< Ayubu 27 >

1 Ayubu akaendelea kuoengea na kusema,
And Job adds to lift up his allegory and says:
2 “Kama aishivyo Mungu, ameniondolea haki yangu, Mwenyezi, aliyeyafanya machungu maisha yangu,
“God lives! He turned aside my judgment, And the Mighty—He made my soul bitter.
3 kadili uhai ungalimo ndani yangu uzima wa Mungu upo puani mwangu.
For all the while my breath [is] in me, And the wind of God in my nostrils.
4 Hakika midomo yangu haitanena uovu, wala ulimi wangu kunena uongo.
My lips do not speak perverseness, And my tongue does not utter deceit.
5 Sitakiri kwamba mko sahihi; hata nifapo sitakana uadilifu wangu.
Defilement to me—if I justify you, Until I expire I do not turn aside my integrity from me.
6 Naishikilia haki yangu na sitaiacha; nafsi yangu haitanisuta kadili ninavyoishi.
On my righteousness I have laid hold, And I do not let it go, My heart does not reproach me while I live.
7 Adui yangu na awe kama mwovu; anayeinuka kunyume changu na awe kama asiye haki.
My enemy is as the wicked, And my withstander as the perverse.
8 Kwani tumaini la mwovu ni nini Mungu anapomwondoa, Mungu anapochukua uhai wake?
For what [is] the hope of the profane, When He cuts off? When God casts off his soul?
9 Je Mungu atasikiliza kilio chake tabu zinapompat?
[Does] God hear his cry, When distress comes on him?
10 Je atajifurahisha katika Mwenyezi na kumwita Mungu nyakati zote
Does he delight himself on the Mighty? Call God at all times?
11 Nitawafundisha kuhusu uwezo wa Mungu; sitabatilisha mawazo ya Mwenyezi.
I show you by the hand of God, That which [is] with the Mighty I do not hide.
12 Tazama, ninyi nyote mmeona; kwa nini basi mmeongea yasiyo na maana.
Behold, you—all of you—have seen, And why [is] this—you are altogether vain?
13 Hii ndiyo hatima ya waovu mbele za Mungu, urithi wa mtesaji aupokeao kutoka kwa Mwenyezi.
This [is] the portion of wicked man with God, And the inheritance of terrible ones They receive from the Mighty.
14 Ikiwa watoto wake wataongezeka, ni kwa upanga; uzao wake utakuwa na njaa.
If his sons multiply—a sword [is] for them. And his offspring [are] not satisfied [with] bread.
15 Wanaomsalia watauawa kwa tauni, na wajane wao hawatawaombolezea.
His remnant are buried in death, And his widows do not weep.
16 Japokuwa waovu hurundika mali kama mavumbi,
If he heaps up silver as dust, And prepares clothing as clay,
17 na kukusanya mavazi kama udongo, atakusanya mavazi, lakini mwenye haki atavaa, na wasio na hatia watagawana mali.
He prepares—and the righteous puts [it] on, And the innocent apportions the silver.
18 Hujenga nyumba yake kama buibui, kama kibanda cha muda afanyacho mlinzi.
He has built his house as a moth, And as a shelter a watchman has made.
19 Hulala kitandani akiwa tajiri, lakini hataendelea hivyo; na afumbuapo macho, hana kitu.
He lies down rich, and he is not gathered, He has opened his eyes, and he is not.
20 Vitisho humpata kama maji, dhoruba humwondoa usiku.
Terrors overtake him as waters, By night a whirlwind has stolen him away.
21 Upepo wa mashariki umwondoa, naye huondoka; humwondoa mahali pake.
An east wind takes him up, and he goes, And it frightens him from his place,
22 Humpiga bila kukoma; hujaribu kumnasua katika uwezo wake.
And it casts at him, and does not spare, He diligently flees from its hand.
23 Unampigia makofi kwa kejeli; humwondoa mahali pake.
It claps its hands at him, And it hisses at him from his place.”

< Ayubu 27 >