< Yohana 2 >

1 Baada ya siku tatu, kulikuwa na arusi huko Kana ya Galilaya na mama yake Yesu alikuwa huko. 2 Yesu na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa katika arusi. 3 Wakati walipoishiwa na divai, mama yake Yesu akamwambia, “Hawana divai.” 4 Yesu akajibu, “Mwanamke hiyo inanihusu nini mimi? Muda wangu mimi bado haujatimia.” 5 Mama yake akawambia watumishi, “Chochote atakachowambia fanyeni.” 6 Basi kulikuwa na mitungi sita ya mawe pale iliyowekwa kwa ajili ya kunawa katika sikukuu za Wayahudi, kila moja lilikuwa na ujazo wa nzio mbili tatu. 7 Yesu akawambia, “Ijazeni maji mitungi ya mawe.” Wakajaza hadi juu. 8 Kisha akawambia wale watumishi, “Chukueni kiasi sasa na mpeleke kwa muhudumu mkuu wa meza.” Wakafanya kama walivyoagizwa. 9 Mhudumu mkuu aliyaonja yale maji yaliyokuwa yamebadilika na kuwa divai, ila hakujua yalikotoka (lakini watumishi waliochota maji walijua yalikotoka). Kisha akamwita bwana harusi na 10 kumwambia, “Kila mmoja huanza kuwahudumia watu divai nzuri na wakiishalewa huwapa divai isiyo nzuri. Lakini wewe umeitunza divai nzuri hadi sasa” 11 Muujiza huu wa Kana ya Galilaya, ulikuwa ndio mwanzo wa ishara za miujiza aliyoifanya Yesu, akifunua utukufu wake, hivyo wanafunzi wake wakamwamini. 12 Baada ya hii, Yesu, mama yake, ndugu zake na wanafunzi wake walienda katika mji wa Kapernaum na wakaa huko kwa siku chache. 13 Basi Pasaka ya Wayahudi ilikuwa imekaribia, hivyo Yesu akaenda Yerusalemu. 14 Akawakuta wauzaji wa ng'ombe, kondoo, na njiwa ndani ya Hekalu. Pia na wabadilisha fedha walikuwa wameketi ndani ya Hekalu. 15 Yesu akatengeneza mjeledi wenye vifundo, akawatoa wote walikuwemo katika hekalu, ikijumuisha ng'ombe na kondoo. Akamwaga fedha za wabadili fedha na kuzipindua meza zao. 16 Kwa wauzaji wa njiwa akawambia, “Toeni vitu hivi mbali na mahali hapa, acheni kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa mahali pa soko.” 17 Wanafunzi wake wakakumbuka kuwa ilikuwa imeandikwa, “Wivu wa nyumba yako utanila.” 18 Wakuu wa Kiyahudi wakajibu, wakamwambia, Ni ishara ipi utakayoionyesha kwa sababu unayafanya mambo haya?” 19 Yesu akawajibu, libomoeni Hekalu hili nami nitalijenga baada ya siku tatu.” 20 Kisha wakuu wa Wayahudi wakasema, “Iligharimu miaka arobaini na sita kujenga hekalu hili nawe unasema utalijenga kwa siku tatu?” 21 Ingawa, yeye aliongea hekalu akimaanisha mwili wake. 22 Hivyo baadaye baada ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu, wanafunzi wake wakakumbuka kuwa alisema hivyo, wakaamini maandiko na kauli hii ambayo Yesu alikuwa amekwisha kuisema. 23 Basi alipokuwa Yerusalemu wakati wa Pasaka, wakati wa sikukuu watu wengi waliamini jina lake, walipoona ishara ya miujiza aliyoifanya. 24 Lakini Yesu hakuwa na imani nao kwa sababu aliwajua wanadamu wote. 25 Hakuhitaji mtu yeyote kumwambia kuhusu walivyo wanadamu kwa sababu alijua kilichokuwamo ndani yao.

< Yohana 2 >