< Yeremia 52 >
1 Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja alipoanza kutawala; akatawala miaka kumi na mmoja huko Yerusalemu. Jina la mamaye lilikuwa Hamutali; alikuwa binti Yeremia wa Libna.
Sédécias avait vingt et un ans quand il monta sur le trône, et il régna onze ans à Jérusalem, et sa mère s'appelait Amitaal, et elle était fille de Jérémie, de Lobna.
2 Akafanya maovu machoni pa Yahwe; akafanya kila alichokifanya Yehoyakimu.
3 Kwa hasira ya Yahwe, matukio haya yote yalitukia Yerusalemu na Yuda, hata alipowatoa mbele yake mwenyewe. Kisha Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli.
4 Ikawa katika mwaka wa tisa wa utawala wa mfalme Sedeki, katika mwezi wa kumi, na siku ya kumi ya mwezi huo, Nebukadneza, mfalme wa Babeli, alikuja na jeshi lake lote dhidi ya Yerusalem. Wakapiga kambi kuukabili, nao wakajenga ukuta wa kuusuria kuuzunguka.
Dans la neuvième année de son règne, le neuvième année, le dixième jour du mois, Nabuchodonosor, roi de Babylone, vint avec toutes ses forces vers Jérusalem, et ils l'entourèrent de retranchements, et ils bâtirent alentour un mur en grandes pierres de taille.
5 Hivyo mji ukausuriwa mpaka mwaka wa kumi na moja wa utawala wa mfalme Sedekia.
Et la ville fut investie jusqu'à la onzième année du règne de Sédécias,
6 Katika mwezi wa nne, siku ya tisa ya mwaka huo, njaa ikawa kali sana mjini hata hakukuwa na chakula kwa watu wa nchi.
Jusqu'au neuvième jour du mois; et alors la famine prévalut dans la cité, et il n'y avait plus de pain pour le peuple de la terre.
7 Kisha mji ukatobolewa, na wapiganaji wote wakakimbia nje ya mji wakati wa usiku kwa njia ya lango lililokuwa kati ya kuta mbili, kwa bustani ya mfalme, japokuwa Wakaldayo walikuwa wameuzunguka mji. Hivyo wakaenda kwa njia ya Araba.
Une brèche fut faite aux murailles; les hommes de guerre sortirent de nuit par le chemin de la porte, entre les remparts et les forts avancés qu'on avait élevés près du jardin du roi; et les Chaldéens entouraient le reste de la ville, et les fugitifs prirent la route d'Araba.
8 Lakini jeshi la Wakaldayo likamfuatia mfalme na kumpata Sedekia katika tambarare za bonde la Mto Yordani karibu na Yeriko. Jeshi lote lilikuwa limetawanyika mbali naye.
Et l'armée des Chaldéens les poursuivit, et ils prirent le roi auprès de Jéricho, et tous ses serviteurs s'étaient dispersés loin de lui.
9 Wakamkamata mfalme na kumleta hadi kwa mfalme wa Babeli huko Ribla katika nchi ya Hamathi, alipotoa hukumu juu yake.
Les Chaldéens firent donc le roi captif et ils le menèrent au roi de Babylone, à Déblatha, et Nabuchodonosor prononça contre lui son arrêt.
10 Mfalme wa Babeli akawachinja wana wa Sedekia mbele ya macho yake, na huko Ribla akawachinja viongozi wote wa Yuda.
Et il égorgea les fils de Sédécias sous ses yeux, et il égorgea tous les princes de Juda en Déblatha.
11 Kisha akayaondoa macho ya Sedekia, akamfunga katika vifungo vya shaba, na kumleta Babeli. Mfalme wa Babeli akamweka kifungoni hata siku ya kufa kwake.
Et il arracha les yeux de Sédécias; puis, après l'avoir chargé de chaînes, il l'emmena à Babylone; là il le mit avec les esclaves qui tournaient la meule, jusqu'au jour où il mourut.
12 Basi mwezi wa tano, siku ya kumi ya mwezi, ambao ulikuwa mwaka wa kumi na tisa wa utawala wa mfalme Nebukadneza, mfalme wa Babeli, Nebuzaradani akaja Yerusalemu. Alikuwa jemedari wa walinzi wa mfalme na mtumishi wa mfalme wa Babeli.
Et le cinquième mois, le sixième jour du mois, Nabuzardan, chef des cuisines, qui se tenait devant le roi de Babylone, marcha sur Jérusalem.
13 Akaiteketeza nyumba ya Yahwe, kasiri, na nyumba zote za Yerusalemu; pia kila jengo mhimu mjini alilichoma.
Et il livra aux flammes le temple du Seigneur, le palais du roi et toutes les maisons de la ville, et il mit le feu à toutes les grandes maisons.
14 Kama kwa kuta za kuuzunguka Yerusalemu, jeshi lote la Wababeli lililokuwa pamoja na jemedari wa mlinzi wakaviaribu.
Et l'armée des Chaldéens qui étaient avec le chef des cuisines rasa les remparts dont la ville était entourée.
15 Kama kwa watu maskini sana, watu waliosalia walioachwa katika mji, waliokuwa wamemwendea mfalme wa Babeli, na baadhi ya watu wenye ujuzi - Nebuzaradan, jemedari wa askari walinzi, akawachukua baadhi yao uhamishoni.
16 Lakini Nebuzaradani, jemedari wa mlinzi, akawaacha baadhi ya maskini sana wa nchi kuitunza mizabibu na mashamba.
Mais Nabuzardan y laissa les restes du peuple, pour être vignerons et laboureurs.
17 Lakini kwa nguzo za shaba lilizokuwa katika nyumba ya Yahwe, mishikio na bahari ya shaba iliyokuwa katika nyumba ya Yahwe, Wakaldayo wakaivunja vipande wakaondoka navyo kurudi Babeli.
Et les Chaldéens brisèrent les colonnes d'airain et leurs bases et la mer d'airain qui étaient dans le temple du Seigneur, et ils en emportèrent le métal à Babylone,
18 Vyungu, makoleo, kinara cha taa, mabakuri, na vitu vyote vya shaba ambavyo makuhani walikuwa wakivitumia hekaluni - Wakaldayo wakavichukua vyote.
Avec les couronnes, les coupes et les chaudières, et tous les vases d'airain employés au service du temple.
19 Makalai na chetezo cha uvumba, mabakuri, vyungu, kinara cha taa, vikaango, makalai zilizotengenezwa kwa dhahabu, na zilizotengenezwa kwa dhahabu - kapteni wa mlinzi wa mfalme akazichukua pia.
Et il prit aussi les cassolettes et les bassins, et les vases à verser de l'huile, et les chandeliers, et les encensoirs, et les coupes, qui étaient les unes d'or, les autres d'argent;
20 Nguzo mbili, bahari, na ng'ombe kumi na wawili wa shaba waliokuwa chini yake, vitu Selemani alivyokuwa amevifanya kwa ajili ya nyumba ya Yahwe, vikiwa na shaba nyingi sana isiyoweza kupimwa.
Et les deux colonnes, et la mer, et les douze bœufs d'airain sous la mer, qu'avait faits le roi Salomon pour le temple du Seigneur. On ne sut pas le poids des vases d'airain.
21 Nguzo zilikuwa na urefu wa dhiraha kumi na nane kila moja, na mstari kuzunguka kila moja wenye urefu wa dhiraha kumi na mbili. Kila moja ilikuwa na unene wa vidole vinne na tundu.
Et les colonnes étaient hautes chacune de trente-cinq coudées, et elles étaient, entourées de chaînes longues de douze coudées, épaisses de quatre doigts.
22 Kichwa cha shaba kilikuwa juu yake. Kichwa kilikuwa dhiraha tano urefu wake, kazi ya waya zinazokingamana na makomamanga kukizunguka. Chote kilitengenezwa kwa shaba. Na nguzo nyingine ilikuwa na makomamanga yake vilikuwa kama ya kwanza.
Et leurs chapiteaux d'airain avaient cinq coudées de haut, et elles étaient entourées d'un filet et de grenades d'airain, et il y avait huit grenades par coudée, et il y avait douze coudées,
23 Hivyo kulikuwa na makomamanga tisini na sita ubavuni mwa kila kichwa, na makomamanga mia moja juu ya nyaya zilizokingamana kukizunguka.
Et il y avait quatre-vingt-seize grenades sur les côtés, et il y avait en tout cent grenades sur le filet tout autour.
24 Jemedari wa mlinzi akamchukua Seraya mfungwa, kuhani mkuu, pamoja na Sefania, kuhani wa pili, na wale mabawaba watatu.
Et Nabuzardan prit le premier prêtre, puis le second et les trois gardiens de la voie,
25 Kutoka mjini akamchukua mfungwa afsa aliyekuwa juu ya askari, na watu saba wa wale waliomshauri mfalme, waliokuwa wamesalia mjini. Akamchukua mfungwa afsa wa jeshi la mfalme aliyekuwa na wajibu wa kuwaingiza watu katika jeshi, pamoja na watu mashuhuri sitini kutoka katika nchi waliokuwamo mjini.
Et un eunuque, chef des gens de guerre, et sept hommes distingués se tenant devant le roi, qui se trouvaient dans la ville, et le scribe des armées, chargé des écritures du peuple de la terre, et soixante hommes de la campagne qui se trouvaient dans la ville.
26 Kisha Nebuzaradani, jemedari wa mlinzi, akawachukuwa na kuwaleta kwa mfalme wa Babeli huko Ribla.
Et Nabuzardan, cuisinier en chef du roi, les prit et les conduisit au roi de Babylone à Déblatha.
27 Mfalme wa Babeli akawaua huko Ribla katika nchi ya Hamathi. Kwa njia hii, Yuda akaondoka katika nchi yake na kwenda uhamishoni.
Et le roi les fit mettre à mort à Déblatha, en la terre d'Émath.
28 Hawa walikuwa watu Nebukadneza aliwaamisha: katika mwaka wa saba, Wayudea 3, 023.
29 Katika mwaka wa kumi na nane wa Nebukadneza alichukuwa 832 kutoka Yerusalemu.
30 Katika mwaka wa ishirini na tatu wa Nebukadneza, Nebuzaradani, jemedari wa walinzi wa mfalme, aliwahamisha Wayudea 745. Jumla ya watu walioamishwa walikuwa 4, 600.
31 Ikawa baadaye katika mwaka wa thelathini na saba wa kufungwa kwake Yohoyakini, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na tano ya mwezi, Evili Merodaki, mfalme wa Babeli akamfungua Yehoyakini mfalme wa Yuda kutoka kifungoni. Ilikuwa mwaka ambao Evili Merodaki alianza kutawala.
En la trente-septième année de la captivité de Joakim, roi de Juda, le douzième mois, le vingt-troisième jour du mois, Ulémadachar, roi de Babylone, l'année même où il monta sur le trône, prit la tête de Joakim et lui coupa les cheveux, et le fit sortir de la maison où il était gardé,
32 Akaongea naye kwa upole na akampa kiti cha heshima kuliko cha wafalme wengine aliokuwa pamoja nao huko Babeli.
Et il lui parla avec douceur, et il lui donna un trône plus élevé que les trônes des autres rois qui l'entouraient à Babylone.
33 Evili Merodaki akaondoa mavazi ya gerezani ya Yehoyakini, na Yehoyakini akala chakula cha daima katika meza ya mfalme siku zote zilizosalia za maisha yake.
Et il lui fit changer la robe qu'il avait en prison; et il le fit manger en sa présence tous les jours qu'il vécut.
34 Na alipewa posho ya chakula cha kila siku kwa maisha yake yote yaliyosalia mpaka siku ya kufa kwake.
Et tous les jours, jusqu'à ce qu'il mourût, il régla constamment toute sa dépense.