< Yeremia 40 >
1 Hili lilikuwa neno ambalo lilikuja kwa Yeremia toka kwa Yahwe baada ya Nebuzaradni, amri wa walinzi wa mfalme, amemtuma mbali kutoka Ramah. Huko ndiko Yeremia alikuwa amechukuliwa, na huko alikuwa amefungwa kwa minyororo. Alikuwa miongoni mwa mateka wote ya Yerusalem na Yuda ambayo walipaswa kuwa matekani Babeli.
2 Mlinzi mkuu alimchukua Yeremia na kusema kwake, “Yahwe Mungu wako aliamrisha maafa haya dhidi ya eneo hili.
3 Basi Yahwe alileta. Alifanya kama alivyoamrisha, kwani ninyi watu mmefanya dhambi dhidi yake na hamkutii sauti yake. Hii ni sababu ya jambo hili limetokea kwenu. Lakini sasa tazama!
4 Nimekuacha huru leo toka kwenye minyororo iliyokuwa kwenye mikono yako. Kama ni vizuri katika macho yako kuja nami Babeli, njoo, na nitakujali. Lakini kama si vizuri katika macho yako kuja pamoja nami, basi usifanye hivyo. Tazama nchi yote mbele yako. Nenda ambapo ni pazuri na sawa katika macho yako kwenda.”
5 Wakati Yeremia hakujibu, Nebuzaradani alisema, “Nenda kwa Gedalia mwana wa Ahikam mwana wa Shafani, ambaye mfalme wa Babeli amemweka msimamizi wa miji ya Yuda. Baki pamoja naye miongoni mwa watu au nenda popote ni pazuri katika macho yako kwenda.” Amri wa walinzi wa mfalme alimpa chakula na zawadi, na kisha akamtuma mbali.
6 Basi Yeremia alienda kwa Gedalia mwana wa Ahikam, huko Mizpah. Alibaki pamoja naye miongoni mwa watu ambao walibaki nyuma katika nchi.
7 Sasa baadhi ya amri wa wanawajeshi wa Yuda ambao walikuwa bado katika uwanja- wao na watu wao - walisikia kuwa mfalme wa Babeli alimfanya Gedalia mwana wa Ahikam, liwali juu ya nchi. Pia walisikia kuwa amemweka kusimamia wanaume, wanawake, na watoto ambao walikuwa watu maskini katika nchi, wale ambao hawakuwa wamechukuliwa mateka Babeli.
8 Basi walienda kwa Gedalia huko Mizpa. Hawa watu walikuwa Ishmaeli mwana Nethania; Yonathan na Yonathani, wana wa Kareaa; Seraya mwana wa Tanhumethi; wana wa Efai Netophathite; na Yezania mwana wa Mmaaka-wao na watu wao.
9 Gedalia mwana wa Ahikam mwana wa Shafan, alichukua kiapo kwao na kwa watu wao, na kusema kwao, “Usiogope kuwatumikia maafisa wa Wakaldayo. Ishi katika nchi na kumtumkia mfalme wa Babeli, na itakuwa vizuri kwenu.
10 Na tazama, Ninaishi Mizpa kukutana pamoja na Wakaldayo waliokuja kwetu. Basi vuna mvinyo, matunda ya kiangazi, na mafuta na viweke kwenye vyombo vyako. Uishi katika miji ambayo umechukua.”
11 Kisha Wayahudi wote katika Moabu, miongoni mwa watu wa Ammoni, na katika Edomu, na katika kila nchi ilisikiwa kwamba mfalme wa Babalei ameruhusu mabaki ya Yuda kubaki, kwamba alimteua Gedalia mwana wa Ahikam mwana wa Shafani juu yao.
12 Basi Wayahudi wote walirudi toka kila eneo ambako walikuwa wametawanyika. Walirudi kwenye nchi ya Yuda, kwa Gedalia huko Mizpa. Walivuna mvinyo na matunda ya kiangazi kwa wingi.
13 Yonathan mwana wa Karea na amri wote wa jeshi katika uwanja walikuja kwa Gedalia huko Mizpa.
14 Walisema kwake, “Haujui kuwa Baalis mfalme wa watu wa Ammoni amemtuma Ishmael mwana wa Nethania kukuua?” Lakini Gedalia mwana wa Ahikim hakuwaamini.
15 Basi Yonathan mwana wa Karea alizungumza kwa siri kwa Gedalia huko Mizpa na kusema, “Niruhusu niende kumuua Ishmael mwana wa Nethania. Hakuna atakaye nituhumu. Kwanini asikuue wewe? Kwanini kuruhusu Yuda yote ambayo imekusanywa kwako kutawanyishwa na mabaki ya Yuda kuharibiwa?”
16 Lakini Gedalia mwana wa Ahikam alisema kwa Yonathan mwana wa Karea, “Usifanye jambo hili, kwa kuwa unasema uongo kuhusu Ishmael.”