< Yoshua 12 >
1 Basi hawa ndio wafalme wa nchi, ambao watu wa Israeli walishindwa. Waisraeli walichukua miliki ya nchi katika upande wa mashariki mwa Yordani sehemu ambako jua huchomoza, kutoka bonde la Mto Arnoni hadi Mlima Hermoni, na nchi yote ya Araba kuelekea kusini.
2 Sihoni, mfalme wa Waamori, aliishi katika Heshiboni. Alitawala kutoka Aroeri, ambayo iko juu ya bonde la Arnoni kutoka katikati ya bonde, na nusu ya Geleadi kushuka mpaka Mto Yaboki katika mpaka wa Waamori.
3 Sihoni pia alitawala juu ya Araba mpaka Bahari ya Kinerethi, kwenda mashariki, kuelekea Bahari ya Araba (Bahari ya Chumvi) upande wa mashariki, hadi huko Bethi Yeshimothi na upande wa kusini, kuelekea chini ya miteremko wa Mlima Pisiga.
4 Ogu, mfalme wa Bashani, mmoja kati ya mabaki ya Rephaimu, aliyeishi huko Shatarothi na Edrei.
5 Alitawala juu ya Mlima Hermoni, Saleka, na Bahani yote, hadi mpaka wa watu wa Geshuri na Wamakathi, na nusu ya Gleadi, hadi kufika mpaka wa Sihohi, mfalme wa Heshboni.
6 Musa mtumishi wa Yahweh, na watu wa Israeli walikuwa wamewashinda, na Musa mtumishi wa Yahweh aliwapa nchi kama mali ya Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase.
7 Hawa ndio wafalme wa nchi ambayo Yoshua na watu wa Israeli waliwashinda katika upande wa magharibi mwa mto Yordani, kutoka Baali Gadi katika bonde karibu na Lebanoni hadi Mlima Halaki karibu na Edom. Yoshua aliyapa nchi makabila ya Israeli ili yaimiliki.
8 Aliwapa nchi ya milima, tambarare, Araba, sehemu za milima, nyika na Negevu, nchi ya Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi.
9 Wafalme hawa walikuwa ni mfalme wa Yeriko, mfalme wa Ai iliyo karibu na Betheli,
10 mfalme wa Yerusalemu, mfalme wa Enaimu,
11 mfalme wa Yarmuthi, mfalme wa Lakishi,
12 mfalme wa Egloni, mfalme wa Gezeri,
13 mfalme wa Debiri, mfalme wa Gederi,
14 mfalme wa Horima, mfalme wa Aradi,
15 mfalme wa Libna, mfalme wa Adula,
16 mfalme wa Makeda, mfalme wa Betheli,
17 mfalme wa Tapua, mfalme wa Heferi,
18 mfalme wa Afeki, mfalme wa Lasharoni,
19 mfalme wa Madoni, mfalme wa Hazori,
20 mfalme wa Shimroni - Meroni, mfalme wa Akshafu.
21 mfalme wa Taanaki, mfalme wa Megido,
22 mfalme wa Kedeshi, mfalme wa Jokineamu katika Karmeli,
23 mfalme wa Dori katika Nafutali Dori, mfalme Goyimu katika Giligali, na
24 mfalme Tiriza. Hesabu ya wafalme ilikuwa ni thelathini na moja kwa ujumla wake.