< Yohana 10 >

1 Amin, Amini nawaambieni, yule asiyeingia kwa kupitia mlango wa zizi la kondoo, lakini anapanda kwa njia nyingine, mtu huyo ni mwizi na mnyang'anyi.
En verdad, en verdad les digo: El que no entra por la puerta en el redil de las ovejas, pero se mete por otro lugar es ladrón y asaltante.
2 Yeye aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo.
Pero el que entra por la puerta es [el] pastor de las ovejas.
3 Kwake mlinzi wa mlango humfungulia. Kondoo waisikia sauti yake na huwaita kondoo zake kwa majina yao na kuwatoa nje.
El portero le abre y las ovejas oyen su voz. Llama a sus ovejas por nombre y las saca.
4 Atakapowatoa nje hao walio wake, huwatangulia, na kondoo humfuata, kwa sababu wanaijua sauti yake.
Cuando saque todas las suyas, va delante de ellas. Las ovejas lo siguen porque conocen su voz.
5 Hawatamfuata mgeni lakini badala yake watamuepuka, kwa sababu hawazijui sauti za wageni.”
De ningún modo seguirán al extraño, sino huirán de él, porque no conocen la voz de los extraños.
6 Yesu alisema mfano huu kwao, lakini hawakuyaelewa mambo haya ambayo alikuwa akisema kwao.
Jesús les dijo esta alegoría, pero ellos no entendieron lo que les decía.
7 Yesu akasema nao tena, “Amini, amini, nawaambia, Mimi ni mlango wa kondoo.
Jesús les habló otra vez: En verdad, en verdad les digo: Yo soy la Puerta de las ovejas.
8 Wote walionitangulia ni wezi na wanyang'anyi, lakini kondoo hawakuwasikiliza.
Todos los que vinieron antes de Mí son ladrones y asaltantes, pero las ovejas no los oyeron.
9 Mimi ni mlango. Yeyote aingiaye kupitia kwangu, ataokolewa; ataingia ndani na kutoka, naye atajipatia malisho.
Yo soy la Puerta. Si alguno entra por Mí será salvo. Entrará y saldrá, y hallará pasto.
10 Mwizi haji isipokuwa kuiba, kuua, na kuangamiza. Nimekuja ili kwamba wapate uzima na wawe nao tele.
El ladrón no viene sino para robar, matar y destruir. Yo vine para que tengan vida, y [la] tengan en abundancia.
11 Mimi ni mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.
Yo soy el excelente Pastor. El excelente Pastor da su vida por las ovejas.
12 Mtumishi aliyeajiriwa, na siyo mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, huwaona mbwa mwitu wakija na huwaacha na kuwakimbia kondoo.
El asalariado, que no es el pastor, ni le pertenecen las ovejas, cuando ve el lobo que se acerca, huye y abandona las ovejas. El lobo las ataca y [las] dispersa.
13 Na mbwa mwitu huwakamata na kuwatawanya. Hukimbia kwa sababu ni mtumishi wa kuajiriwa na hawajali kondoo.
[Él huye] porque es asalariado y no le importan las ovejas.
14 Mimi ni mchungaji mwema, na ninawajua walio wangu, nao walio wangu wananijua mimi.
Yo soy el excelente Pastor. Conozco mis ovejas y las mías me conocen,
15 Baba ananijua, nami namjua Baba, nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo.
como el Padre me conoce y Yo lo conozco. Y doy mi vida por las ovejas.
16 Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili. Hao pia, yanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu ili kwamba pawepo na kundi moja na mchungaji mmoja.
Además tengo otras ovejas que no son de este redil. A ellas también debo traer y oirán mi voz. Habrá un rebaño y un Pastor.
17 Hii ndiyo sababu Baba ananipenda: Niutoe uhai wangu halafu niutwae tena.
Por esto el Padre me ama, porque Yo doy mi vida para volverla a tomar.
18 Hakuna auchukuaye kutoka kwangu, lakini mimi nautoa mwenyewe. Ninayo mamlaka ya kuutoa, na ninayo mamlaka ya kuutwaa pia. Nimelipokea agizo hili kutoka kwa Baba.”
Nadie me la quita, sino Yo la doy de Mí mismo. Tengo autoridad para darla y para volverla a tomar. Este Mandamiento recibí de mi Padre.
19 Mgawanyiko tena ukatokea kati ya wayahudi kwa sababu ya maneno haya.
Otra vez hubo una división entre los judíos por estas palabras.
20 Wengi wao wakasema, “Ana pepo na ni kichaa. Kwa nini mnamsikiliza?”
Muchos de ellos decían: Tiene demonio y está fuera de sí. ¿Por qué lo oyen?
21 Wengine wakasema, “Haya siyo maneno ya mtu aliyepagawa na mapepo. Pepo linaweza kufungua macho ya kipofu?”
Otros decían: Estas palabras no son de un endemoniado. ¿Puede un demonio abrir ojos de ciegos?
22 Ndipo ikaja Sikukuu ya Kuwekwa Wakfu Yerusalemu.
En Jerusalén se celebraba la fiesta de La Dedicación. Era invierno,
23 Ulikuwa wakati wa baridi, na Yesu alikuwa akitembea hekaluni katika ukumbi wa Selemani.
y Jesús caminaba en el Templo por el patio de Salomón.
24 Ndipo Wayahudi walipomzunguka na kumwambia, “Mpaka lini utatuweka katika mashaka? kama wewe ni Kristo, tuambie wazi.
Entonces los judíos lo rodearon y le preguntaban: ¿Hasta cuándo nos mantienes en suspenso? Dinos con claridad si Tú eres el Cristo.
25 Yesu akawajibu, “Nimekwisha waambia lakini hamuamini. Kazi nizifanyazo kwa jina la Baba yangu, hizo zinashuhudia juu yangu.
Jesús les respondió: Les dije, y no creen. Las obras que Yo hago en el Nombre de mi Padre dan testimonio de Mí,
26 Hata hivyo hamuamini kwa sababu ninyi si kondoo wangu.
pero ustedes no creen porque no son de mis ovejas.
27 Kondoo wangu waisikia sauti yangu; Nawajua, nao wanifuata mimi.
Mis ovejas oyen mi voz. Yo las conozco y me siguen.
28 Nimewapa uzima wa milele; hawataangamia kamwe, na hakuna hata mmoja atakayewanyakuwa kutoka mkononi mwangu. (aiōn g165, aiōnios g166)
Yo les doy vida eterna, y que ninguna perezca jamás. Nadie las arrebatará de mi mano. (aiōn g165, aiōnios g166)
29 Baba yangu, aliyenipa hao, ni mkuu kuliko wengine wote, na hakuna hata mmoja aliye na uwezo wa kuwanyakua kutoka mkononi mwa Baba.
Lo que me dio mi Padre es mayor que todo y nadie [lo] arrebata de la mano del Padre.
30 Mimi na Baba tu mmoja.”
Yo y el Padre somos uno.
31 Wakabeba mawe ili wamponde tena.
Los judíos tomaron piedras otra vez para apedrearlo.
32 Yesu akawajibu, “Nimeshawaonesha kazi nyingi nzuri kutoka kwa Baba. Kwa kazi zipi kati ya hizo mnataka kuniponda mawe?”
Jesús les dijo: Les mostré muchas buenas obras de mi Padre. ¿Por cuál de ellas me apedrean?
33 Wayahudi wakamjibu, “Hatukupondi mawe kwa kazi yoyote iliyo nzuri, lakini kwa kukufuru, kwa sababu wewe, uliye mtu, unajifanya kuwa Mungu.”
Los judíos respondieron: No te apedreamos por buenas obras sino por blasfemia, porque Tú, Quien eres Hombre, te proclamas Dios.
34 Yesu akawajibu, “Haikuandikwa katika sheria yenu, 'Nilisema, “Ninyi ni miungu”'?”
Jesús les respondió: ¿No está escrito en la Ley de ustedes? Yo dije que ustedes son dioses.
35 Ikiwa aliwaita miungu, kwa wale ambao Neno la Mungu liliwajilia (na Maandiko hayawezi kuvunjwa),
Si llamó dioses a aquellos a quienes se dirigió la Palabra de Dios (y la Escritura no puede ser quebrantada),
36 mnasema juu ya yule ambaye Baba alimtoa na kumtuma katika ulimwengu, 'Unakufuru,' kwa sababu nilisema, 'mimi ni Mwana wa Mungu'?
¿al que el Padre santificó y envió al mundo, ustedes le dicen que blasfema, porque dije que soy Hijo de Dios?
37 “Ikiwa sifanyi kazi za Baba yangu, msiniamini.
Si no hago las obras de mi Padre, no me crean.
38 Hata hivyo, ikiwa ninazifanya, hata kama hamniamini, ziaminini kazi ili kwamba muweze kujua na kufahamu kwamba Baba yuko ndani yangu na mimi niko ndani ya Baba.”
Pero si [las] hago, aunque no me crean a Mí, crean en las obras, para que sepan y entiendan que el Padre está en Mí y Yo en el Padre.
39 Wakajaribu tena kumkamata Yesu, lakini alienda zake kutoka mikononi mwao.
Otra vez [los judíos] intentaron arrestarlo, pero escapó de sus manos.
40 Yesu akaenda zake tena ng'ambo ya Yordani sehemu ambayo Yohana alikuwa akibatiza kwanza, na akakaa huko.
Volvió al otro lado del Jordán, donde Juan bautizaba al principio, y permaneció allí.
41 Watu wengi wakaja kwa Yesu. Waliendelea kusema, “Yohana kweli hakufanya ishara yoyote, lakini mambo yote aliyoyasema Yohana juu ya huyu mtu ni ya kweli.”
Muchos acudieron a Él y decían: Juan, a la verdad, ninguna señal hizo, pero todas las cosas que Juan dijo con respecto a Éste eran verdaderas.
42 Watu wengi wakamwamini Yesu hapo.
Allí muchos creyeron en Él.

< Yohana 10 >