< Yeremia 38 >
1 Shefatia mwana wa Matani, Gedalia mwana wa Pashuri, na Pashuri mwana wa Malkiya alisikia maneno ambayo Yeremia alikuwa akitanganza kwa wato wote. Alikuwa akisema,
Shefatia mwana wa Matani, na Gedalia mwana wa Pashuri, na Yehukali mwana wa Shelemia, na Pashuri mwana wa Malkiya wakasikia kile Yeremia alichokuwa akiwaambia watu wote wakati aliposema,
2 “Yahwe asema hivi: Yeyote anayeishi kwenye mji huu atauwawa kwa upanga, njaa, na pigo. Lakini yeyote ambaye aendae kwa Wakaldayo ataishi. Atatoroka pamoja na maisha yake mwenyewe, na kuishi.
“Hili ndilo asemalo Bwana: ‘Yeyote akaaye ndani ya mji huu atakufa kwa upanga, njaa au tauni, lakini yeyote atakayejisalimisha kwa Wakaldayo ataishi. Atakayeyatoa maisha yake kama nyara, ataishi.’
3 Yahwe asema hivi: Huu mji huu utapewa kwa mkono wa jeshi la mfalme wa Babeli, na ataukamata.”
Tena hili ndilo asemalo Bwana: ‘Mji huu kwa hakika utatiwa mikononi mwa jeshi la mfalme wa Babeli, ambaye atauteka.’”
4 Kwa hiyo maafisa walisema kwa mfalme, “Acha mtu huu afe, kwa kuwa kwa njia hii anadhofisha mikono ya wanaume wapiganaji waliobaki kwenye mji huu, na mikono ya watu wote. Anatanganza maneno haya, kwa kuwa huyu mtu hafanyi kwa usalama wa watu hawa, lakini kwa majanga.”
Ndipo maafisa wakamwambia mfalme, “Mtu huyu imempasa kuuawa. Anawakatisha tamaa askari waliobaki katika mji huu, vivyo hivyo na watu wote pia, kwa ajili ya mambo anayowaambia. Mtu huyu hawatakii mema watu hawa, bali maangamizi yao.”
5 Basi mfalme Sedekia alisema, “Tazama, yuko mkononi mwako kwa kuwa hakuna mfalme awezae kumpinga.”
Mfalme Sedekia akajibu, “Yeye yuko mikononi mwenu! Mfalme hawezi kufanya lolote kuwapinga ninyi.”
6 Kisha walimchukua Yeremia na kumtupa kwenye kisima cha Malkiya, mwana wa mfalme. Kisima kilikuwa kwenye uwanja wa mlinzi. Walimshusha Yeremia chini kwa kamba. Hapakuwa na maji kwenye kisima, lakini kulikuwa na matope, na alizama chini ya matope.
Basi wakamchukua Yeremia na kumtia kwenye kisima cha Malkiya, mwana wa mfalme, kilichokuwa katika ua wa walinzi. Wakamteremsha Yeremia kwa kamba ndani ya kisima. Hakikuwa na maji ndani yake, ila tope tu, naye Yeremia akazama ndani ya matope.
7 Sasa Ebed Meleki Mkushi alikuwa mmoja wa watowashi katika nyumba ya mfalme. Alisikia kwamba walikuwa wamemuweka Yeremia kwenye kisima. Sasa mfalme alikuwa ameketi kwa mlango wa Benjamini.
Lakini Ebed-Meleki Mkushi, aliyekuwa afisa katika jumba la kifalme, akasikia kuwa walikuwa wamemtia Yeremia ndani ya kisima. Wakati mfalme alipokuwa ameketi katika Lango la Benyamini,
8 Basi Ebed Meleki alienda toka nyumba ya mfalme na kuzungumza na mfalme.
Ebed-Meleki akatoka nje ya jumba la kifalme na kumwambia,
9 Alisema, “Bwana wangu mfalme, hawa wanaume wamefanya uovu kwa namna walivyomtendea Yeremia nabii. Walimtupa kwenye kisima kwa ajili ya kufa kutokana na njaa, tangu hakuna chakula zaidi katika mji.”
“Mfalme bwana wangu, watu hawa wamefanya uovu kwa yote waliomtendea nabii Yeremia. Wamemtupa ndani ya kisima, mahali ambapo atakufa kwa njaa wakati ambapo hakuna chakula popote katika mji.”
10 Kisha mfalme alitoa amri kwa Ebed Meleki Mkushi. Alisema, “Chukua amri ya watu thelasini kutoka hapa na mtoe Yeremia nabii nje ya kisima kabla hajafa.”
Basi mfalme akamwamuru Ebed-Meleki Mkushi, akisema, “Chukua watu thelathini kutoka hapa pamoja nawe, mkamtoe nabii Yeremia huko kwenye kisima kabla hajafa.”
11 Basi Ebed Meleki alichukua amri ya watu hao na akaenda nyumba ya mfalme, kwenye ghala la nguo chini ya nyumba. Toka hapo alichukua vitambaa na nguo zilizochanika na kuyashusha chini kwa kamba kwa Yeremia ndani ya kisima.
Basi Ebed-Meleki akawachukua watu pamoja naye, wakaenda mpaka kwenye chumba kilichoko chini ya hazina ndani ya jumba la kifalme. Akachukua matambaa makuukuu pamoja na nguo zilizochakaa kutoka huko, na kumshushia Yeremia kwa kamba ndani ya kisima.
12 Ebed Meleki Mkushi alisema kwa Yeremia, “Weka matambara na nguo zilizoraruka chini ya mikono yako na juu ya kamba.” Basi Yeremia alifanya hivyo.
Ebed-Meleki Mkushi akamwambia Yeremia, “Weka haya matambaa makuukuu na hizo nguo zilizochakaa makwapani ili kuzuia kamba.” Yeremia akafanya hivyo,
13 Kisha walimvuta Yeremia kwa kamba. Kwa njia hii walimtoa kutoka kisimani. Basi Yeremia alibaki kwenye uwanja wa mlinzi.
nao wakamvuta juu kwa kamba na kumtoa katika kisima. Yeremia akakaa katika ua wa walinzi.
14 Kisha Mfalme Sedekia alituma neno na kumleta Yeremia nabii kwake, kwenye lango la tatu la nyumba ya Yahwe. Mfalme alisema kwa Yeremia, “Nataka nikuulize kitu. Usinizuilie jibu mimi.”
Ndipo Mfalme Sedekia akatuma watu wamwitie nabii Yeremia wamlete kwake kwenye ingilio la tatu la Hekalu la Bwana. Mfalme akamwambia Yeremia, “Ninataka kukuuliza jambo fulani, usinifiche kitu chochote.”
15 Yeremia alisema kwa Sedekia, “Kama nakujibu, hautaniuawa kwa hakika? Na kama nakupa ushauri, hautanisikiliza mimi.”
Yeremia akamwambia Sedekia, “Nikikupa jibu, je, hutaniua? Hata kama nikikupa shauri, wewe hutanisikiliza.”
16 Lakini Mfalme Sedekia aliapa kwa Yeremia kwa siri na kusema, “Kama Yahwe aishivyo, yeye aliyetufanya sisi, Sitakuuwa au kukuweka kwenye mkono wa watu wale wanaotafuta maisha yako.”
Lakini Mfalme Sedekia akamwapia Yeremia kiapo hiki kwa siri, akisema, “Hakika kama aishivyo Bwana, ambaye ametupa pumzi, sitakuua wala sitakutia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wako.”
17 Kwa hiyo Yeremia alisema kwa Sedekia, “Yahwe, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi: Kama kwa kweli utatoka kwenda kwa maafisa wa mfalme wa Babeli basi utaishi, and mji huu hautachomwa. Wewe na familia yako mtaishi.
Kisha Yeremia akamwambia Sedekia, “Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: ‘Ikiwa utajisalimisha kwa maafisa wa mfalme wa Babeli, maisha yako yatasalimika, na mji huu hautateketezwa kwa moto. Pia wewe na jamaa yako mtaishi.
18 Lakini kama hautaenda kwa maafisa wa mfalme wa Babeli, basi mji huu utachukuliwa kwa mkono wa Wakaldayo. Watauchoma, na hautakwepa kutoka mkono wao.”
Lakini ikiwa hutajisalimisha kwa maafisa wa mfalme wa Babeli, mji huu utatiwa mikononi mwa Wakaldayo na watauteketeza kwa moto, nawe mwenyewe hutaweza kujiokoa mikononi mwao.’”
19 Mfalme Sedekia alisema kwa Yeremia, “Lakini ninaogopa watu wa Yuda waliotoka jangwani kwenda kwa Wakaldayo, kwa sababu nitapewa katika mkono wao, kwa kunifanyia vibaya.”
Mfalme Sedekia akamwambia Yeremia, “Ninawaogopa Wayahudi ambao wamekimbilia kwa Wakaldayo, kwa kuwa Wakaldayo wanaweza kunitia mikononi mwao, nao wakanitenda vibaya.”
20 Yeremia alisema, “Hawatakutoa kwao. Tii ujumbe toka kwa Yahwe ambao ninakuambia, ili kusudi mambo yataenda vizuri kwako, na ili kusudi utaishi.
Yeremia akajibu, “Hawatakutia mikononi mwao. Mtii Bwana kwa kufanya kile ninachokuambia. Kisha utafanikiwa na maisha yako yatakuwa salama.
21 Lakini kama unakataa kutoka, hivi ndivyo Yahwe amenionesha mimi.
Lakini ukikataa kujisalimisha, hili ndilo Bwana alilonifunulia:
22 Tazama! Wanawake wote walioachwa kwenye nyumba yako, mfalme wa Yuda, ataletwa kwa maafisa wa mfalme wa Babeli. Hawa wanawake watasema kwako, “Umedaganywa na rafiki zako; wamekuharibu. Miguu yako sasa imezama kwenye matope, na rafiki zako watakimbia.'
Wanawake wote walioachwa katika jumba la kifalme la mfalme wa Yuda wataletwa mbele ya maafisa wa mfalme wa Babeli. Wanawake hao watakuambia: “‘Walikupotosha na kukushinda, wale rafiki zako uliowaamini. Miguu yako imezama matopeni; rafiki zako wamekuacha.’
23 Kwa kuwa wake zenu wote na watoto wataletwa kwa Wakaldayo, na wewe mwenyewe hautatoroka nchi yao. Utashikwa na mkono wa mfalme wa Babeli, na mji huu utachomwa.”
“Wake zako wote na watoto wataletwa na kutiwa mikononi mwa Wakaldayo. Wewe mwenyewe hutaweza kujiokoa mikononi mwao. Lakini utatekwa na mfalme wa Babeli, na mji huu utateketezwa kwa moto.”
24 Kisha Sedekia alisema kwa Yeremia, “Usimjulishe yeyote kuhusu maneno haya, ili kwamba usije kufa.
Kisha Sedekia akamwambia Yeremia, “Usiruhusu mtu yeyote ajue kuhusu haya mazungumzo, la sivyo utakufa.
25 Kama maafisa wanasikia kwamba nimeongea na wewe- kama wanakuja na kusema kwako, 'Tuambia umezungumza nini pamoja na mfalme. Usitufiche, au tutakuuwa. Na tuambie nini mfalme amesema kwako'-
Maafisa wakisikia kwamba nimezungumza nawe, nao wakakujia na kusema, ‘Tuambie kile ulichozungumza na mfalme na kile mfalme alichokuambia, usitufiche au sivyo tutakuua,’
26 kisha unapaswa kusema nao, “Nilishawishiana pamoja na mfalme asirudi kwangu kwa nyumba ya Yonathan nitakufa humo.”
basi waambie, ‘Nilikuwa ninamsihi mfalme asinirudishe kwenye nyumba ya Yonathani nisije nikafia humo.’”
27 Kisha maafisa wote walikuja kwa Yeremia na kumuuliza, basi aliwajibu kama mfalme alivyomuelekeza. Basi waliacha kuongea pamoja naye, kwa sababu hawakusikia mazungumzo kati ya Yeremia na mfalme.
Maafisa wote wakamjia Yeremia na kumuuliza, naye Yeremia akawaambia kila kitu mfalme alichomwagiza kusema. Kisha hawakusema lolote zaidi na Yeremia kwa sababu hakuna yeyote aliyesikia mazungumzo yake na mfalme.
28 Basi Yeremia alibaki kwenye uwanja wa mlinzi mpaka siku ile Yerusalem ilipotekwa.
Naye Yeremia akabaki katika ua wa walinzi hadi siku Yerusalemu ilipotekwa.