< Ayubu 3 >

1 Baada ya hayo, Ayubu akafunua kinywa chake na kuilani siku aliyozaliwa.
After this, Job opened his mouth and cursed the day of his birth.
2 Akasema,
And this is what he said:
3 “Na ipotelee mbali siku niliyozaliwa mimi, usiku uliosema, 'Mimba ya mtoto wa kiume imetungwa.'
“May the day of my birth perish, and the night it was said, ‘A boy is conceived.’
4 Siku hiyo na iwe giza; Mungu toka juu asiifikilie, wala mwanga usiiangazie.
If only that day had turned to darkness! May God above disregard it; may no light shine upon it.
5 Ishikwe na giza na giza la mauti liwe lake. Wingu na likae juu yake; kila kitu kiifanyacho siku kuwa giza kweli na kiitishe.
May darkness and gloom reclaim it, and a cloud settle over it; may the blackness of the day overwhelm it.
6 Usiku huo, na ukamatwe na giza tororo. Usihesabiwe miongoni mwa siku za mwaka; na usiwekwe katika hesabu ya miezi.
If only darkness had taken that night away! May it not appear among the days of the year; may it never be entered in any of the months.
7 Tazama, usiku huo na uwe tasa; na sauti ya shangwe isiwe ndani yake.
Behold, may that night be barren; may no joyful voice come into it.
8 Na wailani siku hiyo, hao wafahamuo namna ya kumuamsha lewiathani.
May it be cursed by those who curse the day — those prepared to rouse Leviathan.
9 Nyota za mapambazuko yake zitiwe giza. Siku hiyo iutafute mwanga, lakini isiupate; wala makope ya mapambazuko isiyaone,
May its morning stars grow dark; may it wait in vain for daylight; may it not see the breaking of dawn.
10 kwasababu haikuifunga milango ya tumbo la mama yangu, na kwasababu haikunifichia taabu machoni pangu.
For that night did not shut the doors of the womb to hide the sorrow from my eyes.
11 Kwanini si-kufa wakati lipotokeza katika tumbo la uzazi? Kwanini sikuitoa roho yangu hapo mama aliponizaa?
Why did I not perish at birth; why did I not die as I came from the womb?
12 kwanini magoti yake yalinipokea? Kwanini maziwa yake yanipokee hata ninyonye?
Why were there knees to receive me, and breasts that I should be nursed?
13 Kwa sasa ningelikuwa nimelala chini kimya kimya. Ningelala usingizi na kupata pumziko
For now I would be lying down in peace; I would be asleep and at rest
14 pamoja na wafalme na washauri wa dunia, ambao walijijengea makaburi ambayo sasa ni magofu.
with kings and counselors of the earth, who built for themselves cities now in ruins,
15 Au Ningelikuwa nimelala pamoja na wakuu wenye dhahabu, waliozijaza nyumba zao fedha.
or with princes who had gold, who filled their houses with silver.
16 Au pengine ningekuwa sijazaliwa, kama watoto wachanga wasio uona mwanga kabisa.
Or why was I not hidden like a stillborn child, like an infant who never sees daylight?
17 Huko waovu huacha kusumbua; huko waliochoka hupumzika.
There the wicked cease from raging, and there the weary find rest.
18 Huko wafungwa kwa pamoja hupata amani; hawaisikii sauti ya msimamizi wa watumwa.
The captives enjoy their ease; they do not hear the voice of the oppressor.
19 Wote wadogo na watu maarufu wako huko; mtumishi yuko huru kwa bwana wake huko.
Both small and great are there, and the slave is freed from his master.
20 Kwa nini yeye aliye mashakani kupewa mwanga? Kwa nini hao wenye uchungu moyoni kupewa uhai,
Why is light given to the miserable, and life to the bitter of soul,
21 ambao hutamani mauti lakini hawapati; ambao huyachimbulia mauti zaidi ya kutafuta hazina iliyofichika?
who long for death that does not come, and search for it like hidden treasure,
22 Kwa nini kupewa mwanga ambao hushangilia mno na kufurahi walionapo kaburi?
who rejoice and greatly exult when they can find the grave?
23 Kwanini kupewa mwanga mtu ambaye njia zake zimefichika, mtu ambaye Mungu amemzungushia uwa?
Why is life given to a man whose way is hidden, whom God has hedged in?
24 Kwa kuwa kushusha kwangu pumzi kwatokea badala ya kula; kuugua kwangu kumemiminika kama maji.
I sigh when food is put before me, and my groans pour out like water.
25 Maana jambo lile niliogopalo limenipata; nalo linitialo hofu limenijilia.
For the thing I feared has overtaken me, and what I dreaded has befallen me.
26 Mimi sioni raha, sipati utulivu, na sipati pumziko; badala yake huja taabu.”
I am not at ease or quiet; I have no rest, for trouble has come.”

< Ayubu 3 >