< Yeremia 47 >

1 Hili ni neno la Yahwe lililokuja kwa Yeremia nabi juu ya Wafilisiti. Neno hili lilimjia kabla Farao hajaishambulia Gaza.
在法郎尚未進攻迦薩以前,關於培肋舍特,上主有話傳給耶肋米亞先知說:
2 “Yahwe asema hivi: Tazama, mafuriko ya maji yanainuka huko kaskazini. Yatakuwa kama mto uliofurika! Kisha yataigharikisha nchi na kila kitu ndani yake, miji yake na watu wakaao ndani yake! Kila mtu atapiga kelele ya kuomba msaada, na wakaaji wote wa nchi wataomboleza.
上主這樣說:「看,有水從北方湧來,形成一條氾濫的河流,淹沒大地和地上的一切,首都和其中的居民;人們必要喊叫,大地所有的居民必要哀號。
3 Kwa sauti ya kukanyaga kwa kwato za farasi wao wenye nguvu, kwa mwungurumo wa vibandawazi vyao na kelele za magurudumu yao, wazazi hawatawasaidia watoto wao kwa sababu ya udhaifu wao.
一聽到他駿馬的鐵蹄聲,轔轔的戰車聲,和隆隆的飛輪聲,為父親的已束手無策,不能再顧及自己的兒子,
4 Kwa maana siku inakuja itakayowaacha ukiwa Wafilisiti wote, kumwondoa kila mtu aliyesalia anayetaka kuwasaidia. Kwa maana Yahwe anawaangamiza Wafilisiti, waliosalia katika kisiwa cha Kaftori.
因為消滅一切培肋舍特人,和摧毀提洛及漆冬一切殘餘助手的日子來到了,上主要消滅培肋舍特人,加非托爾島的遺民
5 Maombolezo yatakuja juu ya Gaza. Hata kwa Ashikeloni, watu waliosalia bondeni watakuwa kimya. Ni kwa muda gani mtajiondoa katika maombolezo?
迦薩已一片荒涼,阿市刻隆已遭受滅亡;阿納克人的遺民,你們要割傷己身到何時呢﹖
6 Ole, upanga wa Yahwe! itachukua muda gani hata unyamaze? Rudini alani mwenu! Acha na unyamaze.
唉! 上主的刀劍! 到何時纔休息﹖請你入鞘休息安歇罷!
7 Wawezaje kuwa kimya, maana Yahwe amekuagiza. Amekuamuru kumpiga Ashikeloni na dhidi ya nchi ya pwani ya bahari.
但上主既對它出了命,它怎能休息﹖阿市刻隆和海濱,是他給它指向的地方。

< Yeremia 47 >