< Ayubu 16 >

1 Ndipo Ayubu akajibu na kusema,
Kisha Ayubu akajibu:
2 “Mimi nimevisikia vitu hivyo vingi; ninyi nyote ni wafariji wenye kuhuzunisha.
“Nimepata kusikia mambo mengi kama haya, nanyi nyote ni wafariji wenye kutaabisha!
3 Maneno yenye upuuzi daima yanaweza kuwa na mwisho? Nini kimeharibika kwenu kwamba mnajibu kama hivi?
Je, maneno yenu mengi yasiyo na maana hayana mwisho? Mna nini hata mwendelee kushindana kwa maneno?
4 Mimi pia ningeweza kuzungumza kama ninyi mnavyofanya, kama ninyi mngekuwa katika nafasi yangu; Mimi ningekusanya na kuunganisha maneno pamoja dhidi yenu na kutikisa kichwa changu kwenu ninyi katika dhihaka.
Mimi pia ningeweza kuzungumza kama ninyi, kama mngekuwa katika hali yangu; ningeweza kutoa hotuba nzuri dhidi yenu, na kuwatikisia ninyi kichwa changu.
5 Laiti, jinsi gani Mimi ningewatia moyo na midomo yangu! Jinsi gani faraja kutoka midomo yangu ingenga'risha huzuni yenu!
Lakini kinywa changu kingewatia moyo; faraja kutoka midomoni mwangu, ingewaletea nafuu.
6 Ikiwa Mimi ninazungumza, kuomboleza kwangu hakujasikilizwa; Ikiwa nikiendelea katika kuzungumza, jinsi gani mimi ninaidiwa?
“Lakini kama nikisema, maumivu yangu bado hayatulizwi; nami kama nikijizuia, wala hayaondoki.
7 Lakini sasa, Mungu,
Ee Mungu, hakika umenichakaza; umewaangamiza kabisa watu wa nyumbani mwangu wote.
8 wewe umenifanya mimi kuchoka; wewe umeifanya familia yangu yote kuwa ukiwa. Wewe umenifanya mimi kukauka, ambayo yenyewe ni ushuhuda dhidi yangu mimi; kukonda kwa mwili wangu huinuka dhidi yangu, na kunashuhudia dhidi ya macho yangu.
Umenikunjakunja, nalo limekuwa ushahidi; nako kukonda kwangu kumeongezeka sana na kushuhudia dhidi yangu.
9 Mungu amenirarua mimi katika ghadhabu yake na amenitesa mimi; Yeye amenisaga mimi kwa meno yake; Adui yangu amenikazia macho yake juu yangu kama yeye anavyonirarua mimi vipande.
Mungu amenishambulia na kunirarua katika hasira yake, na kunisagia meno yake; adui yangu hunikazia macho yake makali.
10 Watu wameachama na midomo iliyowazi juu yangu; wamenipiga mimi katika shavu kwa kunitukana; wamekusanyika pamoja kinyume changu mimi.
Watu wamenifumbulia vinywa vyao kunidhihaki; hunipiga shavuni mwangu kwa dharau, na kuungana pamoja dhidi yangu.
11 Mungu amenikabidhi mimi juu ya watu wasio mcha Mungu, na kunitupa mimi ndani ya mikono ya watu waovu.
Mungu amenigeuzia kwa watu wabaya, na kunitupa katika makucha ya waovu.
12 Mimi nilikuwa katika wepesi, na yeye amenivunjavunja mimi vipande. Hakika, amenichukua mimi kwa shingo na ameniponda mimi vipande vipande; yeye pia ameniweka mimi juu kama shabaha yake.
Mambo yote yalikuwa mazuri, lakini alinivunjavunja; amenikamata shingo na kuniponda. Amenifanya mimi kuwa shabaha yake;
13 Wapiga upinde wake wote wamenizunguka mimi; Mungu huzikata vipande vipande figo zangu, na haniokoi mimi; yeye humwaga nje nyongo yangu juu ya ardhi.
wapiga upinde wake wananizunguka. Bila huruma, huchoma figo zangu, na kuimwaga nyongo yangu juu ya nchi.
14 yeye hukanyaga kanyaga kupitia ukuta wangu tena na tena; yeye hukimbia juu yangu mimi kama shujaa.
Huniponda tena na tena; hunishambulia kama shujaa wa vita.
15 nguo ya magunia juu ya ngozi yangu; Mimi nimeisukuma kwa nguvu pembe yangu ndani ya ardhi.
“Nimejishonea nguo ya gunia juu ya mwili wangu nami nimekizika kipaji cha uso wangu kwenye vumbi.
16 Uso wangu ni mwekundu na kuomboleza; juu ya ngozi inayofunika macho kuna kivuli cha mauti
Uso wangu umekuwa mwekundu kwa kulia, macho yangu yamepigwa na giza kuu.
17 ingawa hakuna dhuluma katika mikono yangu, na kuomba kwangu ni safi.
Hata hivyo mikono yangu haijafanya jeuri, na maombi yangu ni safi.
18 Nchi, haifuniki juu damu yangu mimi; acha kulia kwangu kuwe hakuna mahali pa kupumzika.
“Ee nchi, usiifunike damu yangu, nacho kilio changu kisinyamazishwe kamwe.
19 Hata sasa, tazama, ushuhuda wangu uko mbinguni; yeye ambaye ashuhudiaye kwa ajili yangu mimi yuko juu.
Hata sasa shahidi wangu yuko mbinguni; wakili wangu yuko juu.
20 Rafiki zangu wananicheka kwa dharau, lakini jicho langu linamwaga machozi kwa Mungu.
Mwombezi wangu ni rafiki yangu macho yangu yamwagapo machozi kwa Mungu;
21 Mimi ninaomba ule ushuhuda ulioko mbinguni kumtetea mtu huyu na Mungu kama mwanadamu afanyavyo na jirani yake.
kwa niaba ya mtu anamsihi Mungu kama mtu anavyosihi kwa ajili ya rafiki yake.
22 Kwa maana wakati miaka michache itakapokuwa imepita, Mimi nitakwenda mahali ambapo mimi sitaweza kurudi.
“Ni miaka michache tu itapita kabla sijaenda safari ambayo sitarudi.

< Ayubu 16 >