< Yeremia 3 >

1 Wanaema, 'Mwanamume akimfukuza mke wake, naye akaondoka kwake na kuwa mke wa mwanamume mwingine. Je, anaweza kumrudia tena? Je huyo si najisi kabisa?' Huyo mwanamke ndiyo hii nchi! Mmetenda kama kama Kahaba aliye na wapenzi wengi, na sasa mnapenda kurudi kwangu tena? - asema BWANA wa majeshi.
有話說:人若休妻, 妻離他而去,作了別人的妻, 前夫豈能再收回她來? 若收回她來,那地豈不是大大玷污了嗎? 但你和許多親愛的行邪淫, 還可以歸向我。 這是耶和華說的。
2 Inua macho yako uvitazame vielele tasa! Je kuna mahali ambapo hukufanya ukahaba? Pembeni mwa barabara ulikaa ukisubiri wapenzi wako, kama vile Mwarabu jangwani. Uneiharibu nchi kwa ukahaba na uovu wako.
你向淨光的高處舉目觀看, 你在何處沒有淫行呢? 你坐在道旁等候, 好像阿拉伯人在曠野埋伏一樣, 並且你的淫行邪惡玷污了全地。
3 Kwa hiyo chemichemi za mvua zilizuiliwa na mvua za vuli hazikunyesha. Lakini uso wako una kiburi, kama uso wa mwanamke kahaba. Unakataa kuona aibu.
因此甘霖停止, 春雨不降。 你還是有娼妓之臉, 不顧羞恥。
4 Na sasa hutaniita mimi: 'Baba yangu, hata marafiki zangu wa tangu ujanani! Je, atakuwa na hasira dhidi yangu milele?
從今以後,你豈不向我呼叫說: 我父啊,你是我幼年的恩主。
5 Je, utaendelea kuwa na hasira zako?' Tazama! Umesema kuwa utatenda maovu, na kweli umetenda hivyo. kwa hiyo endelea kufanya hivyo!”
耶和華豈永遠懷怒,存留到底嗎? 看哪,你又發惡言又行壞事, 隨自己的私意而行。」
6 Kisha BWANA akanena nami katika siku za mfalme Yosia, “Je, unaona jinsi Israeli alivyoniasi? Yeye anaenda kwenye kila kilima na katika kila mti wenye majani mabichi, na kule anafanya kama mwanamke kahaba.
約西亞王在位的時候,耶和華又對我說:「背道的以色列所行的,你看見沒有?她上各高山,在各青翠樹下行淫。
7 Nikisema, 'Baada ya kuwa amefanya mambo haya yote, atanirudia,' lakini hakurudi. Kisha dada yake Yuda ambaye ni mwasi pia aliona alichokifanya.
她行這些事以後,我說她必歸向我,她卻不歸向我。她奸詐的妹妹猶大也看見了。
8 Kwa hiyo nami nikaona kuwa kwa sababu amefanya uzinzi huu wote. Huyo Israeli aliyeasi! Nilimfukuza na kumpatia talaka ya ndoa. Lakini dada yake Yuda mwenye hiana hakuwa na hofu, na yeye akaenda kuafanya kama mwanamke kahaba!
背道的以色列行淫,我為這緣故給她休書休她;我看見她奸詐的妹妹猶大,還不懼怕,也去行淫。
9 Hukusikitika kuwa ameinajisi nchi, kwa hiyo wakatengeneza sanamu za mti na za jiwe.
因以色列輕忽了她的淫亂,和石頭木頭行淫,地就被玷污了。
10 Kisha baada ya haya yote, wala Yuda dada yake muasi hakurudi kwangu na moyo wake wote, bali alikuja na uongo! -asema BWANA wa majeshi,”
雖有這一切的事,她奸詐的妹妹猶大還不一心歸向我,不過是假意歸我。這是耶和華說的。」
11 Kisha BWANA akanena na mimi, “Israeli muasi amekuwa mwenye haki zaidi kuliko Yuda muasi!
耶和華對我說:「背道的以色列比奸詐的猶大還顯為義。
12 Nenda ukaseme maneno haya huko kaskazini. Uwaambie, 'Rudi wewe Israeli uliyeasi! - asema BWANA - sitakuwa na hasira dhidi yako. Kwa kuwa mimi ni mwaminifu - asema BWANA - sitakuwa na hasira milele.
你去向北方宣告說: 耶和華說:背道的以色列啊,回來吧! 我必不怒目看你們; 因為我是慈愛的, 我必不永遠存怒。 這是耶和華說的。
13 Kiri uovu wako, kwa kuwa umefanya dhambi dhidi ya BWANA, Mungu wako; umemshirikisha njia zako mgeni chini ya kila mti wenye majani mabichi! wala hukuisikiliza sauti yangu! - asema BWANA.
只要承認你的罪孽, 就是你違背耶和華-你的上帝, 在各青翠樹下向別神東奔西跑, 沒有聽從我的話。 這是耶和華說的。
14 Rudini, enyi watu waasi! - asema BWANA - kwa kuwa mimi nimekuoa wewe! Nitakurudisha wewe mmoja katika mji, wawili katika ukoo mmoja, na nitawarudisha Sayuni!
耶和華說:背道的兒女啊,回來吧! 因為我作你們的丈夫, 並且我必將你們從一城取一人, 從一族取兩人,帶到錫安。
15 Nitawapa wachungaji niwapendao, na watawachunga kwa maarifa na ufahamu.
我也必將合我心的牧者賜給你們。他們必以知識和智慧牧養你們。」
16 Ndipo itakapotokea kuwa utaongezeka na kuzaa matunda katika nchi hiyo siku hizo-asema BWANA. Hawataweza kusema kuwa, “Sanduku la agano la BWANA! Jambo hili hawatalikumbuka tena katika mioyo yao, kwa kuwa hawataliwaza tena wala kulijali tena. Usemi huu hawatausema tena.'
耶和華說:「你們在國中生養眾多;當那些日子,人必不再提說耶和華的約櫃,不追想,不記念,不覺缺少,也不再製造。
17 Katiak wakati huo watasema juu ya Yerusalemu, 'Hii ndiyo enzi ya BWANA,' na mataifa mengine yote yatakusanyika Yerusalemu katika jna la BWANA. Hawataishi katika taabu ya uovu wa mioyo yao.
那時,人必稱耶路撒冷為耶和華的寶座;萬國必到耶路撒冷,在耶和華立名的地方聚集。他們必不再隨從自己頑梗的惡心行事。
18 Katika siku hizo, nyumba ya Yuda itaishi na nyumba ya Israeli. Watarudi pamoja kutoka katika nchi ya kaskazini katika nchi niliyowapa mababu wao kuwa urithi.
當那些日子,猶大家要和以色列家同行,從北方之地一同來到我賜給你們列祖為業之地。」
19 Lakini mimi, Nilisema, 'Jinsi nipendavyo kukuheshimu kama mwanangu na kukupa nchi ipendezayo, kuwa urithi mzuri kuliko ulio katika taifa lolote!' Nami nikasema, ''mtaniita baba yangu''.'Nami nitasema kwamba hamtageuka na kuacha kunifuata.
我說:我怎樣將你安置在兒女之中, 賜給你美地, 就是萬國中肥美的產業。 我又說:你們必稱我為父, 也不再轉去不跟從我。
20 Lakini kama mwanamke aliyemwasi mume wake, mmenisaliti, enyi nyumba ya Israeli - asema BWANA.”
以色列家,你們向我行詭詐, 真像妻子行詭詐離開她丈夫一樣。 這是耶和華說的。
21 Sauti ilisikika juu ya nyanda, kilio na kusihi kwa watu wa Israeli! kwa kuwa wamezibadili njia; wamemsahau BWANA, Mungu wao.
在淨光的高處聽見人聲, 就是以色列人哭泣懇求之聲, 乃因他們走彎曲之道, 忘記耶和華-他們的上帝。
22 “Rudini enyi watu mlioasi! Nami nitawaponya na uasi wenu!” “Tazama! tutakuja kwako, kwa kuwa wewe ni BWANA, Mungu wetu!
你們這背道的兒女啊,回來吧! 我要醫治你們背道的病。 看哪,我們來到你這裏, 因你是耶和華-我們的上帝。
23 Uongo hutoka kwenye vilima, kutoka kwenye milima mingi. Kwa hakika wokovu wa Israeli unapatikana kwa BWANA, Mungu wetu.
仰望從小山或從大山的喧嚷中得幫助, 真是枉然的。 以色列得救,誠然在乎耶和華-我們的上帝。
24 Lakini miungu ya aibu imeramba kazi ambayo mababu zetu waliifanya - makundi yao ya kondoo na ng'ombe, wana wao na binti zao!
從我們幼年以來,那可恥的偶像將我們列祖所勞碌得來的羊群、牛群,和他們的兒女都吞吃了。
25 Na tulale chini kwa aibu. Aibu yetu na itufunike, kwa kuwa tumefanya dhambi dhidi ya BWANA, Mungu wetu! Sisi wenyewe na mababu zetu, kutoka wakati wa ujana wetu hadi leo, hatujaisikiliza sauti ya BWANA, Mungu wetu!”
我們在羞恥中躺臥吧!願慚愧將我們遮蓋;因為從立國以來,我們和我們的列祖常常得罪耶和華-我們的上帝,沒有聽從耶和華-我們上帝的話。

< Yeremia 3 >