< Ayubu 28 >

1 Hakika kuna machimbo ya fedha, wanaposafisha dhahabu.
“Kuna machimbo ya fedha, na mahali dhahabu isafishwapo.
2 Chuma uchimbwa; shaba uyeyushwa kutoka katika jiwe.
Chuma hupatikana ardhini, nayo shaba huyeyushwa kutoka mawe ya madini.
3 Mtu anaondoa giza na kutafuta, katika mpaka wa mbali, mawe hayaonekani na giza totoro.
Mwanadamu hukomesha giza; huyatafuta hadi sehemu iliyo mbali, kwa ajili ya kuchimbua mawe yenye madini katika giza jeusi sana.
4 Huchimba shimo mbali na makazi ya watu, mahali pasipopitwa na mtu. Huning'inia mbali na watu; uharakisha kwenda na kurudi.
Huchimba shimo jembamba mbali na makao ya watu, mahali paliposahaulika na nyayo za wanadamu; mbali na wanadamu huningʼinia na kupembea kwa kamba.
5 Kwa nchi, kizalishwapo chakula, inapinduliwa kama kwa moto.
Ardhi, ambako chakula hutoka, chini hugeuzwa kwa moto;
6 Mawe yake yana johari, na vumbi lake lina dhahabu.
yakuti samawi hutoka katika miamba yake, nalo vumbi lake lina vipande vya dhahabu.
7 Hata ndege mwindaji hapajui, wala jicho la kipanga halijapaona.
Hakuna ndege awindaye aijuaye njia ile iliyofichika, wala hakuna jicho la mwewe lililoiona.
8 Ndege mwenye majivuna hajawai kuiona njia hiyo, wala simba mkali kupita pale.
Wanyama wa porini wanaotamba hawajawahi kupakanyaga, wala simba azungukaye huko.
9 Mtu huchimba mwamba mgumu; hupindua milima katika vyanzo vyake.
Mikono ya mwanadamu hushambulia miamba migumu sana, na kuiacha wazi mizizi ya milima.
10 Huweka njia katika miamba; macho yake pale kila kilicho cha thamani.
Hutoboa shimo refu la kupenya chini kwa chini kwenye miamba; macho yake huona hazina zake zote.
11 Hufunga vyanzo hata wasiondoke; kilichofichika pale hukifunua.
Hutafuta vyanzo vya mito na kuvileta vitu vilivyofichika katika nuru.
12 Hekima itakuwa wapi? Mahali pa ufahamu ni wapi?
“Lakini hekima inaweza kupatikana wapi? Ufahamu unakaa wapi?
13 Mtu hafahamu thamani yake; wala haipatikani katika nchi ya walio hai.
Mwanadamu hatambui thamani yake; haiwezi kupatikana katika nchi ya walio hai.
14 Vilindi vya maji chini ya nchi husema, 'Haiko kwangu'; bahari husema, 'Haipo pamoja nami.'
Kilindi husema, ‘Haiko ndani yangu’; bahari nayo husema, ‘Haiko pamoja nami.’
15 Hainunuliwi kwa dhahabu; wala hailinganishwi na fedha.
Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi kuliko zote, wala thamani yake haiwezi kupimwa kwa fedha.
16 Haiwezi kuthamanishwa na dhahabu ya Ofiri, kwa jiwe jeusi la thamani au johari.
Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu ya Ofiri, kwa shohamu ya thamani kubwa au yakuti samawi ya thamani kubwa.
17 Dhahabu na fuwele hailingani nayo kwa thamani; wala haiwezi kubadilishwa kwa vito vya dhahabu safi.
Dhahabu wala mawe maangavu haviwezi kulinganishwa nayo, wala haiwezi hubadilishwa na vito vya dhahabu.
18 Hailinganishwi na marijani wala yaspi; hakika, thamani ya hekima inapita madini ya rubi.
Marijani na yaspi hazistahili kutajwa; thamani ya hekima ni zaidi ya akiki nyekundu.
19 Topazi ya Ethiopia hailinganishwi nayo; wala kuthamanishwa kwa dhahabu safi.
Yakuti manjano ipatikanayo Kushi haiwezi kulinganishwa nayo, wala haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi.
20 Je hekima inatoka wapi? Mahali pa ufahamu ni wapi?
“Ni wapi basi hekima itokako? Ufahamu hukaa wapi?
21 Hekima imejificha mbali na macho ya viumbe wote na ndege wa angani.
Imefichika machoni pa kila kitu kilicho hai, imesitiriwa hata kwa ndege wa angani.
22 Mauti na uharibifu husema, 'Tumesikia tu tetesi kwa masikio yetu.'
Uharibifu na Mauti husema, ‘Ni uvumi wake tu uliotufikia masikioni mwetu.’
23 Mungu hufahamu njia ya kuipata; anapafahamu ilipo.
Mungu anaifahamu njia ya kuiendea hekima na ndiye peke yake anayefahamu inakokaa,
24 Kwani uona miisho yote ya dunia na huona chini ya mbingu zote.
kwa maana yeye huitazama miisho ya dunia na huona kila kitu chini ya mbingu.
25 Hapo kale, alifanya nguvu za upepo na kuyagawanya maji kwa kipimo.
Alipofanyiza nguvu za upepo na kuyapima maji,
26 Aliiwekea mvua tamko na njia ya radi na munguromo.
alipofanya maagizo kwa ajili ya mvua na njia kwa ajili ya umeme wa radi,
27 Kisha akaiona hekima na kuitangaza; aliianzisha, bila shaka, na kuipima.
ndipo alipoitazama hekima na kuikadiria thamani yake, akaithibitisha na kuihakikisha.
28 Aliwambia watu, 'Tazameni, kumcha Bwana - ni hekima; kuacha uovu ni ufahamu.”
Naye Mungu akamwambia mwanadamu, ‘Kumcha Bwana: hiyo ndiyo hekima, nako kujitenga na uovu ndio ufahamu.’”

< Ayubu 28 >