< Yeremia 44 >

1 Hili lilikuwa neno ambalo lilikuja kwa Yeremia kuhusu Wayahudi wote walioishi katika nchi ya Misri, wale wanaoishi Migdoli, Tahpanhesi, Memphis, na katika nchi ya Patrosi.
Verbum, quod factum est per Ieremiam ad omnes Iudaeos, qui habitabant in Terra Aegypti, habitantes in Magdalo, et in Taphnis, et in Memphis, et in Terra Phatures, dicens:
2 “Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi: Wewe mwenyewe umeyaona maafa yote niliyoleta juu ya Yerusalemu na miji yote ya Yuda. Ona, ni ukiwa leo. Hakuna yeyote anaishi mwao.
Haec dicit Dominus exercituum Deus Israel: Vos vidistis omne malum istud, quod adduxi super Ierusalem, et super omnes urbes Iuda: et ecce desertae sunt hodie, et non est in eis habitator:
3 Hii ni kwa sababu ya mambo maovu waliyofanya kunikosea mimi kwa kwenda kuchoma ubani na kuabudu miungu mengine. Hawa walikuwa miungu ambao wala wao wenyewe, wala ninyi, wala mababu zenu walijua.
Propter malitiam, quam fecerunt ut me ad iracundiam provocarent, et irent ut sacrificarent, et colerent deos alienos, quos nesciebant et illi, et vos, et patres vestri.
4 Basi nirudie kuwatuma watumwa wangu wote manabii kwao. Niliwatuma wao kusema, 'Acha kufanya vitu hivi machukizo ambayo nachukia.
Et misi ad vos omnes servos meos prophetas de nocte consurgens, mittensque et dicens: Nolite facere verbum abominationis huiuscemodi, quam odivi.
5 Lakini hawakunisikiliza. Walikataa kuwa makini au kuyaacha maovu kwa kuchoma ubani kwa miungu mingine.
Et non audierunt, nec inclinaverunt aurem suam ut converterentur a malis suis, et non sacrificarent diis alienis.
6 Basi hasira yangu na gadhabu yangu zilimwanga na kuwasha moto kwenye miji ya Yuda na mitaa ya Yerusalemu. Basi waliharibiwa na kuteketezwa, kama katika siku ya leo.”
Et conflata est indignatio mea et furor meus, et succensa est in civitatibus Iuda, et in plateis Ierusalem: et versae sunt in solitudinem et vastitatem secundum diem hanc.
7 Basi sasa Yahwe, Mungu wa majeshi na Mungu wa Israel, asema hivi, “Kwanini unafanya maovu makubwa dhidi yenu? Kwanini mnasababisha ninyi wenyewe kujitenga kutoka miongoni mwa Yuda - wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao? Hakuna mabaki yenu yatabaki.
Et nunc haec dicit Dominus exercituum Deus Israel: Quare vos facitis malum grande hoc contra animas vestras, ut intereat ex vobis vir et mulier, parvulus et lactens de medio Iuda, nec relinquatur vobis quidquam residuum:
8 Kwa maovu yenu mmenikosea pamoja na matendo ya mikono yenu, kwa kuchoma ubani kwa miungu mingine kwenye nchi ya Misri, ambapo mmekwenda kuishi. Mmeenda huko ili kwamba mtaangamizwa, ili kwamba mtalaaniwa na mashutumu miongoni mwa mataifa yote ya duniani.
Provocantes me in operibus manuum vestrarum, sacrificando diis alienis in Terra Aegypti, in quam ingressi estis ut habitetis ibi: et dispereatis, et sitis in maledictionem, et in opprobrium cunctis gentibus terrae?
9 Mmesahau maovu yaliyofanywa na mababu zenu na maouvu yaliyofanywa na wafalme wa Yuda na wake zao? Mmesahau uovu uliofanywa na ninyi na wake zenu katika nchi ya Yuda na mitaa ya Yerusalemu?
Numquid obliti estis mala patrum vestrorum, et mala regum Iuda, et mala uxorum eius, et mala vestra, et mala uxorum vestrarum, quae fecerunt in Terra Iuda, et in regionibus Ierusalem?
10 Kwa siku hii, hawajanyenyekea bado. Hawashimu sheria yangu au maagizo niliyoweka mbele yao na mababu zao, wala hawatembei nazo.”
Non sunt mundati usque ad diem hanc: et non timuerunt, et non ambulaverunt in lege Domini, et in praeceptis meis, quae dedi coram vobis et coram patribus vestris.
11 Kwa hiyo sasa Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi, “Ona, Nimekaribia kuweka uso wangu dhidi yenu kuleta maafa kwenu na kuiharibu Yuda yote.
Ideo haec dicit Dominus exercituum Deus Israel: Ecce ego ponam faciem meam in vobis in malum: et disperdam omnem Iuda.
12 Kwa kuwa nitachukua mabaki wa Yuda ambaye ameanza safari kwenda nchi ya Misri kuishi huko. Nitafanya hivi ili kwamba wataangamia wote katika nchi ya Misri. Wataanguka kwa upanga na njaa. Kutoka wadogo kwa wakubwa wataangamia kwa upanga na njaa. Watakufa na watakuwa sababu ya kuaapa, kulaani, mashutumu, na kitu kibaya.
Et assumam reliquias Iuda, qui posuerunt facies suas ut ingrederentur Terram Aegypti, et habitarent ibi: et consumentur omnes in Terra Aegypti: cadent in gladio et in fame: et consumentur a minimo usque ad maximum in gladio, et in fame morientur: et erunt in iusiurandum, et in miraculum, et in maledictionem, et in opprobrium.
13 Kwa kuwa nitawaadhibu watu wakazi wa nchi ya Misri kama nilivyoadhibu Yerusalem kwa upanga, njaa, na pigo.
Et visitabo super habitatores Terrae Aegypti, sicut visitavi super Ierusalem in gladio, et fame, et peste.
14 Hakuna mkimbizi au mwathirika wa mabaki ya Yuda ambaye wataenda kuishi huko kwenye nchi ya Misri watarudi kwenye nchi ya Yuda, hata kama wanataka kurudi na kuishi huko. Hakuna kati yao atarudi, ijapokuwa wachache ambayo watatoroka kutoka huko.”
Et non erit qui effugiat, et sit residuus de reliquiis Iudaeorum, qui vadunt ut peregrinentur in Terra Aegypti: et revertantur in Terram Iuda, ad quam ipsi elevant animas suas ut revertantur, et habitent ibi: non revertentur nisi qui fugerint.
15 Kisha watu wote ambao walijua kwamba wake zao walikuwa wakichoma ubani kwa miungu mingine, na wanawake wote waliokuwa katika kusanyiko kuu, na watu wote ambao walikuwa wakiishi kwenye nchi ya Misri katika Pathrosi walimjibu Yeremia.
Responderunt autem Ieremiae omnes viri scientes quod sacrificarent uxores eorum diis alienis: et universae mulieres, quarum stabat multitudo grandis, et omnis populus habitantium in Terra Aegypti in Phatures, dicentes:
16 Walisema, “Kuhusu neno ambalo mmetuambia sisi kwa jina la Yahwe: Hatutakusikiliza.
Sermonem, quem locutus es ad nos in nomine Domini, non audiemus ex te:
17 Kwa hakika tutafanya mambo yote ambayo tulisema tungefanya: kuchoma ubani kwa malkia wa Mbingu na kumwaga kinywaji cha sadaka kwake kama sisi, mababu zetu, wafalme wetu, na viongozi wetu walivyofanya kwenye miji ya Yuda na mitaa ya Yerusalemu. Kisha tutajazwa pamoja na chakula na tutafanikiwa, pasipo kupata maafa yoyote.
sed facientes faciemus omne verbum, quod egredietur de ore nostro ut sacrificemus reginae caeli, et libemus ei libamina, sicut fecimus nos, et patres nostri, reges nostri, et principes nostri in urbibus Iuda, et in plateis Ierusalem: et saturati sumus panibus, et bene nobis erat, malumque non vidimus.
18 Wakati tunajiepusha kutofanya mambo haya, si kutoa sadaka ya ubani kwa Malkia wa Mbinguni na si kumwanga kinywaji cha sadaka kwake, tulikuwa wote tunaumwa umaskini na tulikuwa tunakufa kwa upanga na njaa.”
Ex eo autem tempore, quo cessavimus sacrificare reginae caeli, et libare ei libamina, indigemus omnibus, et gladio, et fame consumpti sumus.
19 Wanawake walisema, “Wakati tulipokuwa tunatengeneza ubani wa sadaka mbele ya Malkia wa Mbinguni na kumwaga kinywaji cha sadaka kwake, tulifanya hivi vitu pasipo waume wetu kujua.”
Quod si nos sacrificamus reginae caeli, et libamus ei libamina: numquid sine viris nostris fecimus ei placentas ad colendum eam, et libandum ei libamina?
20 Kisha Yeremia alisema kwa watu wote - kwa wanaume na wanawake, na watu wote waliomjibu yeye - alihubiri na kusema,
Et dixit Ieremias ad omnem populum adversum viros, et adversum mulieres, et adversum universam plebem, qui responderant ei verbum, dicens:
21 “Je Yahwe hakukumbuka ubani ambao mliuchoma kwenye miji ya Yuda na mitaa ya Yerusalem - wewe na mababu zenu, wafalme wenu na viongozi, na watu wa nchi? Kwa kuwa Yahwe anakumbuka hili kwenye akili; inakuja kwenye mawazo yake.
Numquid non sacrificium, quod sacrificastis in civitatibus Iuda, et in plateis Ierusalem vos et patres vestri, reges vestri, et principes vestri, et populus terrae, horum recordatus est Dominus, et ascendit super cor eius?
22 Basi hawakuweza tena kuvumilia kwa sababu ya matendo yenu maovu, kwa sababu machukizo ambayo mlifanya. Basi nchi yenu imekuwa ukiwa, kutisha, na laana basi hapakuwa na mkazi tena kwa siku hii.
Et non poterat Dominus ultra portare propter malitiam studiorum vestrorum, et propter abominationes, quas fecistis, et facta est terra vestra in desolationem, et in stuporem, et in maledictum, eo quod non sit habitator, sicut est dies haec.
23 Kwa sababu mlichoma ubani na kufanya dhambi dhidi ya Yahwe, na kwa sababu msingesikiliza sauti yake, sheria yake, amri zake, au maagizo ya agano lake, maafa haya dhidi yenu yemetokea kama kwa siku hii. “
Propterea quod sacrificaveritis idolis, et peccaveritis Domino: et non audieritis vocem Domini, et in lege, et in praeceptis, et in testimoniis eius non ambulaveritis: idcirco evenerunt vobis mala haec, sicut est dies haec.
24 Kisha Yeremia alisema kwa watu wote na wanawake wote, “Sikia neno la Yahwe, Yuda yote ambao wamo katika nchi ya Misri.
Dixit autem Ieremias ad omnem populum, et ad universas mulieres: Audite verbum Domini omnis Iuda, qui estis in Terra Aegypti:
25 Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi, Wewe na wake zako wote mmesema kwa vinywa vyenu na kubeba kwa mikono yenu kile mlichosema, “Hakika tutabeba viapo ambavyo tulifanya kumwabudu Malkia wa Mbinguni, kwanga kinywaji cha sadaka kwake.” Sasa timiza viapo vyenu, vibebe.”
Haec inquit Dominus exercituum Deus Israel, dicens: Vos, et uxores vestrae locuti estis ore vestro, et manibus vestris implestis, dicentes: Faciamus vota nostra, quae vovimus, ut sacrificemus reginae caeli, et libemus ei libamina. implestis vota vestra, et opere perpetrastis ea.
26 Basi, sikiliza neno la Yahwe, Yuda yote ambao mnaishi katika nchi ya Misri, 'Ona, Nimeapa kwa jina langu kuu-asema Yahwe. Jina langu halitaitwa kwa vinywa vya wanaume wowote wa Yuda kwenye nchi ya Misri, wewe ambaye sasa unasema, “Kama Bwana Yahwe aishivyo.”
Ideo audite verbum Domini omnis Iuda, qui habitatis in Terra Aegypti: Ecce ego iuravi in nomine meo magno, ait Dominus: quia nequaquam ultra vocabitur nomen meum ex ore omnis viri Iudaei, dicentis: Vivit Dominus Deus in omni Terra Aegypti.
27 Ona, Ninakutazama juu yako kwa ajili ya maafa na si kwa uzuri. Kila mtu wa Yuda katika nchi ya Misri ataangamia kwa upanga na njaa mpaka wote wameishia.
Ecce ego vigilabo super eos in malum, et non in bonum: et consumentur omnes viri Iuda, qui sunt in Terra Aegypti, gladio, et fame donec penitus consumantur.
28 Kisha waathirika wa upanga watarudi kutoka nchi ya Misri kwa nchi ya Yuda, peke idadi ndogo yao. Basi mabaki yote ya Yuda walioenda kwenye nchi ya Misri kuishi huko watajua ambao neno litakuwa kweli: yangu au yao.
Et qui fugerint gladium, revertentur de Terra Aegypti in Terram Iuda viri pauci: et scient omnes reliquiae Iuda ingredientium Terram Aegypti, ut habitent ibi, cuius sermo compleatur, meus, an illorum.
29 Hii itakuwa ishara kwa ajili yako - hili ni tamko la Yahwe - kwamba ninaweka dhidi yenu katika eneo hili, ili kwamba mtajua kwamba maneno yangu hakika yatawavamia pamoja na maafa.
Et hoc vobis signum, ait Dominus, quod visitem ego super vos in loco isto: ut sciatis quia vere complebuntur sermones mei contra vos in malum.
30 Yahwe asema hivi, 'Tazama, ninakaribia kumtoa Farao Hofra mfalme wa Misri kwenye mkono wa adui zake na kwenye mkono wa wale wanaotafuta kumuua. Itakuwa sawa kama wakati nilimpa Sedekia mfalme wa Yuda kwenye mkono wa Nebukadreza mfalme wa Babeli, adui wake aliyetafuta maisha yake.
Haec dicit Dominus: Ecce ego tradam Pharaonem Ephree regem Aegypti in manu inimicorum eius, et in manu quaerentium animam illius: sicut tradidi Sedechiam regem Iuda in manu Nabuchodonosor regis Babylonis inimici sui, et quaerentis animam eius.

< Yeremia 44 >