< Ayubu 4 >

1 Kisha Elifazi Mtemani akajibu na kusema,
Then Eliphaz the Temanite answered and said,
2 Kama mtu yeyote akijaribu kuzungumza na wewe, je utakosa ustahimilivu? Lakini ni nani anaweza kujizuia asizungumze?
[If] we essay to commune with thee, wilt thou be grieved? but who can refrain from speaking?
3 Tazama, wewe umewafunza wengi; wewe imeipa nguvu mikono iliyokuwa dhaifu.
Behold, thou hast instructed many, and thou hast strengthened the weak hands.
4 Maneno yako yamemsaidia yeye mwanamme aliyekuwa anaanguka; wewe umeyaimarisha magoti dhaifu.
Thy words have upheld him that was falling, and thou hast strengthened the feeble knees.
5 Lakini sasa matatizo yamekuja kwako, na wewe umechoka; yanakugusa wewe, na wewe umetatizika.
But now it hath come upon thee, and thou faintest; it toucheth thee, and thou art troubled.
6 Je si hofu yako imani yako, na ukamilifu wa njia zako tumaini lako?
[Is] not [this] thy fear, thy confidence, thy hope, and the uprightness of thy ways?
7 Tafakari juu ya hili, tafadhari: ni nani aliyeangamia akiwa hana kosa? Au ni lini watu wakamilifu walikatiliwa mbali?
Remember, I pray thee, who [ever] perished, being innocent? or where were the righteous cut off;
8 Kutokana na vile nilivyoona, wale walimao uovu na kupanda taabu huvuna hayo.
Even as I have seen, they that plow iniquity, and sow wickedness, reap the same.
9 Kwa pumzi ya Mungu huangamia; kwa mlipuko wa hasira zake huteketea.
By the blast of God they perish, and by the breath of his nostrils are they consumed.
10 Kuunguruma kwa simba, sauti ya simba mkali, meno ya simba wadogo - yamevunjika.
The roaring of the lion, and the voice of the fierce lion, and the teeth of the young lions, are broken.
11 Simba mzee huangamia kwa kukosa wahanga; watoto wa simba jike wametawanyiko kila mahali.
The old lion perisheth for lack of prey, and the stout lion's whelps are scattered abroad.
12 Sasa nililetewa kwangu jambo fulani kisiri, na sikio langu likapokea uvumi kuhusu hilo.
Now a thing was secretly brought to me, and my ear received a small sound of it.
13 Kisha yakaja mawazo kupitia ndoto wakati wa usiku, wakati uwaangukiwapo usingizi mzito watu.
In thoughts from the visions of the night, when deep sleep falleth on men.
14 Ilikuwa usiku wakati nilipopatwa hofu na kutetemeka, na mifupa yangu yote ikatikisika.
Fear came upon me, and trembling, which made all my bones to shake.
15 Kisha nafsi ikapita mbele ya uso wangu, na nywele zangu za mwili zilisimama.
Then a spirit passed before my face; the hair of my flesh stood up:
16 Nafsi ilisimama kimya, lakini sikuweza kupambanua sura yake. Umbo lilikuwa mbele ya macho yangu; kulikuwa kimya, nami nikasikia sauti ikisema,
It stood still, but I could not discern its form: an image [was] before my eyes, [there was] silence, and I heard a voice, [saying],
17 “Je binadamu anaweza kuwa mwenye haki zaidi kuliko Mungu? Je mtu anaweza kuwa msafi zaidi kuliko muumba wake?
Shall mortal man be more just than God? shall a man be more pure than his maker?
18 Tazama, kama Mungu hawaamini watumishi wake; kama hulaumu upumbavu wa malaika zake,
Behold, he put no trust in his servants; and his angels he charged with folly:
19 je si zaidi sana ukweli huu kwa wale waishio katika nyumba za udongo, ambao misingi yao ipo katika vumbi, wale waliopondwa mbele ya nondo?
How much less [in] them that dwell in houses of clay, whose foundation [is] in the dust, [who] are crushed before the moth?
20 Kati ya asubuhi na jioni wameangamizwa; wameangamia milele wala bila yeyote kuwatambua.
They are destroyed from morning to evening: they perish for ever without any regarding [it].
21 Je kamba za hema yao hazikung'olewa kati yao? Wanakufa; wanakufa bila hekima.
Doth not their excellence [which is] in them depart? they die, even without wisdom.

< Ayubu 4 >