kabila la Dani waliishambulia Leshemu, wakapigana nao, na wakauteka. Waliua kila mtu kwa upanga, wakauchukua ukawa mali yao, na wakakaa ndani yake. Wakauita mji ule Dani jina la babu yao badala ya Leshemu.
(Lakini Wadani walipata shida kulimiliki eneo lao; kwa hiyo walipanda kuishambulia Leshemu, wakaitwaa, wakawaua watu wake kwa upanga na kuukalia. Walikaa Leshemu na kuuita Dani kufuatana na jina la baba yao.)
48 Huu ulikuwa urithi wa kabila la Dani, waliopewa kufuatana na koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.
Miji hii na vijiji vyake ndio iliyokuwa urithi wa kabila la Dani, ukoo kwa ukoo.
49 Walipomaliza kugawana urithi wa nchi, watu wa Israeli walimpa urithi Yoshua mwana wa Nuni kutoka miongoni mwao.
Walipomaliza kugawanya nchi katika migawo kulingana na sehemu zao zilizowaangukia, Waisraeli wakampa Yoshua mwana wa Nuni urithi katikati yao,
50 Kwa amri ya Yahweh walimpatia mji wa Timnathi Sera ambao aliuomba, ulikuwa katika nchi ya milima ya Efraimu. Aliujenga mji na akaishi huko.
kama vile Bwana alivyokuwa ameamuru. Walimpa mji alioutaka, ambao ni Timnath-Sera ulio katika nchi ya vilima ya Efraimu. Naye akajenga mji, akakaa huko.
51 Na huu ndio urithi ambao Eliazari kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa makabila ya familia za mababu zao miongoni mwa watu wa Israeli, waligawa kwa kupiga kura huko Shilo, mbele za Yahweh katika mlango wa hema la kukutania. Na hivyo wakamaliza kuigawa nchi.
Haya ndiyo maeneo ambayo kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa koo za kabila za Israeli waliyoyagawanya kwa kura huko Shilo mbele za Bwana penye ingilio la Hema la Kukutania. Hivyo wakamaliza kuigawanya nchi.

< Yoshua 19 >