< Ayubu 42 >

1 Kisha Ayubu akamjibu Yahweh na kusema,
约伯回答耶和华说:
2 “Ninajua kwamba unaweza kufanya mambo yote, ya kuwa hakuna kusudi lako linaweza kuzuiliwa.
我知道,你万事都能做; 你的旨意不能拦阻。
3 Ni nani huyo ambaye pasipo maarifa huificha mipango? Kwa kweli nilisema mambo ambayo sikuyaelewa, mambo magumu kwangu kuyafahamu, ambayo juu yake sikujua chochote.
谁用无知的言语使你的旨意隐藏呢? 我所说的是我不明白的; 这些事太奇妙,是我不知道的。
4 Uliniambia, 'Sikiliza sasa, nami nitasema; nitakuuliza mambo, nawe utaniambia.'
求你听我,我要说话; 我问你,求你指示我。
5 Nimekuwa nikikusikia kwa usikivu wa sikio langu, lakini sasa jicho langu linakuona wewe.
我从前风闻有你, 现在亲眼看见你。
6 Basi ninajidharau mwenyewe; ninatubu kwa mavumbi na majivu.”
因此我厌恶自己, 在尘土和炉灰中懊悔。
7 Ilitokea baada ya kuwa amekwisha kusema maneno hata kwa Ayubu, Yahweh alimwambia Elifazi Mtemani, “Ghadhabu yangu imewaka dhidi yako na dhidi ya marafiki zako wawili kwa kuwa hamkusema maneno ya haki juu yangu kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu.
耶和华对约伯说话以后,就对提幔人以利法说:“我的怒气向你和你两个朋友发作,因为你们议论我不如我的仆人约伯说的是。
8 Sasa basi, jitwalieni mafahari saba na mabeberu saba, kisha mmwendee mtumishi wangu Ayubu na mtoe sadaka ya kuteketezwa kwa ajili yenu. Ndipo Mtumishi wangu Ayubu atawaombea ninyi, nami nitayapokea maombi yake, ili kwamba nisiwashughulikie sawasawa na upumbavu wenu. Maana hamkusema mambo ya haki juu yangu, kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu.”
现在你们要取七只公牛,七只公羊,到我仆人约伯那里去,为自己献上燔祭,我的仆人约伯就为你们祈祷。我因悦纳他,就不按你们的愚妄办你们。你们议论我,不如我的仆人约伯说的是。”
9 Basi Elifazi Mtemani, Bildadi Mshuhi na Zofari Mnaamathi walienda na kufanya kama vile Yahweh alivyowaamuru, na Mungu alimtakabali Ayubu.
于是提幔人以利法、书亚人比勒达、拿玛人琐法照着耶和华所吩咐的去行;耶和华就悦纳约伯。
10 Na wakati Ayubu alimpowaombea rafiki zake, Yahweh alirejeza bahati yake. Yahweh alimjalia mara mbili ya kile alichokimiliki hapo awali.
约伯为他的朋友祈祷。耶和华就使约伯从苦境转回,并且耶和华赐给他的比他从前所有的加倍。
11 Ndipo ndugu zake na Ayubu, na wale jamaa zake wote walikuwa wanajuana naye hapo mwanzo, walikuja hapo kwake na kula chakula pamoja naye katika nyumba yake. Waliomboleza pamoja naye na walimfariji kwa ajili majanga yote ambayo Yahweh alikuwa ameyaleta juu yake. Kila mtu alimpa Ayubu kipande cha fedha na pete ya dhahabu.
约伯的弟兄、姊妹,和以先所认识的人都来见他,在他家里一同吃饭;又论到耶和华所降与他的一切灾祸,都为他悲伤安慰他。每人也送他一块银子和一个金环。
12 Yahweh aliubarikiwa mwisho wa maisha ya Ayubu kuliko mwanzo wake; alikuwa na kondoo kumi na nne elfu, ngamia elfu sita, jozi elfu moja, na punda jike elfu moja.
这样,耶和华后来赐福给约伯比先前更多。他有一万四千羊,六千骆驼,一千对牛,一千母驴。
13 Pia alikuwa na wana saba na mabinti watatu.
他也有七个儿子,三个女儿。
14 Binti wa kwanza alimwita Yemima, na wa pili Kezia, na wa tatu Kerenihapuki.
他给长女起名叫耶米玛,次女叫基洗亚,三女叫基连·哈朴。
15 Katika nchi yote hawakupatikana wanawake wazuri kama mabinti wa Ayubu. Baba yao aliwapa urithi miongoni mwa kaka zao.
在那全地的妇女中找不着像约伯的女儿那样美貌。她们的父亲使她们在弟兄中得产业。
16 Baada ya haya, Ayubu aliishi miaka 140; aliwaona wana wake na wana wa wanawe, hata kizazi cha nne.
此后,约伯又活了一百四十年,得见他的儿孙,直到四代。
17 Basi Ayubu alifariki, akiwa mzee na akijawa na siku nyingi.
这样,约伯年纪老迈,日子满足而死。

< Ayubu 42 >