< Ayubu 14 >

1 Mwanadamu, ambaye amezaliwa na mwanamke, huishi siku chache tu na amejaa mahangaiko.
“Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake ni chache nazo zimejaa taabu.
2 Yeye huchanua kutoka katika ardhi kama ua na kukatwa chini; yeye hukimbia kama kivuli na hawezi kudumu.
Huchanua kama ua kisha hunyauka; huwa kama kivuli kipitacho upesi, wala hadumu.
3 Je, wewe unatazama chochote katika hivi? Mnanileta mimi hukumuni pamoja nanyi?
Je, unamwekea jicho lako mtu kama huyo? Je, utamleta mbele yako katika hukumu?
4 Ni nani anayeweza kukileta kitu safi kutoka katika kitu kichafu? Hakuna awaye yote.
Ni nani awezaye kutoa kitu safi kutoka kitu najisi? Hakuna awezaye!
5 Siku za mwanadamu zimeamriwa. Idadi ya miezi yake unayo wewe; umekiweka kikomo chake ambacho hawezi kukivuka.
Siku za mwanadamu zimewekewa mpaka; umekwisha kutangaza idadi ya miezi yake na kuweka mpaka ambao hawezi kuuvuka.
6 Tazama mbali kutoka kwake kwamba yeye aweze kupumzika, ili kwamba aweze kufurahia siku yake kama mtu aliyekodishwa kama yeye anaweza kufanya hivyo.
Hivyo angalia mbali umwache, hadi awe amekamilisha muda wake kama mtu aliyeajiriwa.
7 Kunaweza kuwa na tumaini kwa mti; kama ukikatwa chini, unaweza kuchipua tena, hivyo chipukizi lake halitapotea.
“Kwa maana lipo tumaini kwa mti; kama ukikatwa utachipuka tena, nayo machipukizi yake mapya hayatakoma.
8 Japokuwa mizizi yake inakua na kuzeeka katika ardhi, na shina lake kufa katika udongo,
Mizizi yake yaweza kuchakaa ardhini na kisiki chake kufa udongoni,
9 hata kama bado lina harufu ya maji pekee, litachipua tena na kutoa nje matawi kama mche.
lakini kwa kupata dalili ya maji utachipua na kutoa machipukizi kama mche.
10 Lakini mwanadamu hufa; yeye huwa dhaifu; haswaa, mwanadamu hukoma kupumua, na tena yuko wapi yeye?
Lakini mwanadamu hufa, na huo ndio mwisho wake; hutoa pumzi ya mwisho, naye hayuko tena!
11 Kama maji yanavyopotea kutoka ziwani, na kama vile mto upotezavyo maji na kukauka,
Kama vile maji yatowekavyo katika bahari, au mkondo wa mto ukaushwavyo na kuwa mkavu,
12 vivyo hivyo watu hulala chini na hawaamki tena. Mpaka pale mbingu zitakapokuwa hazipo tena, hawataamka wala kuamshwa kutoka katika kulala kwao.
ndivyo mwanadamu alalavyo chini asiamke; hadi mbingu zitakapokuwa hazipo tena, wanadamu hawataamka au kuamshwa kutoka kwenye usingizi wao.
13 Laiti, kwamba ungenificha mimi mbali katika kuzimu mbali kutoka katika mahangaiko, na kwamba ungenitunza mimi katika siri hadi hasira yake imalizike, kwamba ungeniwekea mimi muda maalumu wa kukaa huko na kisha kuniita mimi katika fahamu! (Sheol h7585)
“Laiti kama ungenificha kaburini, na kunisitiri hadi hasira yako ipite! Laiti ungeniwekea wakati, na kisha ukanikumbuka! (Sheol h7585)
14 Ikiwa mwanadamu akifa, yeye ataishi tena? Ikiwa hivyo, ningependa kusubiri kule muda wangu wote wa kuharibika mpaka kufunguliwa kwangu kutakapokuja.
Je, kama mtu akifa, aweza kuishi tena? Siku zote za kazi zangu ngumu nitangojea kufanywa upya kwangu.
15 Wewe ungeita, na mimi ningekujibu wewe. Wewe ungekuwa na shauku ya kazi ya mikono yako.
Utaniita nami nitakuitika; utakionea shauku kiumbe ambacho mikono yako ilikiumba.
16 Wewe ungehesabu na kutunza nyayo zangu; Wewe usingejali kumbukumbu ya dhambi yangu.
Hakika ndipo utakapozihesabu hatua zangu, lakini hutazifuatia dhambi zangu.
17 Uovu wangu ungetiwa muhuri katika mkoba; wewe ungeufunga uovu wangu.
Makosa yangu yatafungiwa kwa lakiri kwenye mfuko, nawe utazifunika dhambi zangu.
18 Lakini hata milima huanguka na kuwa si chochote; hata miamba huhamishwa kutoka mahali pake;
“Lakini kama mlima umomonyokavyo na kufikichika na kama vile mwamba uondolewavyo mahali pake,
19 maji yaliyokuwa chini ya mawe; kufurika kwake huondoa mbali mavumbi ya nchi. Kama hivi, ninyi mnavyoharibu matumaini ya mwanadamu.
kama maji yamalizavyo mawe, na mafuriko yachukuavyo udongo, ndivyo unavyoharibu tegemeo la mwanadamu.
20 Ninyi daima humshinda yeye, na yeye hupita mbali; Ninyi mnabadilisha uso wake na kumtuma yeye mbali kufa.
Humshinda mara moja kwa daima, naye hutoweka; waibadilisha sura yake na kumwondoa.
21 Kama watoto wake wa kiume ni wa kuheshimiwa, yeye, hatambui hicho; na kama wakishushwa chini, yeye haoni hicho.
Kama wanawe wakipewa heshima, yeye hafahamu; kama wakidharauliwa, yeye haoni.
22 Yeye hujisikia tu maumivu ya mwili wake mwenyewe, na hujiombolezea yeye mwenyewe.
Yeye hasikii kingine isipokuwa maumivu ya mwili wake mwenyewe, naye huomboleza kwa ajili yake mwenyewe.”

< Ayubu 14 >