< Ayubu 9 >
1 Kisha Ayubu akajibu na kusema,
Kisha Ayubu akajibu:
2 “kweli najua kwamba ndivyo hivyo. Lakini ni kwa namna gani mtu anakuwa na haki kwa Mungu?
“Naam, najua hili ni kweli. Lakini mwanadamu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu?
3 Kama akitaka kujibishana na Mungu, hatamjibu yeye mara moja katika elfu zaidi.
Ingawa mtu angetaka kushindana naye, asingaliweza kumjibu Mungu hata mara moja miongoni mwa elfu moja.
4 Mungu ni mwenye hekima moyoni na ukuu katika nguvu; ni nani daima aliyejifanya mwenyewe kuwa mgumu dhidi yake na akafanikiwa? -
Hekima yake ni kubwa sana na ana uwezo mwingi mno. Ni nani aliyempinga naye akawa salama?
5 ambaye huiondoa milima bila kumtahadharisha yeyote wakati akiipindua katika hasira zake -
Aiondoa milima bila yenyewe kujua na kuipindua kwa hasira yake.
6 ambaye huitikisa nchi itoke mahali pake na mihimili yake hutikisika.
Aitikisa dunia kutoka mahali pake na kuzifanya nguzo zake zitetemeke.
7 Ni Mungu yule yule ambaye huliamuru jua lisichomoze, nalo halichomozi, na ambaye huzihifadhi nyota,
Husema na jua, nalo likaacha kuangaza; naye huizima mianga ya nyota.
8 ambaye peke yake ni mwenye kupanua mbingu na kuyatuliza mawimbi ya bahari,
Yeye peke yake huzitandaza mbingu na kuyakanyaga mawimbi ya bahari.
9 ambaye huumba Dubu, Orioni, kilima, na makundi ya nyota ya kusini.
Yeye ndiye Muumba wa nyota za Dubu, na Orioni, Kilimia, na makundi ya nyota za kusini.
10 Ni Mungu yule yule atendaye mambo makuu, mambo yasiyofahamika - hasa, mambo ya ajabu yasiyohesabika.
Hutenda maajabu yasiyopimika, miujiza isiyoweza kuhesabiwa.
11 Tazama, huenda karibu nami, na siwezi kumuona yeye; pia hupita kwenda mbele, lakini ni simtambue.
Anapopita karibu nami, siwezi kumwona; apitapo mbele yangu, simtambui.
12 Kama akichukua kitu chochote, nani atamzuia? Nani awezaye kumuuliza, 'unafanya nini?'
Anapochukua kwa ghafula, ni nani awezaye kumzuia? Ni nani awezaye kumwambia, ‘Unafanya nini?’
13 Mungu hataondoa hasira yake; wamsaidiao Rahabu huinama chini yake.
Mungu hataizuia hasira yake; hata jeshi kubwa la Rahabu lenye nguvu linajikunyata miguuni pake.
14 Je ni upungufu kiasi gani mimi nitamjibu, je nichague maneno kuhojiana naye?
“Ni vipi basi mimi nitaweza kubishana naye? Nawezaje kupata maneno ya kuhojiana naye?
15 Hata kama ni mwenye haki, nisingelimjibu; ningeomba msamaha tu kwa hukumu yangu.
Ingawa sikuwa na hatia, sikuweza kumjibu; ningeweza tu kumsihi Mhukumu wangu anihurumie.
16 Hata kama ningelimwita na yeye akanitikia, nisingeamini kuwa ameisikia sauti yangu.
Hata kama ningemwita kwenye shauri, naye akakubali, siamini kama angenisikiliza.
17 kwa kuwa yeye anidhoofishaye kwa dhoruba na kuyaongeza majeraha yangu pasipo sababu.
Yeye angeniangamiza kwa dhoruba na kuongeza majeraha yangu pasipo na sababu.
18 Yeye hataki hata kuniruhusu nipate kuvuta pumzi; badala yake, hunijaza uchungu.
Asingeniacha nipumue bali angenifunika kabisa na huzuni kuu.
19 Kama ni habari ya nguvu, tazama! yeye ni mwenye uwezo! Kama ni habari ya haki, ni nani atakaye mhukumu?
Kama ni suala la nguvu, yeye ni mwenye nguvu! Kama ni suala la haki, ni nani awezaye kumwita mahakamani?
20 Ingawa ni mwenye haki, kinywa changu mwenyewe kitanihukumu; na ingawa ni mtakatifu, maneno yangu yatashuhudia kuwa ni mwenye kosa.
Hata kama sikuwa na hatia, kinywa changu kingenihukumu; kama sikuwa na kosa, kingenitangaza kuwa mwenye hatia.
21 Mimi ni mtakatifu, lakini siijali zaidi nafsi yangu; Naudharau uhai wangu mwenyewe.
“Ingawa mimi sina kosa, haileti tofauti katika nafsi yangu; nauchukia uhai wangu.
22 Haileti tofauti yoyote, kwa sababu hiyo nasema kwamba yeye huangamiza watu wasio na makosa na waovu pia.
Hayo yote ni sawa; ndiyo sababu nasema, ‘Yeye huwaangamiza wasio na makosa pamoja na waovu.’
23 Kama hilo pigo likiua ghafla, yeye atafurahi mateso yake mtu asiye na kosa.
Wakati pigo liletapo kifo cha ghafula, yeye hudhihaki kule kukata tamaa kwa yule asiye na kosa.
24 Dunia imetiwa mkononi mwa watu waovu; Mungu hufunika nyuso za waamuzi wake. kama si yeye hufanya, ni nani basi?
Wakati nchi inapoangukia mikononi mwa waovu, yeye huwafunga macho mahakimu wake. Kama si yeye, basi ni nani?
25 Siku zangu zinapita haraka kuliko tarishi akimbiae; siku zangu zinakimbia mbali; wala hazioni mema mahali popote.
“Siku zangu zapita mbio kuliko mkimbiaji; zinapita upesi bila kuona furaha hata kidogo.
26 Zinapita kama mashua zilizoundwa kwa mafunjo ziendazo kwa kasi, na zinakasi kama tai ashukaye upesi katika mawindo yake.
Zinapita upesi kama mashua ya mafunjo, mfano wa tai ayashukiaye mawindo kwa ghafula.
27 Kama ni kisema kwamba mimi nitasahau kuhusu manung'uniko yangu, kwamba nitaacha kuonyesha sura ya huzuni na kuwa na furaha,
Kama nikisema, ‘Nitayasahau malalamiko yangu, nitabadili sura ya uso wangu na kutabasamu,’
28 Mimi nitaziogopa huzuni zangu zote kwa sababu nafahamu kuwa hutanihesabu kuwa sina hatia.
bado ninahofia mateso yangu yote, kwa kuwa ninajua hutanihesabu kuwa sina hatia.
29 Nitahukumiwa; kwa nini, basi, nitaabike bure?
Kwa kuwa nimeonekana mwenye hatia, kwa nini basi nitaabishwe bure?
30 Kama najiosha mwenyewe kwa maji ya theluji na kuitakasa mikono yangu na kuwa safi zaidi,
Hata kama ningejiosha kwa sabuni na kutakasa mikono yangu kwa magadi,
31 Mungu atanitumbukiza shimoni, na nguo zangu mwenyewe zitanichukia.
wewe ungenitupa kwenye shimo la utelezi kiasi kwamba hata nguo zangu zingenichukia sana.
32 Kwa kuwa Mungu si mtu, kama mimi, kwamba naweza kumjibu, hata tukaribiane katika hukumu.
“Yeye si mwanadamu kama mimi ili niweze kumjibu, ili kwamba tuweze kushindana naye mahakamani.
33 Hakuna hakimu baina yetu awezaye kuweka mkono wake juu yetu sote.
Laiti angelikuwepo mtu wa kutupatanisha kati yetu, aweke mkono wake juu yetu sote wawili,
34 Hakuna hakimu mwingine ambaye anaweza kuniondolea fimbo ya Mungu, awezaye kuzuia kitisho chake kisinitie hofu. kisha ningesema na nisimuogope.
mtu angeliiondoa fimbo ya Mungu juu yangu, ili utisho wake usiendelee kunitia hofu.
35 Lakini kama mambo yalivyo sasa, sitaweza kufanya hivyo.
Ndipo ningenena naye, bila kumwogopa, lakini kama ilivyo kwangu sasa, sitaweza.