< Yeremia 39 >

1 Katika mwaka wa tisa na mwezi wa kumi wa Sedekia mfalme wa Yuda, Nebukadreza mfalme wa Babeli alikuja pamoja na jeshi lake lote dhidi ya Yerusalem na kuizingira.
유다 왕 시드기야의 구년 시월에 바벨론 왕 느부갓네살과 그 모든 군대가 와서 예루살렘을 에워싸고 치더니
2 Katika mwaka wa kumi na moja na mwezi wa nne wa Sekeia, siku ya tisa ya mwezi, mji uliharibiwa.
시드기야의 제 십 일년 사월 구일에 성이 함락되니라 예루살렘이 함락되매
3 Kisha maafisa wote wa mfalme wa Babeli walikuja na kukaa kwenye lango la katikati: Nergali Sharezeri, Samgari Nebo, na Sarsechimu, afisa muhimu. Nerga Sharezeri alikuwa afisa mkuu na wote waliobaki maafisa wa mfalme wa Babeli.
바벨론 왕의 모든 방백이 이르러 중문에 앉으니 곧 네르갈사레셀과 삼갈르보와 환관장 살스김과 박사장 네르갈사레셀과 바벨론 왕의 기타 모든 방백들이었더라
4 Ilitokea kwamba wakati Sedekia, mfalme wa Yuda, na wanaume wapiganaji wake wote walipowaona, walikimbia. Walitoka nje usiku toka kwenye mji kwa njia ya bustani ya mfalme, kupitia lango la kati la kuta mbili. Mfalme alitoka nje katika mwelekeo wa Arabah.
유다 왕 시드기야와 모든 군사가 그들을 보고 도망하되 밤에 왕의 동산길로 좇아 두 담 샛문을 통하여 성읍을 벗어나서 아라바로 갔더니
5 Lakini jeshi la Wakaldayo walimfatilia na kumpata Sedekia kwenye tambarare za mto Yordani karibu na Yeriko. Kisha walimshika na kumleta kwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, Riblah kwenye nchi ya Hamath, ambapo Nebukadreza alipitisha sentensi juu yake.
갈대아인의 군대가 그들을 따라 여리고 평원에서 시드기야에게 미쳐 그를 잡아서 데리고 하맛 땅 립나에 있는 바벨론 왕 느부갓네살에게로 올라가매 왕이 그를 심문하였더라
6 Mfalme wa Babeli alimchinja binti wa Sedekia mbele ya macho yake huko Ribla. Pia aliwachinja wanaume wote wa heshima wa Yuda.
바벨론 왕이 립나에서 시드기야의 목전에서 그 아들들을 죽였고 왕이 또 유다의 모든 귀인을 죽였으며
7 Kisha alingoa macho ya Sedekia na kumfunga mnyororo wa shaba ili kusudi kumpeleka Babeli.
왕이 또 시드기야의 눈을 빼게하고 바벨론으로 옮기려 하여 사슬로 결박하였더라
8 Kisha Wakaldayo walichoma nyumba ya mfalme na nyumba za watu. Pia walivunja kuta za Yerusalem.
갈대아인들이 왕궁과 백성의 집을 불사르며 예루살렘 성벽을 헐었고
9 Nebukadreza, nahodha wa walinzi wa mfalme, waliwachukua katika mateka watu wengine waliobaki katika mji. Hii ilijumuisha watu waliotoka jangwa kwenda Wakaldayo na watu wengine walioachwa katika mji.
시위대장 느부사라단이 성 중에 남아 있는 백성과 자기에게 항복한 자와 그 외의 남은 백성을 바벨론으로 잡아 옮겼으며
10 Lakini Nebukadreza nahodha wa walinzi wa mfalme aliwaruhusu watu maskini ambayo hawakuwa na chochote wao kubaki katika chi ya Yuda. Aliwapa mashamba ya mizabibu na maeneo katika siku ile.
시위대장 느부사라단이 아무 소유가 없는 빈민을 유다 땅에 남겨두고 그 날에 포도원과 밭을 그들에게 주었더라
11 Nebukadreza mfalme wa Babeli alikuwa ametoa amri kuhusu Yeremia kwa Nebuzaradani nahodha wa walinzi wa mfalme. Alikuwa amesema,
바벨론 왕 느부갓네살이 예레미야에 대하여 시위대장 느부사라단에게 명하여 가로되
12 “Mchukue na umjali. Usimdhuru. Fanya kwa ajili yake chochote anachokuambia.”
그를 데려다가 선대하고 해하지 말며 그가 네게 말하는 대로 행하라
13 Basi Nebuzaradani nahodha wa walinzi wa mfalme, Nebushazbani mkuu wa matoashi, Nergali Sharezeri afisa mkuu, na wote maafisa wa muhimu wa mfalme wa Babeli walituma watu nje.
이에 시위대장 느부사라단과 환관장 느부사스반과 박사장 네르갈사레셀과 바벨론 왕의 모든 장관이
14 Watu wao walimchukua Yeremia kutoka uwanja wa mlinzi na kumkabidhi kwa Gedalia mwana wa Ahikami mwana wa Shafani, kumchua nyumbani, basi Yeremia alibaki miongoni mwa watu.
보내어 예레미야를 시위대 뜰에서 취하여 내어 사반의 손자 아히감의 아들 그다랴에게 붙여서 그를 집으로 데려가게 하매 그가 백성 중에 거하니라
15 Sasa neno la Yahwe lilikuwa limekuja kwa Yeremia wakati alipokuwa chini ya kifungo kwenye uwanja wa mlinzi, na alisema,
예레미야가 시위대 뜰에 갇혔을 때에 여호와의 말씀이 그에게 임하니라 가라사대
16 “Zungumza kwa Ebedi Meleki Mkushi na sema, 'Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi: Ona, Nimekaribia kubeba maneno yangu dhidi ya mji huu kwa ajili ya janga na si kwa uzuri. Kwa kuwa yatakuwa kweli mbele yako katika siku hiyo.
너는 가서 구스인 에벳멜렉에게 말하기를 만군의 여호와 이스라엘의 하나님의 말씀에 내가 이 성에 재앙을 내리고 복을 내리지 아니하리라 한 나의 말이 그 날에 네 목전에 이루리라
17 Lakini nitakuokoa katika siku hiyo - hili ni tamko la Yahwe - na hautatiwa katika mkono wa wanaume ambayo unawaogopa.
나 여호와가 말하노라 내가 그 날에 너를 구원하리니 네가 그 두려워하는 사람들의 손에 붙이우지 아니하리라
18 Kwa kuwa nitakuokoa hakika. Hautaanguka kwa upanga. Utatoroka pamoja na maisha yako, kwani unanitumaini - hili lilikuwa tamko la Yahwe.”
내가 단정코 너를 구원할 것인즉 네가 칼에 죽지 아니하고 네 생명이 노략물을 얻음같이 되리니 이는 네가 나를 신뢰함이니라 여호와의 말이니라

< Yeremia 39 >