< Yeremia 9 >
1 Kama kichwa changu kingetoa maji, na macho yangu kuwa chemichemi ya machozi! kwa kuwa natamani kulia usiku na mchana kwa ajili yao waliokuwa binti za watu wangu ambao wameuawa.
但愿我的头为水, 我的眼为泪的泉源, 我好为我百姓中被杀的人昼夜哭泣。
2 Kama mtu anganipatia mahali pa wasafiri nyikani ili nikae, mahali ambapo ningeenda kuwatelekeza watu wangu. Kama ningewaacha, kwa kuwa wote ni wazinzi, kundi la wenye hiana!
惟愿我在旷野有行路人住宿之处, 使我可以离开我的民出去; 因他们都是行奸淫的, 是行诡诈的一党。
3 asema BWANA, “Huupinda ulimi wao kana kwamba ni upinde ili wapate kuongea uongo, lakini si kwa uamiinifu wao kwamba wanapata nguvu duniani. Wanatoka uovu mmoja hadi mwiingine. Hawanijui mimi.”
他们弯起舌头像弓一样, 为要说谎话。 他们在国中增长势力, 不是为行诚实, 乃是恶上加恶, 并不认识我。 这是耶和华说的。
4 Kila mmoja wenu, awe mlinzi wa jirani yake na usimwamini hata ndugu yako yeyote. kwa kuwa kila ndugu ni mwongo,
你们各人当谨防邻舍, 不可信靠弟兄; 因为弟兄尽行欺骗, 邻舍都往来谗谤人。
5 kila jirani anatembea akilaghai. Kila mwanamume anakejeli jirani yake na haongei ukweli. Ndimi zao hufundisha vitu vya uongo. Hujidhofisha ili kusema uongo.
他们各人欺哄邻舍,不说真话; 他们教舌头学习说谎, 劳劳碌碌地作孽。
6 Makazi yenu yako kati ya udanganyifu; kwa uongo wao wanakataa kunitambua mimi. Asema BWANA.”
你的住处在诡诈的人中; 他们因行诡诈,不肯认识我。 这是耶和华说的。
7 Kwa hiyo BWANA wa majeshi asema hivi, “Tazama, Niko tayari kuwajaribu. Nitawajaribu nione. Jinsi gani niwezavyo kufanya kwa binti za watu wangu?
所以万军之耶和华如此说: 看哪,我要将他们熔化熬炼; 不然,我因我百姓的罪该怎样行呢?
8 Ndimi zao ni mishale iliyochongoka; huongea vitu vya uasi. Kwa midomo yao wanatangaza amani pamoja na jirani zao, lakini katika mioyo yao wanadanganya wakati wa kusubri.
他们的舌头是毒箭,说话诡诈; 人与邻舍口说和平话, 心却谋害他。
9 Kwa nini nisiwaadhibu kwa sababu ya mambo haya - asema BWANA na kwa nini nisijilipizie kisasi kwa taifa ambalo liko kama hili?
耶和华说:我岂不因这些事讨他们的罪呢? 岂不报复这样的国民呢?
10 Nitaimba wimbo wa kuomboleza na kulia kwa ajili ya milima, na wimbo wa mazishi utaimbwa nyikani. Kwa kuwa wameteketezwa kwa hiyo hakuna anAyeweza kupita kati kati yao. Hawatasikia sauti ya ng'ombe yeyote. Ndege wa angani na wanyama wote wamekimbia.
我要为山岭哭泣悲哀, 为旷野的草场扬声哀号; 因为都已干焦,甚至无人经过。 人也听不见牲畜鸣叫, 空中的飞鸟和地上的野兽都已逃去。
11 Kwa hiyo nitaigeuza Yerusalemu kuwa vifusi vya ukiwa, maficho ya mbweha. Nitaifanya miji ya Yuda kuwa miji iliyoharibiwa isiyokaliwa na watu.
我必使耶路撒冷变为乱堆,为野狗的住处, 也必使犹大的城邑变为荒场,无人居住。
12 Ni nani mwenye hekima anayeyaelewa haya? Je, kinywa cha BWANA kinatangaza nini kwake ili aweze kuyasema? Kwa nini nchi imepotea? Imeharibiwa kama jangwa, ambapo hakuna apitaye kati kati yake.
谁是智慧人,可以明白这事?耶和华的口向谁说过,使他可以传说?遍地为何灭亡,干焦好像旷野,甚至无人经过呢?
13 BWANA asema, “Ni kwa sababu wameziacha sheria zake ambazo niliwatengenezea, kwa sababu hawaisikilizi sauti yangu au kuishi kwa kuifuta.
耶和华说:“因为这百姓离弃我在他们面前所设立的律法,没有遵行,也没有听从我的话;
14 Ni kwa sababu wameishi kwa ushupavu wa mioyo yao na wamewafuata Mabaali kama baba zao walivyowafundisha kufanya.
只随从自己顽梗的心行事,照他们列祖所教训的随从众巴力。”
15 Kwa hiyo BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, 'Tazama, Ninataka kuwafanya hawa watu wale pakanga na kunywa maji ya sumu.
所以万军之耶和华—以色列的 神如此说:“看哪,我必将茵 给这百姓吃,又将苦胆水给他们喝。
16 Ndipo nitakapowasambaza kati ya mataifa ambayo hawajayajua, wao wala mababu zao. Nitatuma upanga kwa ajili yao mpaka nimewaangamiza wote kabisa.'”
我要把他们散在列邦中,就是他们和他们列祖素不认识的列邦。我也要使刀剑追杀他们,直到将他们灭尽。”
17 BWANA wa majeshi asema hivi, “Yafikirini haya: Waiteni waliaji; waje. Tumeni wanawake wenye taaluma ya kuomboleza, waje.
万军之耶和华如此说: 你们应当思想, 将善唱哀歌的妇女召来, 又打发人召善哭的妇女来,
18 Waje haraka waimbe wimbo wa maombolezo juu yetu, ili macho yetu yatokwe na machozi na kope zetu zibubujikwe na maji.
叫她们速速为我们举哀, 使我们眼泪汪汪, 使我们的眼皮涌出水来。
19 Kwa kuwa sauti ya kilio imesikika Sayuni, 'Jinsi tulivyoharibiwa. Tumeaibishwa sana, kwa kuwa tumeitelekeza nchi tangu walIpoangusha nyumba zetu.'
因为听见哀声出于锡安,说: 我们怎样败落了! 我们大大地惭愧! 我们撇下地土; 人也拆毁了我们的房屋。
20 Kwa hiyo ninyi wanawake, sikieni neno la BWANA; zingatieni ujumbe unaokuja toka kinywani mwake. Kisha wafundisheni binti zenu wimbo wa maombolezo, na kila mwanamke wa jirani wimbo wa kilio.
妇女们哪,你们当听耶和华的话, 领受他口中的言语; 又当教导你们的儿女举哀, 各人教导邻舍唱哀歌。
21 Kwa kuwa vifo vimekuja kupitia dirishani; vinaelekea mahali petu. Vinawaharibu watoto kutoka nje na vijana kwenye viwanja vya miji.
因为死亡上来, 进了我们的窗户, 入了我们的宫殿; 要从外边剪除孩童, 从街上剪除少年人。
22 Uyatangaze haya, 'Asema BWANA - mizoga ya wanaume itaanguka kama mavi kwenye mashamba na kama mabua baada ya mvunaji, na hapatakuwa na mtu wa kuyakusanya.'”
你当说,耶和华如此说: 人的尸首必倒在田野像粪土, 又像收割的人遗落的一把禾稼, 无人收取。
23 BWANA asema hivi, “Usimwache mtu mwenye busara ajivune kwa ajili ya hekima yake, au shujaa kwa sababu ya uwezo wake. Usimwache mtu tajiri ajivunie utajiri wake.
耶和华如此说:“智慧人不要因他的智慧夸口,勇士不要因他的勇力夸口,财主不要因他的财物夸口。
24 Kwa kuwa kama mtu atajivunia chochote kile, acha iwe hivi, yeye awe na busra na kunijua mimi. Kwa kuwa mimi ni BWANA, atendaye katika agano la wema, haki, na hukumu duniani. Ni katika hili kwamba ninafurahia- asema BWANA.
夸口的却因他有聪明,认识我是耶和华,又知道我喜悦在世上施行慈爱、公平,和公义,以此夸口。这是耶和华说的。”
25 Tazama, siku zaja - asema BWANA wakati nitakapowaadhibu wote ambao hawajatahiriwa ambao wako hivyo hivyo katika miili yao.
耶和华说:“看哪,日子将到,我要刑罚一切受过割礼、心却未受割礼的,
26 Nitaiadhibu Misri na Yuda, Edomu, watu wa Amoni, Moabu, na watu wote wanaonyoa denge. Kwani mataifa yote haya hayajatahiriwa, na nyumba yote ya Israeli ina moyo ambao haujatahiriwa.”
就是埃及、犹大、以东、亚扪人、摩押人,和一切住在旷野剃周围头发的;因为列国人都没有受割礼,以色列人心中也没有受割礼。”