< Yeremia 19 >

1 Bwana akasema hivi, “Nenda ukanunue chupa ya udongo wakati ukiwa na wazee wa watu na makuhani.
כה אמר יהוה הלך וקנית בקבק יוצר חרש ומזקני העם ומזקני הכהנים
2 Kisha uende mpaka bonde la Ben Hinomu wakati wa kuingia kwenye mlango uliovunjika wa mfinyanzi, na huko utangaza maneno nitakayokuambia.
ויצאת אל גיא בן הנם אשר פתח שער החרסות (החרסית) וקראת שם את הדברים אשר אדבר אליך
3 Ukisema, 'Sikilizeni neno la Bwana, wafalme wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu! Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, “Tazameni, na nitaletea msiba juu ya mahali hapa, na masikio ya kila mtu anayesikia yatawaka.
ואמרת שמעו דבר יהוה מלכי יהודה וישבי ירושלם כה אמר יהוה צבאות אלהי ישראל הנני מביא רעה על המקום הזה אשר כל שמעה תצלנה אזניו
4 Nitafanya hivyo kwa sababu wameniacha na kudharau mahali hapa. Katika mahali hapa wanatoa sadaka kwa miungu mingine ambayo hawakuijua. Wao, baba zao, na wafalme wa Yuda pia wamejaza mahali damu isiyo na hatia.
יען אשר עזבני וינכרו את המקום הזה ויקטרו בו לאלהים אחרים אשר לא ידעום המה ואבותיהם ומלכי יהודה ומלאו את המקום הזה דם נקים
5 Walimjengea Baali mahali pa juu na kuwachoma watoto wao kwa moto kama sadaka za kuteketezwa kwake-kitu ambacho sijawaamuru au kutaja, wala hakuingia ndani ya akili yangu.
ובנו את במות הבעל לשרף את בניהם באש--עלות לבעל אשר לא צויתי ולא דברתי ולא עלתה על לבי
6 Kwa hiyo, tazama, siku zinakuja-hili ndilo tamko la Bwana-ambapo mahali hapa hapataitwa tena Tofethi, bonde la Ben Hinomu, kwa kuwa litakuwa bonde la machinjo.
לכן הנה ימים באים נאם יהוה ולא יקרא למקום הזה עוד התפת וגיא בן הנם--כי אם גיא ההרגה
7 Katika mahali hapa nitatamgua mipango ya Yuda na Yerusalemu. Nitawafanya wapate kuuawa kwa upanga mbele ya adui zao na kwa mkono wa wale wanaotafuta maisha yao. Ndipo nitawapa miili yao kuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa dunia.
ובקתי את עצת יהודה וירושלם במקום הזה והפלתים בחרב לפני איביהם וביד מבקשי נפשם ונתתי את נבלתם למאכל לעוף השמים ולבהמת הארץ
8 Ndipo nitaifanya mji huu kuwa uharibifu na kitu cha kuzomewa, kila mtu anayepita atashangaa na kuzomea kwa sababu mateso yake yote.
ושמתי את העיר הזאת לשמה ולשרקה כל עבר עליה ישם וישרק על כל מכתה
9 Nitawafanya wale nyama ya wana wao na binti zao; kila mtu atakula mwili wa jirani yake katika dhiki na katika uchungu ambao umeletwa kwao na maadui zao na wale wanaotaka maisha yao.'”
והאכלתים את בשר בניהם ואת בשר בנתיהם ואיש בשר רעהו יאכלו במצור ובמצוק אשר יציקו להם איביהם ומבקשי נפשם
10 Kisha utavunja chupa ya udongo mbele ya watu ambao walikwenda pamoja nawe.
ושברת הבקבק--לעיני האנשים ההלכים אותך
11 Uwaambie,'Bwana wa majeshi asema hivi: nitafanya jambo hili kwa watu hawa na mji huu- hii ndiyo ahadi ya Bwana, kama vile Yeremia alivyovunja chupa ya udongo ili isiweze kutengenezwa tena. Watu watazika wafu huko Tofethi hata hapatabaki mahali pa kuzika.
ואמרת אליהם כה אמר יהוה צבאות ככה אשבר את העם הזה ואת העיר הזאת כאשר ישבר את כלי היוצר אשר לא יוכל להרפה עוד ובתפת יקברו מאין מקום לקבור
12 Hivyo ndivyo nitakavyopafanya mahali hapa na wenyeji wake nitakapofanya jiji hili kama Tofethi, hili ndio tamko la Bwana;
כן אעשה למקום הזה נאם יהוה--וליושביו ולתת את העיר הזאת כתפת
13 kwa hiyo nyumba za Yerusalemu na wafalme wa Yuda watakuwa kama Tofethi, nyumba zote zilizo juu ya watu waovu wanaoabudu nyota zote za mbinguni na kumwaga sadaka za kinywaji kwa miungu mingine.'”
והיו בתי ירושלם ובתי מלכי יהודה כמקום התפת הטמאים--לכל הבתים אשר קטרו על גגתיהם לכל צבא השמים והסך נסכים לאלהים אחרים
14 Ndipo Yeremia akatoka Tofethi, ambako Bwana amemtuma ahubiri. Akasimama katika ua wa nyumba ya Bwana, akawaambia watu wote,
ויבא ירמיהו מהתפת אשר שלחו יהוה שם להנבא ויעמד בחצר בית יהוה ויאמר אל כל העם
15 “Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazameni, nitawaletea mji huu na miji yake yote maafa yote niliyonena dhidi yake, kwa kuwa walifanya shingo zao kuwa ngumu na kukataa kusikiliza maneno yangu.'”
כה אמר יהוה צבאות אלהי ישראל הנני מבי אל העיר הזאת ועל כל עריה את כל הרעה אשר דברתי עליה כי הקשו את ערפם לבלתי שמוע את דברי

< Yeremia 19 >