< Ayubu 25 >
1 Kisha Bilidadi Mshuhi akajibu na kusema,
respondens autem Baldad Suites dixit
2 “Utawala na hofu vipo naye; anaagiza mahali pa juu pake mbinguni.
potestas et terror apud eum est qui facit concordiam in sublimibus suis
3 Je kuna idadi ya majeshi yake? Ni wapi pasipo na nuru yake?
numquid est numerus militum eius et super quem non surget lumen illius
4 Jinsi gani basi mtu awe mwenye haki kama Mungu? Jinsi gani aliyezaliwa na mwanamke awe safi, amekubaliwa naye?
numquid iustificari potest homo conparatus Deo aut apparere mundus natus de muliere
5 Tazama, hata mwezi kwake haungazii; nyota hazikosafi mbele zake.
ecce etiam luna non splendet et stellae non sunt mundae in conspectu eius
6 Ni vipi mtu, aliyemdudu - mwana wa mtu, aliye mdudu!”
quanto magis homo putredo et filius hominis vermis