< Yeremia 27 >

1 Katika mwanzo wa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, neno hil lilimjia Yeremia kutoka kwa Yahwe. (Ingawa nakala nyingi za Kiebrania zinasema “Yehoyakimu, matoleo mengi ya kisasa yanasema “Sedekia”, kwa sababu tukio katika sura hii lilitokea katika kipindi cha utawala wake).
Mwanzoni mwa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, neno hili lilimjia Yeremia kutoka kwa Bwana:
2 Hiki ndicho Yahwe alisema kwangu, “Tengeneza vifungo na nira kwa ajili yako mwenyewe. Ziweke shingoni mwako.
Hili ndilo Bwana aliloniambia: “Tengeneza nira, ujivike shingoni mwako, uifunge kwa kamba za ngozi.
3 Kisha akawatuma kwenda kw mfalme wa Edomu, mfalme wa Moabu, mfalme wa watu wa amoni, mfalme wa Tiro, na kwa mfalme wa Sidoni. Watume kwa mkono wa wajumbe hao wa wafalme ambao walikuja Yerusalemu kwa Sedekia mfalme wa Yuda.
Kisha utume ujumbe kwa wafalme wa Edomu, Moabu, Amoni, Tiro na Sidoni kupitia wajumbe ambao wamekuja Yerusalemu kwa Sedekia mfalme wa Yuda.
4 Toa amri kwao kwa ajili ya mabwana zao na sema, ' Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Hivyo ndivyo utakavyosema kwa mabwana zenu,
Wape ujumbe kwa ajili ya mabwana zao na uwaambie: Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: ‘Waambieni hivi mabwana zenu:
5 Mimi mwenyewe niliiumba dunia kwa nguvu zangu kuu na mkono wangu ulioinuka. Pia niliwaumba watu na wanyama juu ya dunia, na nikawatoa kwa yeyote aliyesahihi katika macho yangu.
Kwa uwezo wangu mkuu na kwa mkono wangu ulionyooshwa nimeumba dunia na watu wake na wanyama walioko ndani yake, nami humpa yeyote inipendezavyo.
6 Kwa hiyo sasa, Mimi mwenyewe naziweka nchi hizi zote kwenye mkono wa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu. Pia, ninavikabidhi kwake viumbe hai vyote katika mashamba ili vimtumikie.
Sasa nitazitia nchi zenu zote mkononi mwa mtumishi wangu Nebukadneza mfalme wa Babeli, na nitawafanya hata wanyama wa mwituni wamtumikie.
7 Kwa maana mataifa yote watamtumikia yeye, wanaye, na wajukuu zake hadi muda wa nchi yake ufike. Kisha mataifa mengi na wafalme wengi watamtiisha.
Mataifa yote yatamtumikia yeye, pamoja na mwanawe na mwana wa mwanawe, hadi wakati wa nchi yake utakapowadia, kisha mataifa mengi na wafalme wenye nguvu nyingi watamshinda.
8 Kwa hiyo taifa na ufalme ambo haumtumikii Nebukadreza, mfalme wa Babeli, na ule usioweka shingo yake chini ya nira ya Nebukadreza mfalme wa Babeli—nitaliadhibu taifa hilo kwa upanga, njaa, na pigo—hili ni tangazo la Yahwe—hadi nitakapokuwa nimewateketeza kwa mkono wake.
“‘“Lakini kama kukiwa na taifa lolote au ufalme ambao hautamtumikia Nebukadneza mfalme wa Babeli, ama kuinamisha shingo yake chini ya nira yake, nitaliadhibu taifa hilo kwa upanga, njaa na tauni, asema Bwana, mpaka nitakapoliangamiza taifa hilo kwa mkono wake.
9 Kwa hiyo msiwasikilize manabii wenu, wabashiri wenu, waonaji wenu, ndoto zenu, watambuzi wenu, ambao wamekuw wakisema kwenu na kusema, ' Msimtumikie mfalme wa Babeli.'
Kwa hiyo msiwasikilize manabii wenu, waaguzi wenu, waota ndoto wenu, watabiri na wachawi wanaowaambia ninyi: Hamtamtumikia mfalme wa Babeli.
10 Kwa maana wanatabiri uongo kwenu ili kuwapeleka mbali na nchi zenu, kwa maana nitawapeleka mbali, na mtakufa.
Wanawatabiria uongo ambao utawafanya ninyi mhamishwe mbali kutoka nchi yenu. Nitawafukuzia mbali, nanyi mtaangamia.
11 Lakini taifa ambalo wataweka shingo zao chini ya nira ya mfalme wa Babeli na kumtumikia, nitawaruhusu kupumzika katika nchi yao—hili ni tangazo la Yahwe—na watailima na kufanya nyumba zao humo.””
Lakini ikiwa taifa lolote litainama na kuweka shingo lake katika nira ya mfalme wa Babeli na kumtumikia, nitaliacha taifa hilo katika nchi yake yenyewe ili wailime na kuishi humo, asema Bwana.”’”
12 Kwa hiyo nilisema kwa Sedekia mfalme wa Yuda na kumpa ujumbe huu, “Ziwekeni shingo zenu chini ya nira ya mfalme wa Babeli na mtumikieni yeye na watu wake, na mtaishi.
Nilitoa ujumbe huo huo kwa Sedekia mfalme wa Yuda. Nilisema, “Ingiza shingo yako katika nira ya mfalme wa Babeli, umtumikie yeye na watu wake, nawe utaishi.
13 Kwa nini mfe—wewe na watu wako—kwa upanga, njaa, na pigo, kama vile nilivyotangaza kuhusu taifa ambalo watapuuza kumtumikia mfalme wa Babeli?
Kwa nini wewe na watu wako mfe kwa upanga, njaa na tauni, ambazo Bwana ameonya juu ya taifa lolote ambalo halitamtumikia mfalme wa Babeli?
14 Msisikilize maneno ya manabii wanaozungumza kwenu na kusema, 'Msimtumikie mfalme wa Babeli', kwa maana wanatabiri uongo kwenu.
Msiyasikilize maneno ya manabii wanaowaambia kwamba, ‘Hamtamtumikia mfalme wa Babeli,’ kwa sababu wanawatabiria uongo.
15 'Kwa maana mimi sikuwatuma—hili ni tangazo la Yahwe—kwa maana wanatabiri uongo katika jina langu ili kwamba niwafukeze inje na muangamie, ninyi nyote na manabii wanaotabiri kwenu.”'
‘Sikuwatuma hao,’ asema Bwana. ‘Wanatabiri uongo kwa jina langu. Kwa hiyo, nitawafukuzia mbali, nanyi mtaangamia, ninyi pamoja na manabii wanaowatabiria.’”
16 Nilitangaza hili kwa makuhani na watu wote na kusema, “Yahwe anasema hivi: Msisikilize maneno ya manabii wanaotabiri kwenu na kusema, 'Angalia! Vyombo vya nyumba ya Yahwe vinarudishwa kutoka Babeli sasa hivi!' Wanatabiri uongo kwenu.
Kisha nikawaambia makuhani na watu hawa wote, “Hili ndilo asemalo Bwana: Msiwasikilize manabii wanaosema, ‘Hivi karibuni sana vyombo vya nyumba ya Bwana vitarudishwa kutoka Babeli.’ Wanawatabiria ninyi uongo.
17 Msiwasikilize. Mtamtumikia mfalme wa Babeli na mtaishi. Kwa nini mji huu uangamizwe?
Msiwasikilize. Mtumikieni mfalme wa Babeli, nanyi mtaishi. Kwa nini mji huu uwe magofu?
18 Kama ni manabii, na kama neno la Mungu limekuja kwao kweli, basi wamwombe Yahwe wa majeshi asivipeleke Babeli vyombo vilivyosalia katika nyumba, nyumba ya mfalme wa Yuda, na Yerusalemu.
Kama wao ni manabii na wanalo neno la Bwana, basi na wamsihi Bwana Mwenye Nguvu Zote ili vyombo vilivyobaki katika nyumba ya Bwana na katika jumba la kifalme la mfalme wa Yuda na katika Yerusalemu visipelekwe Babeli.
19 Yahwe wa majeshi anasema hivi kuhusu zile nguzo, bahari, na kitako, na vyombo vyote vilivyosalia katika mji huu—
Kwa maana hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote kuhusu zile nguzo, ile Bahari, vile vishikizo viwezavyo kuhamishika, vinara na vyombo vingine vilivyoachwa katika mji huu,
20 vyombo ambavyo Nebukadreza mfalme wa Babeli hakuvichukua wakati alipomchukua Yekonia mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, katika utumwa kutoka Yerusalemu kwenda Babeli pamoja na wakuu wote wa Yuda na Yerusalemu.
ambavyo Nebukadneza mfalme wa Babeli hakuvichukua wakati alipomchukua Yekonia mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda kwenda uhamishoni huko Babeli kutoka Yerusalemu, pamoja na wakuu wote wa Yuda na Yerusalemu.
21 Yahwe wa majeshsi, Mungu wa Israeli, anasema hivi kuhusu vyombo vilivyosalia katika nyumba ya Yahwe, nyumba ya mfalme wa Yuda, na Yerusalemu,
Naam, hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo kuhusu vitu ambavyo vimebaki ndani ya nyumba ya Bwana, na ndani ya jumba la kifalme la mfalme wa Yuda, na katika Yerusalemu:
22 'Vitaletwa Babeli, na vitabaki huko hadi siku niyovipangia kutimia—hili ni tangazo la Yahwe—kisha nitavileta na kuvirudisha kataika sehemu hii.”
‘Vitachukuliwa kupelekwa Babeli, nako huko vitabaki mpaka siku nitakayovijilia,’ asema Bwana. ‘Kisha nitavirudisha na kuvirejesha mahali hapa.’”

< Yeremia 27 >