< Yohana 18 >
1 Baada ya Yesu kusema maneno haya, aliondoka na wanafunzi wake kuelekea bonde la Kidron, ambako kulikuwa na bustani, ambako yeye na wanafunzi wake wakaingia ndani yake.
COMO Jesús hubo dicho estas cosas, salióse con sus discípulos tras el arroyo de Cedrón, donde estaba un huerto, en el cual entró Jesús y sus discípulos.
2 Sasa yule Yuda, aliyetaka kumsaliti, naye alilijua eneo hilo, kwani Yesu alikuwa akienda hili eneo mara kadhaa akiwa na wanafunzi wake.
Y también Judas, el que le entregaba, sabía aquel lugar; porque muchas veces Jesús se juntaba allí con sus discípulos.
3 Naye Yuda, baada ya kuwa amepata kundi la maaskari na maofisa toka kwa wakuu wa makuhani, wakaja wakiwa na taa, kurunzi na silaha.
Judas pues tomando una compañía, y ministros de los pontífices y de los Fariseos, vino allí con linternas y antorchas, y con armas.
4 Naye Yesu, hali akijua kila kitu kilichokuwa kikifanyika dhidi yake, alijitokeza mbele na akawauliza, “Ni nani mnayemtafuta?”
Empero Jesús, sabiendo todas las cosas que habían de venir sobre él, salió delante, y díjoles: ¿A quién buscáis?
5 Nao wakamjibu, “Yesu Mnazareth.” Yesu akawaambia, “Mimi ndiye” Naye Yuda aliyemsaliti, alikuwa amesimama pamoja na wale askari.
Respondiéronle: A Jesús Nazareno. Díceles Jesús: Yo soy. (Y estaba también con ellos Judas, el que le entregaba.)
6 Kwa hiyo alipowaambia, “Mimi ndiye” walirudi kinyume na kuanguka chini.
Y como les dijo, Yo soy, volvieron atrás, y cayeron en tierra.
7 Halafu akawauliza tena, “Ni nani mnayemtafuta? Nao wakamjibu tena “Yesu mnazareth.”
Volvióles, pues, á preguntar: ¿A quién buscáis? Y ellos dijeron: A Jesús Nazareno.
8 Yesu akawajibu, “Nimekwisha kuwaambia kuwa Mimi ndiye; kwa hiyo kama mnanitafuta mimi, waacheni hawa wengine waende.”
Respondió Jesús: Os he dicho que yo soy: pues si á mí buscáis, dejad ir á éstos.
9 Haya yalikuwa hivyo ili lile neno litimilike; pale aliposema; “Katika wale ulionipa, sikumpoteza hata mmoja.”
Para que se cumpliese la palabra que había dicho: De los que me diste, ninguno de ellos perdí.
10 Ndipo Simon Petro, aliyekuwa na upanga, akaufuta na kumkata sikio la kulia mtumishi wa Kuhani mkuu. Na jina lake mtumishi yule lilikuwa Malko.
Entonces Simón Pedro, que tenía espada, sacóla, é hirió al siervo del pontífice, y le cortó la oreja derecha. Y el siervo se llamaba Malco.
11 Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako kwenye ala yake. Kwa nini nisikinywee kikombe kile alichonipa Baba?”
Jesús entonces dijo á Pedro: Mete tu espada en la vaina: el vaso que el Padre me ha dado, ¿no lo tengo de beber?
12 Basi lile kundi la askari na jemedari, na watumishi wa Wayahudi, walimkamata Yesu na kumfunga.
Entonces la compañía y el tribuno, y los ministros de los Judíos, prendieron á Jesús y le ataron,
13 Nao wakamwongoza kwanza mpaka kwa Anasi, kwani yeye alikuwa mkwe wa Kayafa, ambaye ndiye aliyekuwa Kuhani mkuu kwa mwaka huo.
Y lleváronle primeramente á Anás; porque era suegro de Caifás, el cual era pontífice de aquel año.
14 Sasa Kayafa ndiye aliyekuwa amewapa ushauri Wayahudi ya kwamba ilimpasa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu.
Y era Caifás el que había dado el consejo á los Judíos, que era necesario que un hombre muriese por el pueblo.
15 Simon Petro alimfuata Yesu, na vivyo hivyo mwanafunzi mwingine. Na yule mwanafunzi alikuwa akifahamika kwa kuhani mkuu, naye akaingia pamoja na Yesu katika behewa ya Kuhani mkuu;
Y seguía á Jesús Simón Pedro, y otro discípulo. Y aquel discípulo era conocido del pontífice, y entró con Jesús al atrio del pontífice;
16 lakini Petro alikuwa amesimama nje ya mlango. Basi yule mwanafunzi aliyekuwa akifahamika kwa kuhani mkuu, alitoka nje akaenda kuongea na yule mwanamke mtumishi aliyekuwa akilinda mlango na kumwingiza Petro ndani.
Mas Pedro estaba fuera á la puerta. Y salió aquel discípulo que era conocido del pontífice, y habló á la portera, y metió dentro á Pedro.
17 Basi yule kijakazi aliyekuwa akilinda mlango, alimwambia Petro, “Je wewe si mmoja wa wafuasi wa huyu mtu?” Naye akasema, “Mimi siye.”
Entonces la criada portera dijo á Pedro: ¿No eres tú también de los discípulos de este hombre? Dice él: No soy.
18 Na wale watumishi na wakuu walikuwa wakisimama mahali pale; wamekoka moto wa kwa maana, kulikuwa na baridi, na hivyo walikuwa wakiota moto ili kupata joto. Naye Petro alikuwa nao, akiota moto akiwa amesimama.
Y estaban en pie los siervos y los ministros que habían allegado las ascuas; porque hacía frío, y calentábanse: y estaba también con ellos Pedro en pie, calentándose.
19 Kuhani mkuu alimhoji Yesu juu ya wanafunzi wake na mafundisho yake.
Y el pontífice preguntó á Jesús acerca de sus discípulos y de su doctrina.
20 Yesu akamjbu, “Nimeuambia waziwazi ulimwengu; Mimi nilifundisha mara kwa mara kwenye masinagogi na hekaluni mahali ambapo wayahudi hukusanyika. Nami sikusema lolote katika siri.
Jesús le respondió: Yo manifiestamente he hablado al mundo: yo siempre he enseñado en la sinagoga y en el templo, donde se juntan todos los Judíos, y nada he hablado en oculto.
21 Kwa nini mliniuliza? Waulizeni walionisikiliza juu ya kile nilichosema. Hawa watu wanajua mambo yale niliyosema.
¿Qué me preguntas á mí? Pregunta á los que han oído, qué les haya yo hablado: he aquí, ésos saben lo que yo he dicho.
22 Yesu alipokwisha sema hivyo, mmoja wa wakuu aliyekuwa amesimama akampiga Yesu kwa mkono wake na kisha akasema, “Je, hivyo ndivyo inavyokupasa kumjibu kuhani mkuu?”
Y como él hubo dicho esto, uno de los criados que estaba allí, dió una bofetada á Jesús, diciendo: ¿Así respondes al pontífice?
23 Naye Yesu akamjibu, “Kama nimesema jambo lolote baya basi uwe shahidi kwa ajili ya uovu, na kama nimemjibu vyema kwa nini kunipiga?
Respondióle Jesús: Si he hablado mal, da testimonio del mal: y si bien, ¿por qué me hieres?
24 Ndipo Anasi alipompeleka Yesu kwa Kayafa kuhani mkuu akiwa amefungwa.
Y Anás le había enviado atado á Caifás pontífice.
25 Sasa Simoni Petro alikuwa amesimama akijipasha joto mwenyewe. Halafu wale watu wakamwambia. “Je, wewe pia si mmoja wa wanaafunzi wake?” Akakana akisema “Mimi siye.”
Estaba pues Pedro en pie calentándose. Y dijéronle: ¿No eres tú de sus discípulos? El negó, y dijo: No soy.
26 Mmoja wa watumishi wa kuhani mkuu, ambaye alikuwa ndugu wa yule mwanaume ambaye Petro alimkata sikio, alisema, “Je si wewe niliyekuona naye kule bustanini?”
Uno de los siervos del pontífice, pariente de aquél á quien Pedro había cortado la oreja, [le] dice: ¿No te vi yo en el huerto con él?
27 Petro akakana tena, na mara Jogoo akawika.
Y negó Pedro otra vez: y luego el gallo cantó.
28 Kisha wakamchukua Yesu toka kwa Kayafa mpaka kwenye Praitorio. Ilikwa asubuhi na mapema. Wao wenyewe hawakuiingia ile Praitorio ili wasije wakanajisika na kuila pasaka.
Y llevaron á Jesús de Caifás al pretorio: y era por la mañana: y ellos no entraron en el pretorio por no ser contaminados, sino que comiesen la pascua.
29 Kwa hiyo Pilato akawaendea akisema. “Ni shitaka gani linalomhusu huyu mtu?”
Entonces salió Pilato á ellos fuera, y dijo: ¿Qué acusación traéis contra este hombre?
30 Wakamjibu na kumwambia, “Kama huyu mtu asingekuwa mtenda maovu, tusingemleta kwako.”
Respondieron y dijéronle: Si éste no fuera malhechor, no te le habríamos entregado.
31 Pilato akawaambia, “Mchukueni ninyi wenyewe, mkamhukumu kulingana na sheria yenu.” Nao Wayahudi wakamwambia, “Sheria haituruhusu sisi kumwua mtu yeyote.”
Díceles entonces Pilato: Tomadle vosotros, y juzgadle según vuestra ley. Y los Judíos le dijeron: A nosotros no es lícito matar á nadie:
32 Walisema haya ili neno la Yesu litimilike, neno ambalo alikuwa amekwisha sema juu ya aina ya kifo chake.
Para que se cumpliese el dicho de Jesús, que había dicho, dando á entender de qué muerte había de morir.
33 Basi Pilato akaingia tena Praitorio akumwita Yesu; akamwambia, “Je, wewe ni mfalme wa Wayahudi?”
Así que, Pilato volvió á entrar en el pretorio, y llamó á Jesús, y díjole: ¿Eres tú el Rey de los Judíos?
34 Yesu akamjibu, “Je, wewe waniuliza swali hili kwa Sababu wataka kujua au kwa sababu wengine wamekutuma ili uniulize mimi?”
Respondióle Jesús: ¿Dices tú esto de ti mismo, ó te lo han dicho otros de mí?
35 Naye Pilato akamjibu, “Mimi si Myahudi, au sivyo?” Taifa lako na kuhani mkuu ndio waliokuleta kwangu; wewe umefanya nini?
Pilato respondió: ¿Soy yo Judío? Tu gente, y los pontífices, te han entregado á mí: ¿qué has hecho?
36 Yesu akajibu; “Ufalme wangu si wa ulimwengu huu, kama ufalme wangu ungekuwa na sehemu katika ulimwengu huu watumwa wangu wangenipigania ili nisitolewe kwa wayahudi. Kwa kweli ufalme wangu hautoki hapa” Basi
Respondió Jesús: Mi reino no es de este mundo: si de este mundo fuera mi reino, mis servidores pelearían para que yo no fuera entregado á los Judíos: ahora, pues, mi reino no es de aquí.
37 Pilato akamwambia, “Je, wewe basi u mfalme?” Yesu akajibu, “wewe ndivyo unanvyosema kuwa mimi ni mfalme, Kwa sababu hii mimi nilizaliwa na kwa sababu hii mimi nimekuja ulimwenguni ili niwe shahidi wa ile kweli. Yeyote aliye wa hiyo kweli huisikiliza sauti yangu.
Díjole entonces Pilato: ¿Luego rey eres tú? Respondió Jesús: Tú dices que yo soy rey. Yo para esto he nacido, y para esto he venido al mundo, para dar testimonio á la verdad. Todo aquél que es de la verdad, oye mi voz.
38 Pilato akamwambia, “Kweli ni nini?” Naye alipokwisha sema haya akaenda kwa Wayahudi na kuwaambia “Siona katika lolote mtu huyu.
Dícele Pilato: ¿Qué cosa es verdad? Y como hubo dicho esto, salió otra vez á los Judíos, y díceles: Yo no hallo en él ningún crimen.
39 Ninyi mna utamaduni unaonifanya nimfunfungulie mfungwa mmoja wakati wa Pasaka. Je mnataka nimfungulie mfalme wa Wayahudi.”
Empero vosotros tenéis costumbre, que os suelte uno en la Pascua: ¿queréis, pues, que os suelte al Rey de los Judíos?
40 Kisha walipiga kelele wakisema, siyo huyu, tufungulie Baraba.” Naye Baraba alikuwa mnyang'anyi.
Entonces todos dieron voces otra vez, diciendo: No á éste, sino á Barrabás. Y Barrabás era ladrón.