< Ayubu 15 >
1 Ndipo Elifazi Mtemani alijibu na kusema,
Kisha Elifazi Mtemani akajibu:
2 Mtu mwenye hekima anapaswa kujibu kwa maarifa yasiyofaa na kujijaza mwenyewe na upepo wa mashariki?
“Je, mtu mwenye hekima hujibu kwa mawazo matupu, au kujaza tumbo lake kwa upepo wenye joto wa mashariki?
3 Anapaswa kuhojiana na mazungumzo yasiyo na faida au na hotuba ambazo kwa hizo yeye hawezi kufanya mema?
Je, aweza kubishana juu ya maneno yasiyofaa, kwa hotuba zisizo na maana?
4 Dhahiri, wewe wafifisha heshima ya Mungu; Wewe wazuia heshima kwa yeye,
Lakini unadhoofisha hata uchaji wa Mungu na kuzuia ibada mbele za Mungu.
5 kwa maana uovu wako hufundisha midomo yako; Wewe wachagua kuwa na ulimi wa mtu mwenye hila.
Dhambi yako inasukuma kinywa chako, nawe umechagua ulimi wa hila.
6 Mdomo wako mwenyewe hukukukumu wewe, siyo wangu; hakika, midomo yako mwenyewe hushuhudia dhidi yako wewe.
Kinywa chako mwenyewe kinakuhukumu, wala si changu; midomo yako mwenyewe inashuhudia dhidi yako.
7 Je, wewe ni mwanadamu wa kwanza ambaye aliyezaliwa? Wewe ulikuwepo kabla ya vilima kuwepo?
“Je, wewe ni mtu wa kwanza kuzaliwa? Ulizaliwa kabla ya vilima?
8 Wewe Umewahi kusikia maarifa ya siri ya Mungu? Je, wewe wajihesabia mwenye hekima wewe mwenyewe?
Je, wewe husikiliza mashauri ya siri ya Mungu? Je, wewe unaizuia hekima iwe yako mwenyewe?
9 Ni kitu gani unachokifahamu wewe ambacho sisi hatukijui? Ni kitu gani unachokifahamu wewe ambacho hakiko katika sisi?
Wewe unajua kitu gani tusichokijua sisi? Unafahamu kitu gani tusichokifahamu sisi?
10 Pamoja nasi wapo pia wenye mvi na watu wazee sana ambao ni wazee zaidi kuliko baba yako.
Wale wenye mvi na wazee wako upande wetu, watu ambao ni wazee hata kuliko baba yako.
11 Je, faraja ya Mungu ni ndogo sana kwako, maneno ambayo ni ya upole dhidi yako wewe?
Je, faraja za Mungu hazikutoshi, au maneno yaliyosemwa kwako kwa upole si kitu?
12 Kwa nini moyo wako wewe unakupeleka mbali? Kwa nini macho yako yananga'ra,
Kwa nini moyo wako unakudanganya, na kwa nini macho yako yanangʼaa,
13 ili ya kwamba kuirejesha roho yako kwa Mungu na kuyatoa maneno hayo kutoka katika mdomo wako?
ili kwamba upate kutoa hasira yako dhidi ya Mungu, na kumwaga maneno kama hayo kutoka kinywani mwako?
14 Je, mwanadamu yeye ni nini kwamba yeye anapaswa kuwa safi? Yeye mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke ni nini kwamba yeye anapaswa awe mwenye haki?
“Mwanadamu ni kitu gani, hata aweze kuwa safi, au yeye aliyezaliwa na mwanamke, hata aweze kuwa mwadilifu?
15 Tazama, Mungu haweki tumaini lake hata kwa mmoja wake aliye mtakatifu; Hakika, mbingu haziko safi machoni pake yeye;
Kama Mungu hawaamini watakatifu wake, kama hata mbingu zenyewe si safi machoni pake,
16 jinsi gani asivyo safi ni mmoja aliye mbaya na mla rushwa, mtu ambaye hunywa uovu kama maji!
sembuse mwanadamu ambaye ni mwovu na mpotovu, ambaye hunywa uovu kama anywavyo maji!
17 Mimi nitakuonyesha wewe; Nisikilize mimi; Mimi nitakutangazia wewe vitu ambavyo nimeviona,
“Nisikilize mimi nami nitakueleza, acha nikuambie yale niliyoyaona,
18 vitu ambavyo watu wenye hekima wamepita chini yake kutoka kwa baba zao, vile vitu ambavyo mababu zao hawakuvificha.
ambayo watu wenye hekima wameyanena, bila kuficha lolote walilopokea toka kwa baba zao
19 Hawa walikuwa mababu zao, ambao kwao pekee nchi walipewa, na miongoni mwao hakuna mgeni aliyepita.
(wakati ambao wao peke yao ndio walipewa nchi, hakuna mgeni aliyepita miongoni mwao):
20 Mtu mwovu hupitia katika maumivu siku zake zote, idadi ya miaka iliyowekwa juu kwa mtesaji kuteseka.
Mtu mwovu siku zake zote hupata mateso, miaka yote aliwekewa mkorofi.
21 Sauti ya vitisho katika masikio yake; pindi yeye yuko katika kufanikiwa, mharibu atakuja juu yake yeye.
Sauti za kutisha hujaa masikioni mwake; katika kufanikiwa kwake, wanyangʼanyi humshambulia.
22 Yeye hafikiri kwamba yeye atarudi kutoka katika giza; Upanga humngojea yeye.
Hukata tamaa kuokoka gizani; amewekwa kwa ajili ya upanga.
23 Yeye huenda sehemu mbali mbali kwa ajili ya mkate, akisema, 'Kiko wapi? ' Yeye anatambua kuwa siku ya giza iko mkononi.
Hutangatanga, akitafuta chakula; anajua kwamba siku ya giza iko karibu.
24 Dhiki na mateso makali humfanya aogope; wao hushinda dhidi yake yeye, kama mfalme tayari kwa vita.
Taabu na maumivu makuu vinamtia hofu; humshinda kama mfalme aliye tayari kwa vita,
25 Kwa sababu yeye ameunyosha mkono wake dhidi ya Mungu na ameishi kwa kiburi dhidi ya aliye mkuu,
kwa sababu amemkunjia Mungu ngumi yake na kujigamba dhidi ya Mwenyezi,
26 huyu mtu mwovu hukimbia kwa Mungu na shingo ngumu, kwa vifundo vikubwa vya ngao.
kwa kiburi akishambulia dhidi ya Mungu akiwa na ngao nene, iliyo imara.
27 Hii ni kweli, hata ingawa yeye amefunika uso wake kwa mafuta yake na amekusanya mafuta juu ya viuno vyake,
“Ingawa uso wake umefunikwa na mafuta kwa unene na kiuno chake kimevimba kwa kunenepa,
28 na ameishi katika miji yenye ukiwa; katika nyumba ambazo hakuna mwanadamu anayeishi humo sasa na ambazo zilikuwa tayari kuwa magofu.
ataishi katika miji ya magofu, na katika nyumba ambazo haziishi mwanadamu yeyote, nyumba zinazokuwa vifusi.
29 Yeye hatakuwa tajiri; utajiri wake yeye hautadumu; hata kivuli chake hakitadumu katika nchi.
Hatatajirika tena, nao utajiri wake hautadumu, wala mali zake hazitakuwa nyingi juu ya nchi.
30 Yeye hatatoka nje ya giza; mwali wa moto utakausha matawi yake; katika pumzi ya kinywa cha Mungu yeye ataenda zake.
Hatatoka gizani; mwali wa moto utanyausha machipukizi yake, nayo pumzi ya kinywa cha Mungu itamwondolea mbali.
31 Mwacheni yeye asitumaini katika vitu visivyofanya kazi, akijidanganya yeye mwenyewe; maana upuuzi utakuwa mshahara wake yeye.
Asijidanganye mwenyewe kutumainia ubatili, kwa kuwa hatapata malipo yoyote.
32 Itatokea kabla ya wakati wake yeye atapaswa kufa; tawi lake halitakuwa kijani.
Atakuwa amelipwa kikamilifu kabla ya wakati wake, nayo matawi yake hayatastawi.
33 Yeye atazipukutisha zabibu zake zisizovunwa kama mzabibu; yeye atayaondoa maua yake kama mti wa mzeituni.
Atafanana na mzabibu uliopukutishwa matunda yake kabla hayajaiva, kama mzeituni unaodondosha maua yake.
34 Kwa maana msaada wa watu wasiomcha Mungu utakuwa tasa; moto utateketeza hema za rushwa.
Kwa kuwa jamii ya wasiomcha Mungu watakuwa tasa, nao moto utateketeza hema za wale wanaopenda rushwa.
35 Wao wanabeba mimba yenye ubaya na kuzaa uovu; tumbo lao hutunga mimba ya udanganifu.
Hutunga mimba ya madhara na kuzaa uovu; matumbo yao huumba udanganyifu.”