< Yeremia 26 >

1 Mwanzoni mwa utawala wake Yehoyakimu mwana wa Yosia, neno likaja kutoka kwa Yeremia, likisema,
Mwanzoni mwa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, neno hili lilikuja kutoka kwa Bwana:
2 “Yahwe anasema hivi: Simama katika uwanja wa nyumba yangu na sema kuhusu miji yote ya Yuda ambao huja kuabudu katika nyumba yangu. Tangaza maneno yote niliyokuamuru kuyasema kwao. Usipunguze neno lolote!
“Hili ndilo Bwana asemalo: Simama katika ua wa nyumba ya Bwana na useme na watu wote wa miji ya Yuda wanaokuja kuabudu katika nyumba ya Bwana. Waambie kila kitu nitakachokuamuru, usipunguze neno.
3 Labda watasikiliza, kwamba kila mtu ataziacha njia zake mbaya, ili nighairi majanga ninayokusudia kuyaleta juu yao kwa sababu ya uovu wa matendo yao.
Huenda watasikiliza, na kila mmoja akageuka kutoka njia yake mbaya. Kisha nitawahurumia na kuacha kuwaletea maafa niliyokuwa ninapanga kwa sababu ya maovu waliyofanya.
4 Kwa hiyo lazima useme kwao, 'Yahwe anasema hivi: Kama hamtanisikiliza ili mtembee katika sheria yangu ambayo nimeiweka mbele yenu—
Waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Ikiwa hamtanisikiliza na kuifuata sheria yangu ambayo nimeiweka mbele yenu,
5 kama hamsikilizi maneno ya watumishi wangu manabii ambao naendelea kuwatuma kwenu—lakini hamjasikiliza! —
nanyi ikiwa hamtayasikiliza maneno ya watumishi wangu manabii, ambao nimewatuma kwenu tena na tena (ijapokuwa hamkuwasikiliza),
6 kisha nitaifanya nyumba hii kuwa kama Shilo; nitaifanya nyumba hii kuwa laana katika macho ya mataifa yote juu ya dunia.
ndipo nitaifanya nyumba hii kama Shilo na mji huu kuwa kitu cha kulaaniwa na mataifa yote ya dunia.’”
7 Makuhani, manabii, na watu wote wakamsikia Yeremia akitangaza maneno haya katika nyumba ya Yahwe.
Makuhani, manabii na watu wote wakamsikia Yeremia akiyasema maneno haya ndani ya nyumba ya Bwana.
8 Kwa hiyo ikatokea kwamba Yeremia alipomaliza kutangaza aliyokuwa Yahwe alimwwamuru kuyasema kwa watu wote, makuhani, manabii, na watu wote wakamsimamisha na kusema, “Hakika utakufa!
Lakini mara tu Yeremia alipomaliza kuwaambia watu kila kitu Bwana alichomwamuru kukisema, basi makuhani, manabii na watu wote walimkamata wakisema, “Ni lazima ufe!
9 Kwa nini umetabiri katika jina la Yahwe na kusema kwamba nyumba hii itakuwa kama Shilo na mji huu utakuwa ukiwa, pasipo wakaaji?” Kwa maana watu wote wameunda kundi dhidi ya nyumba ya Yeremia.
Kwa nini unatoa unabii katika jina la Bwana kwamba nyumba hii itakuwa kama Shilo na mji huu utakuwa ukiwa na kuachwa tupu?” Nao watu wote wakamkusanyikia na kumzunguka Yeremia ndani ya nyumba ya Bwana.
10 Kisha wakuu wa Yuda wakasikia maneno haya na wakapanda kutoka nyumba ya mfalme kwenda kwenye nyumba ya Yahwe. Wakakaa katika njia ya lango katika Lango Jipya la nyumba ya Yahwe.
Maafisa wa Yuda waliposikia kuhusu mambo haya, wakapanda kutoka jumba la kifalme, wakaenda katika nyumba ya Bwana na kushika nafasi zao kwenye ingilio la Lango Jipya la nyumba ya Bwana.
11 Makuhani na manabii wakasema kwa wakuu wa Yuda na kwa watu wote. Wakasema, “Ni haki kwa mtu huyu kufa, kwa maana ametabiri juu ya mji huu, kama mlivyosikia kwa masikio yenu!”
Kisha makuhani na manabii wakawaambia maafisa pamoja na watu wote, “Mtu huyu anastahili ahukumiwe kifo kwa sababu ametoa unabii mbaya dhidi ya mji huu. Mmesikia kwa masikio yenu wenyewe!”
12 Kwa hiyo Yeremia akasema kwa wakuu wote na watu wote, “Yeremia amenituma kutabiri juu ya nyumb hii na mji wake, kusema maneno yote ambayo mmeyasikia.
Kisha Yeremia akawaambia maafisa wote na watu wote: “Bwana amenituma kutoa unabii dhidi ya nyumba hii na mji huu mambo yote mliyoyasikia.
13 Kwa hiyo sasa, imarisheni njia zenu na matendo yenu, na sikilizeni sauti ya Yahwe Mungu wenu kwamba ataghairi kuhusu janga ambalo ametangaza dhidi yenu.
Sasa tengenezeni njia zenu na matendo yenu, na kumtii Bwana Mungu wenu. Ndipo Bwana atawahurumia na kuacha kuleta maafa aliyokuwa ameyatamka dhidi yenu.
14 Mimi mwenyewe—niangalieni! —niko mikononi mwenu. Nitendeeni yaliyo mema na sahihi katika macho yenu.
Lakini kwa habari yangu mimi, niko mikononi mwenu, nifanyieni lolote mnaloona kuwa ni jema na la haki.
15 Lakini kwa hakika lazima mjue kwamba kama mtaniua mimi, basi mnaiweka damu isiyo na hatia juu yenu wenyewe na juu ya mji huu na wakaaji wake, kwa maana Yahwe amenituma kweli kwenu ili nitangaze maneno yote kwa ajili ya masikio yenu.”
Hata hivyo, jueni kwa hakika, ikiwa mtaniua, mtakuwa mmejipatia dhambi kwa damu isiyo na hatia juu yenu wenyewe, na juu ya mji huu na wote wanaoishi ndani yake, kwa maana ni kweli Bwana amenituma kwenu ili niseme maneno haya yote masikioni mwenu.”
16 Kisha wakuu na watu wote wakasema kwa makuhani na manabii, “Si vyema kwa mtu huyu kufa, kwa maana ametangaza mambo haya kwetu katika jina la Yahwe Mungu wetu.”
Kisha maafisa na watu wote wakawaambia makuhani na manabii, “Mtu huyu asihukumiwe kifo! Amesema nasi katika jina la Bwana, Mungu wetu.”
17 Kisha watu kutoka wazee wa nchi wakasimama na kusema kwa kusanyiko lote la watu.
Baadhi ya wazee wa nchi wakasogea mbele, wakaliambia kusanyiko lote la watu,
18 Wakasema, “Mikaya Mmorashi alikuwa akitabiri katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda. Alinena kwa watu wote wa Yuda na kusema, 'Yahwe wa majeshi anasema hivi: Sayuni utalimwa kama shamba, Yerusalemu utakuwa lundo la magofu, na mlima wa hekalu utakuwa kilima kilichoota vichaka.' Hezekia mfalme wa Yuda na Yunda wote walimuua?
“Mika Mmoreshethi alitoa unabii katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda. Akawaambia watu wote wa Yuda, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “‘Sayuni italimwa kama shamba, Yerusalemu itakuwa lundo la kokoto, na kilima cha Hekalu kitakuwa kichuguu kilichofunikwa na vichaka.’
19 Hakumwogopa Yahwe na kuutaka radhi uso wa Yahwe ili kwamba Yahwe angeghairi kuhusu janga ambalo alilitangaza kwao? Kwa hiyo tutafanya maovu makubwa zaidi juu ya maisha yetu sisi wenyewe?”
Je, Hezekia mfalme wa Yuda au mtu mwingine yeyote katika Yuda alimhukumu Mika kufa? Je, Hezekia hakumcha Bwana na kuhitaji msaada wake? Je, Bwana hakuwahurumia na akaacha kuleta maafa aliyokuwa ametamka dhidi yao? Tunakaribia sana kujiletea maangamizo ya kutisha sisi wenyewe!”
20 Wakati huo huo palikuwa na mtu mwingine ambaye alitabiri katika jina la Yahwe—Uria mwan wa Shemaya kutoka Kiriath Yearimu—pia alitabiri juu ya mji na nchi hii, akikubaliana na maneno yote ya Yeremia.
(Wakati huu, Uria mwana wa Shemaya kutoka mji wa Kiriath-Yearimu alikuwa mtu mwingine aliyetoa unabii kwa jina la Bwana. Alitoa unabii juu ya mambo yaliyofanana na haya dhidi ya mji huu na nchi hii kama alivyofanya Yeremia.
21 Lakini Mfalme Yohoyakimu na wanajeshi wake wote na watumishi wake wote waliposikia maneno yake, kisha mfalme alijaribu kumuua, lakini Uria alisikia na kuogopa, kwa hiyo alikimbia na akaenda Misiri
Mfalme Yehoyakimu na wakuu wake wote na maafisa waliposikia maneno yake, mfalme alitafuta kumuua. Lakini Uria alipata habari, na kwa kuogopa akakimbilia Misri.
22 Kisha mfalme Yehoyakimu alituma watu kwenda Misiri—Elnathani mwana wa Achbori na watu kwenda Misiri kumfuata Uria.
Hata hivyo, Mfalme Yehoyakimu alimtuma Elnathani mwana wa Akbori huko Misri, pamoja na watu wengine ili kwenda kumkamata Uria.
23 Wakamtoa Uria nje kutoka Misiri na kumleta kwa Mfalme Yehoyakimu. Kisha Yehoyakimu akamuua kwa upanga na kumpeleka nje kwenye makaburi ya watu wa kawaida.
Wakamrudisha Uria kutoka Misri na kumpeleka kwa Mfalme Yehoyakimu, ambaye alimuua kwa upanga, na mwili wake kutupwa kwenye eneo la makaburi ya watu wasio na cheo.)
24 Lakini mkno wa Ahikamu mwana wa Shapni alikuwa pamoja na Yeremia, hivyo hakutiwa mikonono mwa watu ili auawe.
Zaidi ya hayo, Ahikamu mwana wa Shafani akamuunga mkono Yeremia, kwa hiyo hakutiwa tena mikononi mwa watu ili auawe.

< Yeremia 26 >