< Ayubu 35 >

1 Aidha, Elihu aliendelea kusema,
Ndipo Elihu akasema:
2 “Je unadhani hii ni sawa unaposema, 'Haki yangu mbele ya Mungu?
“Je, unadhani hili ni haki? Wewe unasema, ‘Nina haki mbele za Mungu.’
3 Kwa kuwa unauliza, 'Inafaa nini kwangu' na 'Ingekuwa nzuri kwangu kama ningekuwa nimetenda dhambi?'
Bado unamuuliza, ‘Ni faida gani nimepata, na imenifaidi nini kwa kutokutenda dhambi?’
4 Nitakujibu, wewe pamoja na marafiki zako.
“Ningependa nikujibu wewe pamoja na marafiki zako walio pamoja nawe.
5 Tazama juu angani, na ulione; angalia anga, ambalo liko juu sana kuliko wewe.
Tazama juu mbinguni ukaone; yaangalie mawingu yaliyo juu sana juu yako.
6 Kama umetenda dhambi, ni madhara gani huwa unayafanya kwa Mungu? Ikiwa makosa yako yameongezeka zaidi, je huwa unafanya nini kwake?
Je, ukitenda dhambi, inamdhuruje Mungu? Kama dhambi zako zikiwa nyingi, hilo linamfanyia nini Mungu?
7 Kama wewe ni mwenye haki, unaweza kumpa nini? Je atapokea nini mkononi mwako?
Kama wewe ni mwadilifu, unampa nini, au yeye anapokea nini mkononi kwako?
8 Uovu wako waweza kuwaumiza mtu, kama ulivyo wewe ni mtu, na haki yako yaweza kumnufaisha mwana mwingine wa mtu.
Uovu wako unamdhuru tu mtu mwingine kama wewe, nayo haki yako inawafaa wanadamu tu.
9 Watu wanalia kwasababu ya matendo mengi ya unyanyasaji; wanaomba msaada katika mikono ya watu wenye nguvu.
“Wanadamu hulia kwa kulemewa na mateso; huomba msaada kutoka mkono wenye nguvu.
10 Lakini hakuna hata mmoja asemaye, ' Mungu Muumba wangu yuko wapi, ambaye hutoa nyimbo wakati wa usiku,
Lakini hakuna asemaye, ‘Yuko wapi Mungu Muumba wangu, yeye anifanyaye niimbe usiku,
11 ambaye hutufundisha sisi zaidi anavyowafundisha wanyama wa dunia, na ambaye hutufanya sisi kuwa wenye hekima kuliko ndege wa angani?
yeye atufundishaye sisi zaidi kuliko wanyama wa dunia, na kutufanya wenye hekima kuliko ndege wa angani?’
12 Huko wanalia, lakini Mungu hawajibu kwasababu ya kibriu ya watu waovu.
Yeye hajibu wakati watu waliapo kwa sababu ya kiburi cha watu waovu.
13 Kwa hakika Mungu hatasikia kilio cha kipumbavu; Mwenye nguvu wala hatajali.
Naam, Mungu hasikilizi maombi yao ya ubatili; Mwenyezi hayazingatii.
14 Ni kwa namna gani atakujibu ikiwa unasema haumwoni, na ya kwamba hoja yako iko mbele yake, na ya kuwa unamngojea yeye!
Si zaidi sana kwamba hatakusikiliza wewe usemapo humwoni, tena ya kwamba shauri lako liko mbele zake na wewe lazima umngojee,
15 Ni kwa jinsi gani atakujibu kama unasema kwamba hamwadhibu yeyote kwa hasira, na ya kwamba hajishughulishi na kiburi cha watu.
pia zaidi, kwamba hasira yake kamwe haiadhibu wala haangalii uovu hata kidogo?
16 Basi Ayubu hufumbua kinywa chake tu ili kusema upumbavu; huongeza maneno bila maarifa.”
Hivyo Ayubu hufumbua kinywa chake kwa maneno yasiyo na maana; anaongea maneno mengi bila maarifa.”

< Ayubu 35 >