< Ayubu 10 >

1 Nimechoka na maisha yangu; Nitanena wazi manung'uniko yangu; nitasema kwa uchungu wa roho yangu.
“I loathe my own life; I will express my complaint and speak in the bitterness of my soul.
2 Nitamwambia Mungu, 'Usinihukumie makosa; nionyeshe sababu za wewe kunilaumu mimi. Je
I will say to God: Do not condemn me! Let me know why You prosecute me.
3 ni vizuri kwako wewe kunionea mimi, kudharau kazi ya mikono yako wakati unafurahia juu ya mipango ya waovu?
Does it please You to oppress me, to reject the work of Your hands and favor the schemes of the wicked?
4 Je wewe una macho ya kimwili? Je wewe unaona kama mtu aonavyo?
Do You have eyes of flesh? Do You see as man sees?
5 Je siku zako ni kama siku za wanadamu au miaka yako ni kama miaka ya watu,
Are Your days like those of a mortal, or Your years like those of a man,
6 hata ukauliza habari za uovu wangu na kuitafuta dhambi yangu,
that You should seek my iniquity and search out my sin—
7 ingawa wewe wafahamu mimi sina kosa na hapana mwingine awezaye kuniokoa mimi na mkono wako?
though You know that I am not guilty, and there is no deliverance from Your hand?
8 Mikono yako imeniumba na kunifinyanga kwa wakati mmoja nawe kunizunguka, hata hivyo unaniangamiza.
Your hands shaped me and altogether formed me. Would You now turn and destroy me?
9 Kumbuka, nakuomba, ulivyonifinyanga kama vile udongo; je utanirudisha mavumbini tena?
Please remember that You molded me like clay. Would You now return me to dust?
10 Je wewe hukunimimina kama maziwa na kunigandisha mfano wa jibini?
Did You not pour me out like milk, and curdle me like cheese?
11 Umenivika ngozi na nyama na kuniunganisha pamoja kwa mifupa na misuli.
You clothed me with skin and flesh, and knit me together with bones and sinews.
12 Wewe umenizawadia mimi uhai na ahadi ya upendeleo na usaidizi wako umeilinda roho yangu.
You have granted me life and loving devotion, and Your care has preserved my spirit.
13 Hata hivyo mambo haya uliyaficha moyoni mwako - nafahamu kwamba hivi ndivyo ufikirivyo:
Yet You concealed these things in Your heart, and I know that this was in Your mind:
14 kuwa kama nimefanya dhambi, wewe utaizingatia; hutaniachilia na uovu wangu.
If I sinned, You would take note, and would not acquit me of my iniquity.
15 Kama mimi ni muovu, ole wangu; hata kama ni mwenye haki, sitaweza kuinua kichwa changu, kwa kuwa nimejaa aibu na kuyaangalia mateso yangu.
If I am guilty, woe to me! And even if I am righteous, I cannot lift my head. I am full of shame and aware of my affliction.
16 Kama kichwa changu kikijiinua chenyewe, waniwinda kama simba; tena wajionyesha mwenyewe kuwa ni mwenye nguvu kwangu.
Should I hold my head high, You would hunt me like a lion, and again display Your power against me.
17 Wewe unaleta mashahidi wapya dhidi yangu na kuzidisha hasira zako dhidi yangu; wanishambulia na majeshi mapya.
You produce new witnesses against me and multiply Your anger toward me. Hardships assault me in wave after wave.
18 Kwa nini, basi, ulinitoa tumboni? Natamani ningekata roho na ili jicho lolote lisinione.
Why then did You bring me from the womb? Oh, that I had died, and no eye had seen me!
19 Ningelikuwa kama asiyekuwepo; ningelichukuliwa kutoka tumboni mpaka kaburini.
If only I had never come to be, but had been carried from the womb to the grave.
20 Je si siku zangu pekee ni chache? Acha basi, usinisumbue, ili kwamba nipate kupumzika kidogo
Are my days not few? Withdraw from me, that I may have a little comfort,
21 kabla sijaenda huko ambako sitarudi, kwenye nchi ya giza na kivuli cha mauti,
before I go—never to return— to a land of darkness and gloom,
22 ni nchi ya giza kama usiku wa manane, nchi ya kivuli cha mauti, isiyokuwa na mpangilio, ambayo nuru yake ni kama usiku wa manane.'”
to a land of utter darkness, of deep shadow and disorder, where even the light is like darkness.”

< Ayubu 10 >