< Ayubu 9 >
1 Kisha Ayubu akajibu na kusema,
2 “kweli najua kwamba ndivyo hivyo. Lakini ni kwa namna gani mtu anakuwa na haki kwa Mungu?
3 Kama akitaka kujibishana na Mungu, hatamjibu yeye mara moja katika elfu zaidi.
4 Mungu ni mwenye hekima moyoni na ukuu katika nguvu; ni nani daima aliyejifanya mwenyewe kuwa mgumu dhidi yake na akafanikiwa? -
5 ambaye huiondoa milima bila kumtahadharisha yeyote wakati akiipindua katika hasira zake -
6 ambaye huitikisa nchi itoke mahali pake na mihimili yake hutikisika.
7 Ni Mungu yule yule ambaye huliamuru jua lisichomoze, nalo halichomozi, na ambaye huzihifadhi nyota,
8 ambaye peke yake ni mwenye kupanua mbingu na kuyatuliza mawimbi ya bahari,
9 ambaye huumba Dubu, Orioni, kilima, na makundi ya nyota ya kusini.
10 Ni Mungu yule yule atendaye mambo makuu, mambo yasiyofahamika - hasa, mambo ya ajabu yasiyohesabika.
11 Tazama, huenda karibu nami, na siwezi kumuona yeye; pia hupita kwenda mbele, lakini ni simtambue.
12 Kama akichukua kitu chochote, nani atamzuia? Nani awezaye kumuuliza, 'unafanya nini?'
13 Mungu hataondoa hasira yake; wamsaidiao Rahabu huinama chini yake.
14 Je ni upungufu kiasi gani mimi nitamjibu, je nichague maneno kuhojiana naye?
15 Hata kama ni mwenye haki, nisingelimjibu; ningeomba msamaha tu kwa hukumu yangu.
16 Hata kama ningelimwita na yeye akanitikia, nisingeamini kuwa ameisikia sauti yangu.
17 kwa kuwa yeye anidhoofishaye kwa dhoruba na kuyaongeza majeraha yangu pasipo sababu.
18 Yeye hataki hata kuniruhusu nipate kuvuta pumzi; badala yake, hunijaza uchungu.
19 Kama ni habari ya nguvu, tazama! yeye ni mwenye uwezo! Kama ni habari ya haki, ni nani atakaye mhukumu?
20 Ingawa ni mwenye haki, kinywa changu mwenyewe kitanihukumu; na ingawa ni mtakatifu, maneno yangu yatashuhudia kuwa ni mwenye kosa.
21 Mimi ni mtakatifu, lakini siijali zaidi nafsi yangu; Naudharau uhai wangu mwenyewe.
22 Haileti tofauti yoyote, kwa sababu hiyo nasema kwamba yeye huangamiza watu wasio na makosa na waovu pia.
23 Kama hilo pigo likiua ghafla, yeye atafurahi mateso yake mtu asiye na kosa.
24 Dunia imetiwa mkononi mwa watu waovu; Mungu hufunika nyuso za waamuzi wake. kama si yeye hufanya, ni nani basi?
25 Siku zangu zinapita haraka kuliko tarishi akimbiae; siku zangu zinakimbia mbali; wala hazioni mema mahali popote.
26 Zinapita kama mashua zilizoundwa kwa mafunjo ziendazo kwa kasi, na zinakasi kama tai ashukaye upesi katika mawindo yake.
27 Kama ni kisema kwamba mimi nitasahau kuhusu manung'uniko yangu, kwamba nitaacha kuonyesha sura ya huzuni na kuwa na furaha,
28 Mimi nitaziogopa huzuni zangu zote kwa sababu nafahamu kuwa hutanihesabu kuwa sina hatia.
29 Nitahukumiwa; kwa nini, basi, nitaabike bure?
30 Kama najiosha mwenyewe kwa maji ya theluji na kuitakasa mikono yangu na kuwa safi zaidi,
31 Mungu atanitumbukiza shimoni, na nguo zangu mwenyewe zitanichukia.
32 Kwa kuwa Mungu si mtu, kama mimi, kwamba naweza kumjibu, hata tukaribiane katika hukumu.
33 Hakuna hakimu baina yetu awezaye kuweka mkono wake juu yetu sote.
34 Hakuna hakimu mwingine ambaye anaweza kuniondolea fimbo ya Mungu, awezaye kuzuia kitisho chake kisinitie hofu. kisha ningesema na nisimuogope.
35 Lakini kama mambo yalivyo sasa, sitaweza kufanya hivyo.